Mbunge Viti Maalum (CCM) matatani; TATIZO la udanganyifu wa umri na elimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge Viti Maalum (CCM) matatani; TATIZO la udanganyifu wa umri na elimu

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by nngu007, Mar 20, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  TATIZO la udanganyifu wa umri na elimu limeibuka tena baada ya Mbunge wa Viti Maalumu kupitia UVCCM Zanzibar, Asha Muhamed Omar, kugundulika kuwa amefanya hivyo na kujipatia nafasi hiyo katika uchaguzi uliofanyika Agosti 2010.

  Hayo yalisemwa na Tarehe Hamad wakati alipozungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam. Alisema kutokana na udanganyifu huo, wa umri na elimu aliweka pingamizi la kumpinga mgombea huyo, Asha ambaye hivi sasa ni mbunge.

  "Asha Omari amechaguliwa wa nafasi ya ubunge kupitia Viti Maalumu UVCCM katika uchaguzi uliofanyika Dodoma Agosti 3, 2010 ambapo nilimuwekea pingamizi ili haki itendeke lakini hakuna hatua za kuridhisha zilizochukuliwa dhidi yake," alisema Tarehe.


  Alisema kwa mujibu wa taratibu za UVCCM, kiongozi anatakiwa asizidi umri wa miaka 35 na elimu isiyokuwa chini ya kidato cha nne.

  Alisema baada ya kufuatilia kwa karibu ndipo alipogundua kuwa katika utambulisho wa umri na elimu yake anatumia vyeti vya Asha Mohamed Omar wa Kiwani ambae ni mwalimu katika shule ya Pemba.

  Alibainisha kuwa kinachoendelea ni ahadi toka kwa viongozi kuwa wangeshughulikia suala hilo lakini hadi leo hakuna hatua zozote za kuridhisha zilizochukuliwa zaidi ya mlalamikiwa kushawishi kulimaliza suala hilo nje ya vikao.
   
 2. V

  Vancomycin Senior Member

  #2
  Mar 20, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkubwa ungeweka na source ya habari hii.
  Na kama ni kweli hatutashangaa ndiyo tabia iliyoota mizizi kwa hao wa kijani,sijui watashughulikianaje wakate wengi tu humo elimu na vyeti vyao utata mtupu.
   
 3. Mipangomingi

  Mipangomingi JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 980
  Trophy Points: 280
  Kwani na huyo tarehe ana umri na elimu gani,na amejiunga lini huko ccm hata ashangae hayo?
   
 4. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mmmm wazanzibar kwa kuchakachua why?
   
 5. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  CCM wanachakachua kila kitu, inakuwaje mtu anachakachua hadi umri?????, kama amefanya hivyo hafai kuwa kiongozi wa watu.
   
 6. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu STEIN Je wajua kiongozi mzuri ndani ya CCM ni nani na wa aina gani? Huyu mama amewakilisha the real CCM. Hakuna sababu yoyote ya kupambana naye. After all hicho kiti hata kama atanyang'anywa atapewa CCM mwingine kama yeye. Kwa hiyo mkulu nikuhakikishie tu kama unataka kutafuta viongozi wakweli na walio straight forward hautawakuta ndan i ya CCM.

  Huyu mama hastahili hukumu yoyote kwani yeye ni mwovu kama walivyo wenzake wengi ndani ya chama. This is the brand of the party.
   
 7. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wandugu,

  Kama hii taarifa ni ya kweli ni budi wananchi wakaishikilia bango. Tabia ya kughushi imezidi nchini mwetu. Kesi za kughushi zimejaa mahakamani. Wanafunzi wanaoghushi vyeti wanalala rumande na kufunguliwa kesi iweje Mbunge aghushi na aachwe? Masauni aliachwa na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa zaidi ya kujiuzulu. Ni nchi gani inaendeshwa na siasa badala ya sheria?

  Kama ameghushi sheria ichukue mkondo wake mara moja. Ujerumani waziri alidesa kwenye thesis yake akalazimika kujiuzulu, hapa kwetu eti abaki tu. Hapana.
   
 8. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  ....................
  Muhimu sana hilo!!
   
 9. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Sijui kamawata chukua hatua, CCM uovo zaidi ndio sera zao; nadhani CCM wanatafuta watu walioghushi ili waweze kuwa Control ki-rahisi, kuwanyang'a nguvu maana akitaka kucharuka akakumbushwa we nyamaza nitaibua swala lako la kughusi lazima akae chini. Sasa Masauni labda alifiri kuwa hawata weza tayari kavuka mtu.
   
 10. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Tumeshuhudia viongozi wengi waliochakachua elimu zao ndani ya CCM na bado wamepewa madaraka makubwa kama uwaziri pengine kwa ushawishi wa elimu waliyoichakachua. Malalamiko mengi yalitolewa na vyombo mbalimbali na hata Bw.Kainerugaba Msemakweli kuandikwa kitabu cha MAFISADI WA ELIMU na kuwaorodhesha viongozi kadhaa na mapungufu yao. Hakuna hata mmoja aliyejisafisha, licha ya Mh. Dr. David Mathayo kusafishwa na spika wa Bunge kipindi hicho Mzee Samweli Sitta. Wengine hatukuona wakijisafisha ama kurekebisha taaluma zao halisia. Ni wawili tu (Mh. Milton Makongoro Mahanga na Mh. Antony Diallo) ambao walifungua kesi kuhusiana na kitabu kilichoandikwa na Bw. Msemakweli, chakushangaza ni Bw. Msemakweli uhudhuria Mahakamani pekeyake na waliomshitaki kutokufika. Mpaka sasa nahisi kesi itakuwa imefutwa ama mbioni kufutwa kufuatia kipindi flani Bw. Msemakweli kulalamika hawaoni waliomtuhumu makakamani ili walete vielelezo vyao na yeye atoe vyakwake.

  Hivyo, waliochangia kuwa CCM hiyo siyo tuhuma na wengi wao inaonyesha ndivyo walivyo, wananishawishi nikubaliane nao kwa asilimia 100. Kama idadi kubwa namna hii ya viongozii wanagushi elimu zao na kujipatia madaraka, je hawa wanaowaongoza wakifanya hivyo watawezaje kuwadhibiti. Tunaomba TCU fanyieni kazi ya kuhakiki elimu za watu kwenye sekta zingine zote ingawa mmeshindwa kwa waheshimiwa wetu, licha ya Tume ya Uchaguzi kutueleza kuwa watashirikiana na TCU ili kuhakiki elimu za wagombea (2010).
   
 11. k

  kijana85 New Member

  #11
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi binafsi nna uwezo wa kukupatieni nakala za vyeti vya halali na ukweli ni kwamba vimewasilishwa kwa wahusika mienzi kadhaa.

  CCM inabidi hii issue waikalie kwa sababu ya kuogopa aibu nyengine. Naturally suala litakaloulizwa ilifikaje fikaje kua namna hii, mpaka mtu anafika kuapishwa, definately wenyewe ni wazembe. kwahio wanaona bora wawe na muwakilishi wa vijana alie mbumbumbu aliefoji vyeti aliekua hajasoma so that they can black mail her and manipulate her wanavyotaka then try to do the right thing and get themselves embarrassed with how ineffective they are wanapokula pesa za vikao vya kuchuja wagombea wa viti hivo.

  They know this issue hata kama itapigiwa kelele vipi it will not go anywhere!!

  Suala ni kwamba, what does this do to Vijana madhubuti who had the right qualifications and are ready kulitumikia Taifa?
   
Loading...