Mbunge wa Bunda na mwenyekiti wa CCM washikiliwa na polisi kwa uchochezi uliosababisha mauaji ya watu wawili!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,847
141,769
Mbunge wa Bunda na mwenyekiti wa CCM wilayani humo wanashikiliwa na polisi kwa uchochezi uliopelekea mauaji ya watu wawili. Pia wananchi takribani 49 wamekamatwa kwa kudaiwa kutekeleza mauaji hayo. Mkuu wa mkoa wa Mara Adamu Malima amesema hakuna mtu hata mmoja aliyehusika kwa namna yeyote ile kufanikisha mauaji hayo atakayekwepa mkono wa sheria. Malima amesema hata wale waliosababisha mauaji hayo wakiwa nyuma ya pazia watashughulikiwa na jeshi la polisi kwa mujibu wa sheria. Source Star Tv habari!
 
Inawezekana Yuko Sawa, wahusika ni wa vyama hasimu, kwa Maana ya CCM na Chadema mfarakano wao umesababisha mauaji hayo, hivyo lazima wote waisaidie polisi
 
Ana maanisha mbunge wa Bunda ambaye pia ni mwenyekiti wa ccm wa wilaya ya Bunda!
 
Back
Top Bottom