Mbunge wa Arumeru mashariki Mhe.Joshua Nassari tarehe 17/02/2019 alikutana na Askofu Paul Erickson katika jimbo la Wisconsin Marekani

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,248
2,000
Mbunge wa Arumeru mashariki Mhe.Joshua Nassari tarehe 17/02/2019 alikutana na Askofu Paul Erickson katika jimbo la Wisconsin Marekani kupata chakula cha mchana.

Pamoja na mambo mengine walijadiliana mambo mabali mbali ya kuendeleza mradi wa Maji ambao waliufadhili kupeleka maji kutoka Tengeru hadi Kikwe ambapo kwa mujibu wa Mhe.Nassari wafadhili hao wanajipanga ili kuufikisha mradi huo hadi msitu wa mbogo na Shambarai Burka.

Mhe.Nassari yupo Marekani kwenye programu ya mafunzo ya viongozi kupitia taasisi ya Obama Foundation kwenye Jimbo la Chicago

Ikumbukwe mnamo mwezi wa nane mwaka jana 2018 Mhe Nassari alimkabidhi Askofu Erickson na timu yake vyeti vya shukrani baada ya kukamilika kwa mradi huu wa maji sehemu ya kwanza uliogharimu takribani tshs 120M chini ya ufadhili wa dayosisi anayoiongoza. Ashukuriwe Mungu.

IMG-20190220-WA0075.jpg
IMG-20190220-WA0076.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom