Mbunge wa Bahi (CCM) ashikiliwa na polisi kwa kuomba rushwa

Kwa sasa rushwa ni jambo la kawaida, kama ilivyo kawaida kuiba rasilimali za umma.
Akikamatwa mmoja inaonekana amehujumiwa tu, kwani kila mmoja nae anakula.
Ukilalamikia rushwa unaonekana kituko kabisa!
Bila kuondoa mfumo mzima itabaki hivihivi, kama haijaongezeka.....
 
Dah jamaa kanaswa mbaya! Lakini yeye kaotewa tu maana maeneo kibao wanakula rushwa tena za mabilioni.
Huyu nae kazidi, anakwenda kudai rushwa mpaka toka kwa maskini! Kweli CCM hamna kitu wanaacha kwa sasa, wataanza kuomba mpaka rushwa ya buku sasa kama wakiona huna kabisa hela ya kuwapa.
 
Hivi katika makosa ya rushwa ni nini tofauti ya uzito wa kosa kati ya kudai rushwa na kuomba rushwa?
 
Juma kidogo, swali lako zuri sana.... nalijibu kama ifuatavyoooo

mimi nimwajiriwa, na bosi wangu ni mwajiriwa, bosi wake bosi wangu ameteuliwa na mkuu.... therefore all our cases lazima yakidhi matakwa ya mkuu.... la sivyo by default wote hatuna kazi....

sasa hivi wakuu hawaelewani....yani wanafanyiana wenyewe ubaya...sisi tunatumika kama wakandamizaji....kwahiyo, saizi utaona ukali wetu

kaka majasho
nakupongeza sana kwa ujasiri wako,ni kweli wakuu wao hujiweka pembeni na kuwatumia wachini yake kukandamizi baadhi ya watu na mwisho wa siku wanaoumia ni watu kama nyie mnaopokea maelekezo na kuyafanyia kazi wakati yeye kama mkuu akipona na kusaga raha mjini
tuamke sasa na tuseme HAPANA kutumika kama kiti cha kukalia,komaeni nao hao wote wasiotaka nyie mfanye kazi kwa maslahi ya taifa ila kwa maslahi yao na kuwakandamizi wasio na hatia
 
Kama hii ni kweli basi ni dhahiri mfumo wetu umefika pabaya sana. Tazama halmashauri zetu zilivyo maskini, nasema maskini kwa sababu ndo zina respond kwenye matatizo ya wananchi with immediate effect. When you talk about Zahanati, shule, majosho, barabara, n.k unazungumzia halmashauri kwa maana ya wataalam na madiwani mbunge akiwa mmojawao.
Mbunge licha ya kulijua hili na licha ya kupewa kila aina ya vitendea kazi na maslahi bora yeye ndo wa kwanza kuomba rushwa ili kile kidogo cha maendeleo kwa ajili ya wananchi maskini kimfae yeye peke yake. Sasa naanza kudhani kuwa ndo maana hawaruhusu adhabu ya kuwanyonga watu wa aina hii. Tumshitaki wapi huyu?
 
Ni tabia yake na siyo kwamba posho hazitoshi afu tena ni kutoka kwa magamba ni kawaida yao!
 
Hivi milion 5 unaweza kuita ni rushwa? tena kwa mbunge?

Kuna watu wanataka kumchafua tu muheshimiwa, ila Kaaibisha jamii yake kama "ikithibitika"
mbona huna msimamo? mara unasema million 5 haiweizi kuitwa rushwa, na ukaenda mbali kumsafisha mtuhumiwa kabla hata ya takukuru hii taasisi ta ccm kumchunguza mwanachama mwenzao kuwa anachafuliwa cha ajabu unahitimisha kuwa ikithibitika atakuwa ameabisha! conclusion yako inaonyesha unataka jamii ielewe hajapokea rushwa ila moyoni kwako unajua kuwa uwezekano wa kupokea rushwa upo ndio maana unaanza kuwa na wasiwasi ikithibitika ni aibu!!
 
Alex Mfungo huyu si yule aliyechukua rushwa ya bilioni moja kwa Subhash Patel(MM Integrated) na akaondolewa kwenye iyo nafasi? yaani amerudishwa tena kwenye nafasi ya ukuu wa uchunguzi? lazima hapa kuna jambo kati yake na Hosea....Majasho naomba ujibu swali langu
 
Hivi milion 5 unaweza kuita ni rushwa? tena kwa mbunge?

Kuna watu wanataka kumchafua tu muheshimiwa, ila Kaaibisha jamii yake kama "ikithibitika"
Kwani ili iwe rushwa inatakiwa iwe shilingi ngapi? inaonekana wewe mwenzetu ni mzoefu wa rushwa kama mwana CCM vile!
 
