Mbunge wa Bahi (CCM) ashikiliwa na polisi kwa kuomba rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge wa Bahi (CCM) ashikiliwa na polisi kwa kuomba rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Majasho, Jun 2, 2012.

 1. M

  Majasho JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2012
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mimi kila siku nasema posho za wabunge hazitoshi

  Mbunge wa Bahi (CCM) anashikiliwa na polisi na atafikishwa kizimbani J3 kwa tuhuma za kuomba rushwa ya 7 mil. Mbunge huyu yupo kwenye kamati ya MH. A L Mrema ya LAAC.

  Habari za undani zinakuja, upelelezi wa takukuru unaendelea.

  =======

  Neville Meena na Fidelis Butahe | Mwananchi | June 3, 2012

  TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inamshikilia Mbunge wa Jimbo la Bahi (CCM), Omary Badwel kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Sh1 milioni kutoka kwa kiongozi wa Serikali.

  Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa taasisi hiyo, Alex Mfungo zinaeleza kuwa Badwel alikamatwa na maofisa wa Takukuru jana saa 9:00 alasiri katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.

  Badwel ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) anadaiwa kukamatwa wakati anapokea rushwa kutoka kwa maafisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkurunga mkoani Pwani jana.

  Mfungo aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa wanaendelea kumshikilia huku wakati wanafanya uchunguzi hadi kesho ambapo watamfikisha mahakamani.

  “Siwezi kumataja aliyekuwa akitoa rushwa kwa sababu bado tunaendelea na upelelezi, ila mpaka sasa yuko mahabusu na tutamfikisha mahakamani Jumatatu(kesho),” alisema Mfungo.

  Alisema kuwa mbali na kumfikisha mahakamani, pia watatoa taarifa zaidi za tukio hilo kesho.
   
 2. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Sasa kuna uhusiano gani kati ya kutotosha posho na ulaji wa rushwa?
   
 3. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mimi nimeshindwa kuconnect dots ...........dot..............
   
 4. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 180
  Omar Badwell? Baada ya hapo Zambi na wenzake. Nimemkumbuka David Kafulila!!!!
   
 5. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #5
  Jun 2, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Naam,

  Nimeiboresha title na content naona mwenzetu amesahau kama hii ni JF.

  Lakini, kiasi chenyewe inadaiwa hakifikii hata 5mil, achilia mbali 7mil. What a shame?
   
 6. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hivi hii ni mara ya kwanza kutokea? Nakumbuka kuna mbunge mwingine alishashutumiwa kupokea rushwa na kesi yake iliishia tu kiana. Angekuwa wa upinzani, angeweza hata kupoteza jimbo, lakini kwa kuwa ni wa magamba nafikiri hii siyo kesi tena.
   
 7. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Aliomba rushwa toka kwa nani,,Halmashauri ama? polisi wajifanye kama amewatoroka vile aje mikononi mwa wananchi
   
 8. Josephine03

  Josephine03 JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 752
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hizi dhiki zao za kilafi zitawagharimu sana

  Sent from my BlackBerry 9910 using JamiiForums
   
 9. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 180
  Ni aibu sana kwa Mbunge kushtakiwa kwa rushwa ya 5 Mil. This is Tanzania bwana
   
 10. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,461
  Trophy Points: 280
  Majasho nilimwambia kwamba wenzie watakuja kutaja yeye akawa anaficha jina...
   
 11. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Hivi milion 5 unaweza kuita ni rushwa? tena kwa mbunge?

  Kuna watu wanataka kumchafua tu muheshimiwa, ila Kaaibisha jamii yake kama "ikithibitika"
   
 12. K

  Kimweli JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 865
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Jamaa kafikisha ujumbe. Asante sana kwa taarifa mkuu. Hao ndiyo CC-HEMU ni hakuna msafi ni matumbo kwanza maendeleo nyuma.
   
 13. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,199
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  ccm hawafai Kama yupo kwenye Kamati anakula rushwa angeteuliwa waziri si angeuza wizara?
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,327
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Pole zake...njaa mwanaharamu,lol!
   
 15. P

  Penguine JF-Expert Member

  #15
  Jun 2, 2012
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Yawezekana hata yale aliyoyasema mwenzao kafulilo bungeni kwamba Zambi, Muhita na huyo Badweli walikuwa wakiomba karushwa yalikuwa ni ya kweli. jamani. Sasa hapo Hosea ndiyo mahali pa kuanzia kujenga discipline kwa hao watu, ukishindwa kumshughulikia huyo basi wote watakushinda jumla.
   
 16. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #16
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  kweli nimeamini milioni 500 si ufisadi ila laki moja ni ufisadi, ina maana 10000 ndio rushwa? Au?
   
 17. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #17
  Jun 2, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Bahi? napiga jaramba mambo yakijipa naenda kuchuka jimbo. Baduweli mrithi wa Kusila mwenyekiti wa ccm mkoa wa Dom, mbwembwe zoooote na mabiashara yako ya miaka na miaka unaomba mil 5? ngoja tuujue ukweli kwanza.
   
 18. M

  Majasho JF-Expert Member

  #18
  Jun 2, 2012
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kaomba rushwa ya 7mil jamani.... mi ndo ninayejua cos mimi i mfanyakazi wa Takukuru
   
 19. M

  Majasho JF-Expert Member

  #19
  Jun 2, 2012
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  tena kwenye halmashauri ili awakaushie....Mrema anakuwa mbogo kuwakaripia halmashauri, kumbe hawa wana chichiem wanaomba rushwa ili wamnutralize
   
 20. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #20
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,404
  Trophy Points: 280
  Aibu yake mwenyeweeeeeee,ashakosa jimbo hilo 2015.
   
Loading...