Mbunge Viti Maalum Sikudhani Chikambo, anusurika kifo kwenye ajali

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
38f07941dbbed01210eefed2de56d073.jpg

Toyota VX lenye namba za usajili T329 DGK alilokuwa akisafiria Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Ruvuma, Sikudhani Chikambo (picha ndogo) iliyopata ajali na kusababisha kifo cha mtu mmoja leo mchana eneo la Dumila, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro.

MBUNGE wa Viti Maalum mkoa wa Ruvuma CCM, Sikudhani Chikambo amenusurika kifo katika ajali ya barabarani hii leo Dumila, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro. Anaandika John Nditi-Morogoro.


Mbunge huyo pamoja na watu wengine watano walikuwa wakisafiri kutoka Dodomna kwenda jijini Dar es Salaam ndipo gari walilokuwa wakisafiria Toyota VX lenye namba za usajili T329 DGK, kupasuka gurudumu na kuacha njia na kupinduka na kusababisha kifo cha ndugu wa Mbunge huyo.


Akizungumza akiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro alikolazwa kwa matibabu alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wake kuwepa shimo lakini kutokana na ukubwa wa shimo hilo gurudumu lilitumbukia na kupasuka kisha gari kupoteza muelekeo na kupinduka mara tano.


“Dereva alikuwa anakwepa shimo, lakini kutokana na ukubwa wa shimo tairi lika tumbukia na kupasuka gari iliyumba na kupoteza mwelekeo …na kupinduka mara tano kabla ya kusimama,”alisema Sikudhani.


Alisema aliyepoteza maisha ni ndugu wa karibu wa kiume aliyekuwa akiishi Dodoma na kufanyia kazi za ujenzi wa nyumba.


Alisema baada ya ajali walikimbizwa Hospitali ya Kanisa Katoliki Dumila na baadae kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Morogoro.


Wabunge Mbalimbali wa mkoa wa Morogoro wakiongozwa na Mbunge wa Morogoro mjini, Abdulaziz Abood, Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Omary Mgumba, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde na Mbunge wa Viti Maalumu Vyuo Vikuu, Dk Jasmine Tisekwa walimtembelea na kumjulia hali.


Dk Tisekwa ndiye alimsaidia Mbunge mwenzake na majeruhi kuletwa hospitali kuu.

Chanzo: Habari leo
 
Mashimo ya barabarani hakuna anaye jari na huwa yanachangia sana ajali na uharibifu wa magari , unakuta shimo katikati ya barax2 likakaa zaid ya mwezi
 
Akirudi bungeni apiganie barabara zitebgezwe ziwe ktk hali nzuri na zisiwepo mashimo

Any way pole mbunge!

Ova
 
MBUNGE wa Viti Maalum mkoa wa Ruvuma CCM, Sikudhani Chikambo amenusurika kifo katika ajali ya barabarani hii leo Dumila, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro. Anaandika John Nditi-Morogoro


Dumila haipo Mvomero, ipo Kilosa
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Inatakiwa wapigie kelele swala la ukarabati wa barabara kuu nyingi zinamashimo hatari
Mf barabara ya tdm dar baadhi maeneo ya mbeya na iringa
Poleni wafikwa wa janga hilo
 
Mashimo ya barabarani hakuna anaye jari na huwa yanachangia sana ajali na uharibifu wa magari , unakuta shimo katikati ya barax2 likakaa zaid ya mwezi
Sio mwezi tu wakati mwingine hadi mwaka....rejea shimo la Mafinga lililoua watu zaidi ya hamsini kwenye Majinja... lilikuwa shimo la mda mrefu sana.
 
Hawa Tanroad wamekuwa kama wapo above the law!! Hili zigo ni la tanroad manager WA Morogoro Ila kwa negligence no one knows who is responsible! Ohh my country
Ndio Maana kuna routine maintenance! Unakuta shimo Lina miezi miwili no one cares! Hata hapo dar mashimo kama hayo ni mengi no one cares
 
Inatakiwa wapigie kelele swala la ukarabati wa barabara kuu nyingi zinamashimo hatari
Mf barabara ya tdm dar baadhi maeneo ya mbeya na iringa
Poleni wafikwa wa janga hilo
Shimo la kwenye barabara ya rami ni baya mara 100 ya shimo la kwenye njia ya vumbi. Sababu sababu zile sehemu zinazo lizunguka zinakuwa kali kama kisu. Ulaya njia kuu zote ambazo zipo busy mchana na usiku kwa kiasi zinafanyiwa ukarabati usiku wa manane ambapo magari huwa machache, kama kuziba vilaka kama hivyo, kwa hiyo ni bora Tanroad wakaiga hilo
 
Wabunge ndio hasa wanapaswa kupigia kelele utendaji mbovu unaosababisha ajali kama hizo, lakini wao muda mrefu ni vijembe kwa wapinzani badala ya kuibana serikali.
Mwishowe watu hawatendi kwani watetezi wapo wa kutosha bungeni
 
Mashimo ya barabarani hakuna anaye jari na huwa yanachangia sana ajali na uharibifu wa magari , unakuta shimo katikati ya barax2 likakaa zaid ya mwezi
Kuanzia Dumila hadi Dodoma.....kuna mashimo mengi yanachongwa na waziba vilaka vya lami.....yamesababisha ajali 5 week 3 hadi sasa.....nenda Kibaigwa Fuso imepiga mweleka same fashion.....mbele yake tena Gari ndogo imepinduka kupiga shimo hilo hilo!! Wakichimba mashimo kuziba vilaka vya lami hawaweki alama!! Yale mashimo ukiyapiga Ukiwa zaidi 60km lazima upasue tairi.....
 
Back
Top Bottom