NI OMARY BADWEL WA JIMBO LA BAHI, KUBURUZWA MAHAKAMNI KESHO
Neville Meena na Fidelis Butahe
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inamshikilia Mbunge wa Jimbo la Bahi (CCM), Omary Badwel kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Sh1 milioni kutoka kwa kiongozi wa Serikali.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa taasisi hiyo, Alex Mfungo zinaeleza kuwa Badwel alikamatwa na maofisa wa Takukuru jana saa 9:00 alasiri katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.

Badwel ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) anadaiwa kukamatwa wakati anapokea rushwa kutoka kwa maafisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkurunga mkoani Pwani jana.

Mfungo aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa wanaendelea kumshikilia huku wakati wanafanya uchunguzi hadi kesho ambapo watamfikisha mahakamani.

“Siwezi kumataja aliyekuwa akitoa rushwa kwa sababu bado tunaendelea na upelelezi, ila mpaka sasa yuko mahabusu na tutamfikisha mahakamani Jumatatu(kesho),” alisema Mfungo.

Alisema kuwa mbali na kumfikisha mahakamani, pia watatoa taarifa zaidi za tukio hilo kesho.

Naye Katibu wa Bunge, Thomas Kashilillah alilithibitishia gazeti hili jana kukamatwa mbunge huyo na kwamba wanasubiri taarifa zaidi kutoka Takukuru kuhusiana na suala hilo.

“Nimepata taarifa ya kukamatwa kwa Badwel, lakini sina taarifa za ndani nasubiri wenzetu wa Takukuru watupe ufafanuzi zaidi,” alisema Kashillilah.

Wakati mbunge huyo akikamatwa jana, Mwenyekiti wa Kamati ya LAAC, Augustine Mrema alikuwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akielekea Uingereza.

Bedwel ni mmoja kati ya wabunge wawili waliotajwa na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR Mageuzi) katika Bunge la Bajeti mwaka jana kwamba waliomba rushwa katika halmashauri ambayo hakuitaja.

Akichangia Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano, Kafulila aliwataja bungeni Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi na Mbunge wa Bahi, Omary Badwel wote wa CCM akidai kwamba aliwakuta wakiomba rushwa kwa viongozi wa halmashauri.

Wakati akitaja majina hayo, Kafulila nusra aingie katika mgogoro na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge, George Simbachawene ambaye alikuwa akimwamuru kukaa chini kutokana na muda wake wa kuchangia kumalizika. Hivi sasa Simbachawene ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini.

Wakati Simbachawene akimwamuru akae chin, Kafulila alikuwa akiendelea kuzungumza bila kujali kengele ya pili iliyopigwa kuashiria kwamba muda wake ulikuwa umekwisha.

"Mheshimiwa Mwenyekiti kwa wakati wa sasa ni vigumu kusimamia matumizi kwani mfumo wetu wa uongozi unaruhusu ufisadi, wapo viongozi, mawaziri, wabunge wanaomba rushwa...." alisema Kafulila na kuamsha zogo ambalo liliambatana na sauti zisizo rasmi katika ukumbi wa Bunge zikiuliza ".....wapo humu humu?" Kafulila alijibu "Ndiyo..."

Sauti moja ilisema wataje, hapo ndipo aliposema "....Wapo kina Zambi, Badwel, niliwakamata na nilichukua hatua, hatuwezi kuendelea namna hii," kisha akaketi.

Baada ya dakika chache tangu alipoketi, Kafulila alionekana akiteta jambo na Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali na Augustine Mrema wa Vunjo na baadaye Mkosamali aliomba mwongozo wa Mwenyekiti wa Bunge, akitaka waliotuhumiwa watajwe ili wafahamike vizuri.

Zambi na Badwel ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa pamoja na Kafulila chini ya Mwenyekiti wao, Mrema.

Mwenyekiti wa Bunge, Simbachawene akijibu hoja hiyo alisema atatoa mwongozo wake baadaye, katika muda ambao ataona unafaa. Hata hivyo, hadi sasa hakuna mwongozo ambao umetolewa na bunge kuhusiana na kauli ya Kafulila.

Naibu Spika

Kauli ya Naibu Spika, Job Ndugai alisema taarifa ya tuhuma za rushwa kwa wabunge ziliwahi kutolewa katika kikao cha Kamati ya Uongozi na Mrema, ijapokuwa majina ya watuhumiwa na mlalamikaji hayakutajwa.

Kafulila aliwahi kukaririwa akieleza kuwa tayari taarifa za tuhuma hizo za rushwa zilikuwa zimefikishwa kwa Spika kwa maandishi pamoja na Mrema kwa ajili ya hatua zaidi.

Kadhalika, Mbunge huyo alisema taarifa hizo zilikuwa zimekwishawafikia viongozi wa juu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na kwamba aliwahi kukutana na Spika kuhusu suala hilo ijapokuwa hakukuwa na hatua zozote ambazo zilichukuliwa.
Wakati hayo yakiendelea Habari zilizopatikana jana kutoka kwa watu walio karibu na Kafulila zimeeleza kuwa huenda leo mbunge huyo akafanya mkutano na waandishi wa habari na kuanika uozo uliopo katika kamati hiyo.



