Ndallo
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 7,619
- 4,292
Kwa niliyoyasikia toka Arusha kwa mkereketwa wa CDM Mheshimiwa LEMA ALIOMBA KICHAPO KILE YEYE MWENYEWE!!SOMO
- Wao CDM walishagoma kwenda kwenye uchaguzi, wenzao wakaendelea! Kama sheria ilikiukwa (na CCM) basi CDM wangesubiri kupinga hilo kwa kufuata sheria!!
- Kuingia ukumbini wakati kikao cha uchaguzi (walichokigomea CDM) kimemalizika na kuanzisha vurugu ya kupinga matokeo ilitafsiriwa kama "kuvuruga amani"...na mbaya zaidi...
- Sheria ya nchi (Under the Criminal Procedures Act ikisomwa pamoja na Law of Evidence na Katiba yetu) inawaruhusu Polisi (au mtu yeyote aliyepewa dhamana ya kulinda usalama) kutumia "nguvu ya kiasi" wakati wa kumkamata (Arrest) na kumdhibiti (restrain) mhalifu/mtuhumiwa asilete madhara!! Bwana Lema alitoa BASTOLA, ni dhahiri endapo asingedhibitiwa angeweza kumdhuru mtu (Kwa kuwa kisheria huwezi kuelewa state of mind ya mtu wakati anafanya tendo lolote lile)....Kwa hiyo ilikuwa ni halali kwa polisi kumkamata na kumnyong'onyeza maana akkuwa anaendelea kutishia na hakujisalimisha kwa polisi!! Isitoshe polisi hawajatumia bastola au silaha nyingine, wametumia Judo na virungu...which so far was reasonable force!!
Tunaipenda CDM lakini mbinu zake sasa zinatuchosha, watapigwa sana kama hawatakaa chini na kujadili mbinu mbadala! Wote tunajua kwa nini RPC Arusha alibadilishwa, yule jamaa na watu wake wako kwa kazi maalumu, wanasubiri kuwa "tuned" tu, sasa kama adui umeshamuelewa anakupaje kazi kupambana naye? Hebu CDM wafuate sheria, wapambane KISAYANSI siyo kwa kutumia nguvu "ZA KIJINGA"....Kamwe hatutaweza kushindana na dola....TUWE MAKINI
Kaka au sijui ni dada tafadhali tuambie nini maana ya kupambana KISAYASI???? Hivi polisi anaruhusiwa kutoa hukumu kwa mtuhumiwa au ni mahakama? unamaanisha wale polisi walivyotoa ile adhabu kwa bwana Lema walitumia nguvu ya KISAYANSI SIO???