Nandagala One
JF-Expert Member
- Aug 19, 2020
- 2,461
- 2,897
Wana JF , Heshima kwenu!!
Moja kwa moja kwenye mada,
Leo katika Bunge alipokuwa anachangia hoja juu ya bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu ,Ndugu Simon Songe,umetumia muda mwingi kumsifia waziri Mkuu, huku ukiwataka wakazi wa Lindi mintarafu Ruangwa kumwamini Waziri Mkuu,ukirejea kuwa kaleta maendeleo kwenye halmashauri mbalimbali nchini.
Ukiangalia vizuri,umejenga hoja dhaifu sana, iliyojaa uchawa ndani yake.
Kwanini nasema uchawa, kwanini wewe kutoka Jimbo la Busega kaskazini mwa Tanzania uwatake watu wa Ruangwa kusini mwa Tanzania wawe na imani na Waziri mkuu??
aghalabu kauli kama hiyo ingalitegemewa itolewe na wabunge wa kusini mwa Tanzania hasa majimbo jirani ya Nachingwea, Mtama, Masasi, na hata Liwale, Nina uhakika Nape Mnauye angekuwa mtu wa kwanza kupongeza kuhusu Waziri Mkuu.
Kauli yako ya kumsifia na kumpigia upatu waziri mkuu Majaliwa "Mjomba " siyo Yako,ipo kimkakati, huenda umepangwa ,hasa mwenyewe mhusika kutokuwa na mahusiano mema na wabunge wa kusini, ambao ingependeza hizo sifa bandia ambazo mimi naziiita "PAMBIO ZA KUSIFU NA KUABUDU " kama zingalifanywa na wabunge wa Kusini.
Hivi wewe ni lini ulitumwa na wana Ruangwa kuwasemea?? Je wenyewe wana Ruangwa hawajui?? hawaoni?? aliyoyafanya??
Je kwanini kauli hii unaleta wakati bunge linaelekea kumaliza muda wake???
Usichokijua kuhusu Waziri Mkuu na Mbunge wa Ruangwa,ni kwamba ili aweze kugombea anapaswa kutangaza Nia ya kugombea.
Tangazo lake la kuwa anagombea kwa ajili 2025 ni batili, maana lilikuwa Lina vinasaba vya kupita bila kupingwa ndani ya chama, na Viongozi akiwemo Mwenyekiti wa CCM Ruangwa kuwa watatoa fomu Moja tu.
Fomu Moja sasa haiwezekani, msimamo wa CCM ni hakuna mgombea kupita bila kupingwa.
Mbunge wa Busega uliyeamua au uliyekubali kufanywa chawa wa Waziri Mkuu Majaliwa, unawakosea sana haki watu wa Ruangwa,nikiwemo mimi Nandagala one niliyeko huku Afrika kusini.
Waziri Mkuu Majaliwa alifanya alichoweza ndani ya Ruangwa,na sasa imetosha, anapaswa kumsaidia Mama yetu Dr Samia ajiteulie waziri mkuu Mwingine 2025 October baada ya Uchaguzi mkuu.
Waziri Mkuu ameshindwa kuwaunganisha wabunge wa kusini kwenye majimbo zaidi ya 30,Wakawa na kauli moja kuhusu Maendeleo ya kusini.
Anaondoka akiwa ameshindwa kutengeneza mazingira ya locked district Liwale kujenga barabara ya lami Toka Nachingwea mpaka Liwale, lakini Liwale mpaka Kilwa Nangurukulu.
Mwisho Mwishoni watu wa Ruangwa wanataka mabadiliko,ushahidi ni mapokezi makubwa aliyoyapata Tundu Antipas Lissu, Kwenye ziara yake siku chache zilizopita katika "No Reforms No Election "
Ile ilikuwa ni dalili ya wana Ruangwa kuchoka na kutamani kuwa na mtu mwingine wa kuwasemea bungeni.
Mwisho Mwishoni Namuomba Waziri Mkuu asome alama za nyakati, kugombea na kurudi bungeni akae back bencher, ni aibu na fedheha.
Ungemshauri baada ya muda kwisha apunzike kama mzee wetu mizengo pinda ambaye analima zabibu na na kufuga nyuki, mbali ya pensheni nzuri.
🙏🙏🙏
Nandagala One -Mpumalanga South Africa.