Mbunge wa Bahi (CCM) ashikiliwa na polisi kwa kuomba rushwa

Naam,

Nimeiboresha title na content naona mwenzetu amesahau kama hii ni JF.

Lakini, kiasi chenyewe inadaiwa hakifikii hata 5mil, achilia mbali 7mil. What a shame?


Kwa hiyo hicho kiasi kingefika zaidi ya 5mil achilia mbali 7mil isingekuwa aibu?
 
Huo ni ushahidi kuwa Kamati za Bunge nazo siyo safi. Niliwahi kuwa katika ujumbe wa wabunge tukatembelea viwanda viwili vya sukari mkoani Morogoro mbali na wabunge kupewa sukari gunia moja kila mmoja pia walipewa bahasha za sh mil 1 katika kila kiwanda. Waratibu wa mambo hayo walikuwa PSRC.
Nani kabaki salama katika suala la rushwa? Na je, kama atapelekwa mahakamani, je, ataendelea na ubunge na tuhuma za jinai kama hizi?
 
Huyu jamaa namfahamu siku nyingi zilizopita. Siku moja nilikuwa pale parokiani wakati wa kampeni mwaka 2010. Yeye alifika pale na kutoa pesa kama sadaka. Nilichoshangaa yeye si muumini lakini alifanya hivyo. Pia aliahidi kuvuta umeme kwa ajili ya parokia ya Bahi. Aliahidi kuanzisha shule ya ufundi pale parokiani na mambo mengine mengi. Mimi nilishangaa sana, atatoa wapi hela zote hizo. Kwenye misikiti pia alifanya vivyo hivyo. Hata hivyo kimoonekano nilibaini kwamba si mtu mwenye uzalendo hata kidogo.
Namwomba Mungu azidi kutufichulia mambo haya. Kwani sasa tunataka kuijenga nchi na si kuibomoa nchi.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Nimemsikia live leo mkurugenzi mmoja wa PCCB clouds fm akisema kuwa wanamshikiria badwel kwa kupokea rushwa ya mil 1 kwa afisa wa mkuranga...bedwel aliomba mil 7 ila jamaa akampa mil 1....so ni kashikwa live..... na walishikwa hotel ya peacock...
 
huyu mtu aliwahi kutuhumiwa na mhs d.kafulila ,sasa yamitimia nasubiri kuona kama mahakama yetu itatenda haki kwa hii kesi ya ccm.
 
Sasa serikali imepania kutonyesha kuwa inaweza,hebu ngoja tuone mwisho wake maana kanaweza kuwa kamchezo flani kakuigiza.
 
kuna uwajibikji na utawala bora kwelli? kafulila alisha eleza bungeni mwaka jana kuwa baadhai ya wabunge ambao ni wajumbe wa kamati ya LAAC wanaomba na kupokea rushwa. hivi posho na marupurupu manoono hayawatoshi tu. Mbunge huyu hayupo kwa kusimamia maendeleo na maslahi ya wananchi bali anajali maslahi yake kwa kuangamiza jamii.
 
Watu wanapopotosha ukweli, nilivyosikia mimi ni kuwa Badwel ndiye aliyewajulisha TAKUKURU kuwa kuna watu wanataka kumhonga na akawapa saa na mahala walipoahidiana kukutana. Sasa vipi tena kibao kigeuzwe kwake?


Mfungo aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa wanaendelea kumshikilia huku wakati wanafanya uchunguzi hadi kesho ambapo watamfikisha mahakamani.

"Siwezi kumataja aliyekuwa akitoa rushwa kwa sababu bado tunaendelea na upelelezi, ila mpaka sasa yuko mahabusu na tutamfikisha mahakamani Jumatatu(kesho)," alisema Mfungo.

Alisema kuwa mbali na kumfikisha mahakamani, pia watatoa taarifa zaidi za tukio hilo kesho.
Jamani anieleweshe kati zomba na Mfungo (aliyenukuliwa na mtoa habari) nani yuko sahihi?.
 
akichaguliwa kiongozi maskini rushwa ndio usiseme (njaa),akichaguliwa kiongozi tajiri dili kwake kama kawa (heshima),so kwa dili alilo-semekana kulilamba mh. mbunge ni dhaili kwa nafasi yake anaonesha njaa kali..roho maskini.......wakati mwingine nsijisumbue kuomba uongozi ili hali uwezo (capability) na subila (tolerance) hamnazo.step down honoroble.
 
Sio kwa sababu posho ni ndogo, ni kwa sababu amezoea kuiba, kama sio hivyo ni kwa sababu wanataka kutanua zaidi ya uwezo wa nchi yao, nani alipie gharama za anasa na vyangudoa?
 
Ni aibu sana kwa Mbunge kushtakiwa kwa rushwa ya 5 Mil. This is Tanzania bwana

Si bora hata ingekua 5mil. NI SHILINGI ZA KITANZANIA MILIONI MOJA TASILIMU (TZS 1,000,000/=) ndo zilizomkamatisha. Kweli hizi ni njaa!!Hio si ni 'Sitting Allowance' ya pale mjengoni siku tatu tu!!!
 
Back
Top Bottom