Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema afungiwa Mikutano 3 ya Bunge

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
UPDATE:

LEMA AFUNGIWA MIKUTANO 3. WABUNGE WA UPINZANI WASUSIA KIKAO

- Kamati ya Maadili imeazimia kumpa Mbunge huyo wa Arusha Mjini adhabu hiyo kwa kuliita Bunge dhaifu

- Baada ya ripoti kusomwa, Wabunge wa upinzani wametoka nje ya Kikao

Spika Ndugai ameagiza Wabunge wote waliotoka ndani ya Ukumbi wa Bunge kutokana na azimio la kumfungia Godbless Lema kushiriki mikutano mitatu ya Bunge, wasiingie tena ukumbini hadi kesho

Aidha, amezuia Waandishi wa habari wanaoripoti habari za Bunge kuwahoji Wabunge hao na mwandishi yeyote atakayeonekana anamhoji Mbunge aliyesusa kikao, atanyang'anywa kitambulisho na kuondolewa bungeni


======
Awali

Hatima ya Mbunge huyo wa Arusha Mjini kuendelea au kutoendelea kuhudhuria vikao vya Bunge inatarajiwa kujulikana leo huku mwenyewe akieleza kuwa tayari ameshajua

Baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali jana, Spika Ndugai, alimtaka Lema afike mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhojiwa

Akizungumza kabla ya kuhojiwa alisema "Jana (juzi) nilipokea barua ya kunitaka kwenda kwenye Kamati ya Maadili kesho (leo) saa nane mchana, lakini kwa bahati mbaya ndani ya Bunge leo (jana), Spika ameona ni bora amalizane na mimi kesho (leo),"

"Mimi nimwambie Mheshimiwa Spika, siogopi kumalizana naye, siogopi kufukuzwa Bunge, ninaogopa kumkosea Mungu katika kazi yangu ya ubunge.

"Leo (jana) Spika amekuja bungeni, kasema niende leo (jana) saa nane, nimeshajiandaa na ninaenda kuongea kile ninachokiamini. Sitayumba, nitaongea kile ninachokiamini.

"Nimejiandaa kisaikolojia. Ninajua safari yangu ya kuwa Dodoma kwa miezi yote hii mitatu ya Bunge la Bajeti inaishia kesho (leo). Na nimeshafanya 'booking' ya safari yangu ya kurejea nyumbani Arusha ili nikaendelee na kazi zangu zingine."

Kamati hiyo ilitumia takribani dakika 132 kumhoji Lema hapo jana ambapo aliingia kuhojiwa mara tatu akihojiwa na kutoka kisha akaitwa tena na hadi saa 11:58 jioni alimaliza

Awali mbunge huyo aliingia ndani ya kamati akitumia dakika 44 kisha akatoka na kuitwa tena saa 9:52 akatoka 10:56, kisha akaitwa kwa mara ya tatu saa 11:34 hadi saa 17:58 alipomaliza kuhojiwa.

Wakati akiitwa mara ya tatu, alikuwa ameketi na Mbunge wa Momba (CHADEMA), David Silinde ambaye alimtaka akitoka wawasiliane kwanza.

Majira ya saa 11:06 kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freman Mbowe alifika katika eneo alilopumzika Lema wakakaa wakizungumza kisha kisha wakaagana.

Mbunge huyo ameitwa mbele ya Kamati kuhojiwa kutokana na mchango wake bungeni jana aliponukuu kauli ya Mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee kuwa "Bunge ni dhaifu".
 
Kuna mbegu ingine na leo tena itasema bunge ni dhaifu... itaitwa kwenye kamati..

Mbona huku uraian tupo wengi tunaosema bunge ni dhaifu na hatuitwi?? Kamati gani inachagua watu wa kuwaita?? 🤨


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Watuuwekee live ili wananchi tuujue ukweli kama wanatendewa haki maana hata CAG amewataka waweke mahojiano yake hadharani ili wananchi tuujue ukweli
Lini waliwahi weka live?

We think too small, like the frog at the bottom of the well. He thinks the sky is only as big as the top of the well. If he surfaced, he would have an entirely different view.
 
Hizi drama tuu kuna mambo mengi tuu ya msingi ya kufanya sio kushinda kwenye kamati hata kwenye mambo ambayo hayastahili Bunge letu linapoteza radha yake kabisa awamu hii.
 
Godbless Lema: Nimesimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge mpaka January 2020. Moyo wangu una amani sana, kwani mahusiano yangu na HAKI yanaendelea kuimarika zaidi. Nawatakia Wabunge wenzangu kazi njema katika wajibu huu, sitanyamaza hata kama adhabu itakuwa ni mauti.
 
Back
Top Bottom