‪Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akamatwa na Polisi kwa madai ya kuzidisha muda wa mkutano‬

Mbunge wa Arusha mjini Mhe.Godbles Lema amekamatwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa madai ya kuzidisha muda katika mkutano wake kwa dakika saba (07).

Polisi wanadai Lema amemaliza mkutano saa 12:7 jioni badala ya saa 12:00 kamili kama ilivyo utaratibu.

Polisi "wamemblock" Lema katika "keepleft" cha mnara wa saa kwa kusimamisha gari mbili (moja mbele na nyingine nyuma), kisha kuingia katika gari ya Lema na kumuelekeza kituo kikuu cha polisi (central).

Hali hii imesababisha foleni kubwa kwenye barabara zinazoingia katikati ya mji.
Jamani hawa polisi sasa imekuwa too much!!!! Huku mtaani hatuna amani kwa ajili ya vibaka na wezi lakini wao wana deal na wanasiasa!!!! Kwa kweli hii sasa ina bore!!!!!
 
Wewe
Kwanini hamkulalamika wakati hayo ya muda yanapitishwa? Hapo naamini alifanya makusudi kuendelea.. kama alirekodiwa alipoongea meanzo mwisho mtajua kuwa polisi hawaonei mtu.
Unajua alichokiongea?Kosa ni alichoongea au kupitisha muda?
Baada ya kukamatwa kwake,Gambo alitoa kauli gani?
Acheni upuuz
 
Hata kama angemaliza mkutano saa 11:50 angekamatwa kwa kutofuata taratibu. dakika 7 hata ndege huwa zinachelewa hata ibada tena polisi ndo wanaoongoza kuchelewa kufika kwenye matukio ila leo wanajidai wako PERFECT; Mungu atawahukumu wote wanaotumia nyadhifa zao kukandamiza wengine. Tunaamini Mungu atajibu maombi yetu kwani sisi ndo tulio wengi. Wanaumia kimya kimya kutokana na huu ukandamizaji ni wengi kuliko wanotokeza humu. majibu yakewatayapata UCHAGUZI WA 2020.
Haaa! ila kweli angeli ambiwa kwanini amekatisha mkutano kabla ya muda
 
Hii nchi kuna kitu si bure, ukiona wazazi wanapigwa viboko kisa mtoto katupa jiwe karibu na DC, walimu wanapigishwa push up na DC kisa hawajui majina yote matatu ya DC, vilema wanatwangwa na polisi kisa hawana miguu ya kukimbia, wapinzani wanawekwa maabusu bila sababu za msingi, mjue kuna laana imeingia humu nchini, huenda ndo maana anataka tumuombee labda anajua chanzo cha hii laana.
Ataombewa na mataahira wa Lumumba tu, sisi wengine tunamuombea kinyume!
 
Polisi nchi hii wanatumika vibaya kweli ila hao wanaotoa maagizo wajue kama madaraka yana ukomo nayo
 
Mbunge wa Arusha mjini Mhe.Godbles Lema amekamatwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa madai ya kuzidisha muda katika mkutano wake kwa dakika saba (07).

Polisi wanadai Lema amemaliza mkutano saa 12:7 jioni badala ya saa 12:00 kamili kama ilivyo utaratibu.

Polisi "wamemblock" Lema katika "keepleft" cha mnara wa saa kwa kusimamisha gari mbili (moja mbele na nyingine nyuma), kisha kuingia katika gari ya Lema na kumuelekeza kituo kikuu cha polisi (central).

Hali hii imesababisha foleni kubwa kwenye barabara zinazoingia katikati ya mji.
Jamani??? Mikutano yenye limit kisheria ni mikutano ya kampeni. Hawa jamaa walio nunua vyeti wataliangamiza hili taifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona ni issue rahisi? Muda Lema alipo shuka jukwaani saa yake ilimuonyesha ni saa 12kasoro dakika mbili.
Polisi wangetaka muda uwe sawa kabla ya mkutano kuanza walitakiwa kuweka saa zao zisome sawa. Hivyo saa za Polisi zilikuwa mbele dakika 9

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda kamanda kwa ushauri wako dakika za nyongeza wangeweka ngapi...kila mkutano
Tatizo hapa askari wetu hawatumii comon sense hizo dakika saba hata error ya saa tu inaweza kuwa ni sababu halafu mtu anatumia magari na askari, akili zisizofikiria gharama ya kufanya jambo maadamu mafuta wanajaza vituoni hawajui ni kodi zetu. Hakuna weledi katika kila jambo kwa sasa ni kufukuzana na wapinzani ili mtu apate cheo!
 
Hawa ma DC Mbona wana muaibisha sana Rais magufuli amewaamini kawapa madaraka lakini wana fanya jina lake litukanwe na kukashifiwa kila siku kutokana na akili zao zilivyo sijui kwanini wana mtukanisha na kumtilia aibu rais kila uchwao na hapo ndipo upinzani hujichukulia point ni aibu kuitwa mwana wa nchi hii.
Si yeye aliyewambia watumie sheria ya kuwaweka ndani masaa 48, hata kama itakuwa ni kwa makosa ! Au mmesahau kauli hizo?
 
....... majibu yakewatayapata UCHAGUZI WA 2020.
Majibu gani unayatarajia?
Tume hii hii ya uchaguzi!
Wapeleka matokeo ya uchaguzi ngazi ya jimbo ni wateule wa rais na wako chini ya rais - unategemea waseme rais ameshindwa na hivyo na wao kukosa kazi! Utakuwa ni muujiza
 
Back
Top Bottom