SOURCE: MWANANCHI OF 03/06/2012
 
Mbona wakina Badwel wako wengi sana kwa nini yeye tu? au alikuwa na bifu na kigogo mwenzake? Majasho hebu weka details maana ninavyojua ccm hakuna msafi wote wananuka rushwa
 
... Lakini, kiasi chenyewe inadaiwa hakifikii hata 5mil, achilia mbali 7mil. What a shame?
Mkuu kwani wewe huwa unapokea rushwa ya kuanzia shilingi ngapi? Ni swali tu kutokana na dharau ya 5m, ila naomba usinipe ban

 
Juma kidogo, swali lako zuri sana.... nalijibu kama ifuatavyoooo

mimi nimwajiriwa, na bosi wangu ni mwajiriwa, bosi wake bosi wangu ameteuliwa na mkuu.... therefore all our cases lazima yakidhi matakwa ya mkuu.... la sivyo by default wote hatuna kazi....

sasa hivi wakuu hawaelewani....yani wanafanyiana wenyewe ubaya...sisi tunatumika kama wakandamizaji....kwahiyo, saizi utaona ukali wetu

Kwa hiyo mkuu Majasho ina maana kuwa huhu mbunge amekamatwa tu kwa kuwa kuna matakwa ya mtu fukani yanataka yatimizwe? Hivi Mkuu wa wilaya ya Bahi ni nani? Just curious!! Connect the dot from zea? Ila nimekupenda umekuwa muwazi hapa maana ninajua kuna rusha grand/corporate na wahusika wanafahamika but no mtego wa kukamata but huyu wa 7m ambaye pengine amefanikiwa kuletewa downpayment ya 1m ndo kawa kafara!!! But hicho chama chenu cha magamba ya kobe wa miaka 300 si ukweli ndo kinaongoza kwa rushwa? Nilitegemea hata uchaguzi wa wabunge wa East Africa ni lazima wangeshikiliwa kadhaa but rushwa was nje nje kabila, halalishwa!!! TAKUKURU has a long way to go to prove to Tanzanians of your credibility!!! mmeshaipoteza. Fanyeni kweli ili muirudishe!!
 
Kwa hiyo mkuu Majasho ina maana kuwa huhu mbunge amekamatwa tu kwa kuwa kuna matakwa ya mtu fukani yanataka yatimizwe? Hivi Mkuu wa wilaya ya Bahi ni nani? Just curious!! Connect the dot from zea? Ila nimekupenda umekuwa muwazi hapa maana ninajua kuna rusha grand/corporate na wahusika wanafahamika but no mtego wa kukamata but huyu wa 7m ambaye pengine amefanikiwa kuletewa downpayment ya 1m ndo kawa kafara!!! But hicho chama chenu cha magamba ya kobe wa miaka 300 si ukweli ndo kinaongoza kwa rushwa? Nilitegemea hata uchaguzi wa wabunge wa East Africa ni lazima wangeshikiliwa kadhaa but rushwa was nje nje kabila, halalishwa!!! TAKUKURU has a long way to go to prove to Tanzanians of your credibility!!! mmeshaipoteza. Fanyeni kweli ili muirudishe!!

anaitwa betty mkwasa,,,,unamhusishaje????maana jamaa amekamatiwa dar,,,,alidai mkuranga
 
Hivi milion 5 unaweza kuita ni rushwa? tena kwa mbunge?

Kuna watu wanataka kumchafua tu muheshimiwa, ila Kaaibisha jamii yake kama "ikithibitika"

Rushwa ni rushwa Mura! We kwa akili yako rushwa huwa inaanzia shilingi ngapi? Kuna watu wanatumikia miaka saba kisa walipokea TShs Elfu kumi na tano tu!

Chonde chonde TAKUKURU, kamati hii imekuwa ikilalamikiwa sana kupokea rushwa toka halmashauri. Mzee mrema kalalamika na kafulila kalalamika bungeni kuwa wenzake wanawageuka kwenye kamati. TAKUKURU kwa hili tunajua DPP hatahusika hivyo tusisikie kisingizio cha DPP.
 
Mimi kila siku nasema posho za wabunge hazitoshi

Mbunge wa Bahi (CCM) anashikiliwa na polisi na atafikishwa kizimbani J3 kwa tuhuma za kuomba rushwa ya 7 mil. Mbunge huyu yupo kwenye kamati ya MH. A L Mrema ya LAAC.

Habari za undani zinakuja, upelelezi wa takukuru unaendelea.

=======

Neville Meena na Fidelis Butahe | Mwananchi | June 3, 2012

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inamshikilia Mbunge wa Jimbo la Bahi (CCM), Omary Badwel kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Sh1 milioni kutoka kwa kiongozi wa Serikali.


Kumbe ni tuhuma..! Nilidhani kashikwa nazo mkononi....du.!???
 
Back
Top Bottom