Mbunge Viti Maalum CCM, Amina Mollel adai Mbunge Joshua Nassari hajui shida za waliomchagua

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mbunge wa Viti Maalum CCM, Amina Mollel amedai tangu Joshua Nassari alipochaguliwa kuwa mbunge wa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chadema, ametokomea kusikojulikana na hajui shida za wananchi waliomchagua.

Mollel ametoa madai hayo leo Jumapili Desemba 2, 2018 katika uzinduzi wa mradi wa uboreshaji huduma za maji safi na maji taka katika jimbo la Arumeru Mashariki uliofanywa na Rais Magufuli.

"Naamini walifanya makosa na hawatarudia tena 2020 na mimi niko hapa kwa ajili ya kuwasemea ili kuhakikisha shida zao zinatatuliwa," amesema Mollel. Katika uzinduzi huo Nassari hakuwepo.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alisema Nassari yupo na wananchi wake na anafanya shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwamo katika sekta ya elimu na afya.

“Kuna kipindi Nasari alikuwa anasoma ila kwa sasa amemaliza na anaendelea na shughuli zake za Kibunge, Amina si msemaji wa wananchi wa Arumeru kazi hiyo ni ya wananchi wa Arumeru na kama alitaka kushitaki angewashitaki kwa Rais, mawaziri waliotajwa kutohudhuria vikao vya Bunge.

Kwa upande wake mbunge wa Monduli, Julius Kalanga amemuomba Rais kuwasaidia kuondokana na shida ya maji kwa sababu wananchi wake wana hali mbaya.

Amesema hata akipewa nafasi kadhaa za kutoa maombi yake ili aweze kusaidiwa katika utekelezaji mara zote angetaja maji.

"Kama ulivyowakumbuka wenzetu wa Arumeru, tunaomba na sisi utukumbuke katika ufalme wako kwa sababu tuna shida kubwa ya maji," amesema Kalanga.

Mbunge wa Jimbo la Siha, Godwin Ole Mollel amesema atahakikisha viongozi wa upinzani wanaopiga kelele wananyamazishwa ili chama tawala kiendelee kujenga na kuboresha uchumi.

"Tuhakikisha wote wananyamazishwa waache kupiga kelele hasa pale mambo mazuri yanapofanyika huku wao wakijaribu kuwapeleka wananchi katika mada zisizojulikana," amesema Mollel.

Chanzo: Mwananchi
 
Acha kupotosha wew hakuna aaesema JPM ameondoa kero zote na ndio maana unamuona anajitahidi kuzindua miradi mikubwa mikubwa

Ni mimi ninaepotosha au wabunge wenu wanaopiga kelele kua tumefika nchi ya maziwa na asali wakati mpaka leo asilimia kubwa ya wanainchi hawana huduma ya maji safi na salama,madawa ni mtihani na elimu nako kunajikongoja.
 
No ulaghai tu Galina binge abstruse Shida za wanajimbo Wake na hata akijua bado kwenye utatuzi atategemea huruma ya wenye dola na hazina yao !
 
Mbunge wa Jimbo la Siha, Godwin Ole Mollel amesema atahakikisha viongozi wa upinzani wanaopiga kelele wananyamazishwa ili chama tawala kiendelee kujenga na kuboresha uchumi.
TULIKUWA TUNAWATAFUTA WATU WASIOJULIKANA, SASA WAMEANZA KUJITOKEZA MMOJA MMOJA. POLISI ANZENI NA HUYU
 
Shughuli ya kuzindua mradi wa maji leo imefanyika jimbo la arumeru magharibi na sio arumeru mashariki, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni
 
Ila Nassari amepwaya sana awamu hii. Huwezi kutumia kisingizio cha shule kwa wananchi ulioomba kuwawakilisha. Ajitahidi kubadilika bana
 
Back
Top Bottom