Mbunge viti maalum aibiwa baa!

magosha

JF-Expert Member
Apr 25, 2012
689
89
mbunge wa viti maalum ccm kutoka mkoa anakotokea Pinda ameibiwa baa usiku wa saa nane za usiku akila bata huko Dodoma.
Source: wapo Radio.

Mbunge aporwa baa




Na Mwandishi wetu



26th April 2012




Jambazi lilitinga na gobore
Lakusanya fedha, simu, mikoba


View attachment 52731



Mbunge wa viti maalum (CCM) Pudesiana Kikwembe


Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi, Pudesiana Kikwembe (44) (pichani), amevamiwa na kuporwa fedha katika baa mjini Dodoma.

Mbali na kuporwa fedha hizo, pia Kikwembe aliporwa kadi za benki katika tukio hilo lililotokea katika baa hiyo inayojulikana kama Lady May Pub mjini hapa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Zelothe Stephen, tukio hilo lilitokea juzi saa 2:30 usiku, katika baa hiyo iliyoko katika barabara ya Iringa, Manispaa ya Dodoma.

Kamanda Zelothe alisema kuwa mtu mmoja ambaye hakufahamika jina, alivamia baa hiyo akiwa na gobore na kumpiga risasi ya mguu wa kulia katikati ya goti na kifundo cha mguu mkaanga chips ambaye amefahamika kwa jina la Ally Kubula (22).

Aidha, Kamanda Zelothe, alisema jambazi hiyo alipora mikoba miwili mmoja ukiwemo wa Mbunge huyo ambao uliokuwa na Dola za Marekani 600 (Sh. 950,628) pamoja na fedha taslimu za Sh. 180,000. Mkoba huo pia ulikuwa na kadi za benki za NMB, CRDB na NBC.

Pia Kamanda Zelothe, alisema mkoba mwingine ulioporwa na jambazi huyo ni wa Sharon Tuli ambaye ni rafiki wa mbunge huyo. Alisema mkoba huo ulikuwa na simu mbili, ambazo hata hivyo, hakutaja aina wala thamani pamoja na fedha taslimu Sh. 100,000.

Alisema juhudi za kumsaka mtuhumiwa huyo zinaendelea na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma bado linatoa rai kwa wananchi kupitia mkakati wa polisi jamii na ulinzi shirikishi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuhakikisha wanawabaini wahalifu na kuwachukulia hatua stahiki.

Pia alisema wanatoa wito kwa wamiliki wa baa zote kufuata sheria, kanuni na taratibu zinazowaelekeza namna ya kufanya biashara ya baa na grocery, ikiwemo kufunga kwa wakati ili kuepusha vitendo vya uhalifu vinavyoweza kuzuilika. Kamanda huyo aliongeza kuwa, majeruhi huyo amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma katika wodi namba 11.

Kikwembe akisimulia tukio hilo, alisema kuwa alikuwa amekwenda kwenye baa hiyo kukutana na wanafunzi waliohitimu Shahada zao za Uzamili wa elimu kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) wanaotoka mikoa ya Rukwa na Katavi.

“Sasa baada ya kumaliza mazungumzo yetu nafikiri ni kati ya saa 2 na saa 2.30 hivi, nikiwa naongea na simu nikaona mtu mmoja aliyevaa koti anaingia,” alisema.

Alisema kuwa ghafla aliona mtu huyo akimsukuma kijana anayekaanga chips na kumwangusha chini, kisha akatoa sauti ya ukali kila mtu alale chini.

“Lala chini. Mara nikasikia mlio wa risasi. Kwa kweli nilishtuka sana. Pamoja na kwenda JKT mlio wa risasi ulinishtua mno,” alisimulia akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana jioni.

Alisema jambazi huyo aliyekuwa amevaa koti refu, alikusanya mikoba yote iliyokuwa mezani na kutokomea, lakini waliposimama walikuta yule mkaanga chips amepigwa risasi ya mguuni.

“Inawezekana yule jambazi alimpiga risasi kijana yule kwa sababu alimtazama usoni, lakini kwa kweli huu ni ukatili mbaya sana,” alisema.

Mbunge huyo alisema kuwa ni jambo la kushangaza kuwa uhalifu wa kutumia silaha unatokea katika mitaa ya mji wa Dodoma wakati viongozi wa serikali akiwamo Waziri Mkuu, mawaziri na wabunge, wakiwa Dodoma muda ambao ulinzi wa polisi unakuwa umeimarishwa.

Pia alisema tukio hilo lilitokea si mbali sana kutoka Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma, tena karibu na nyumbani kwake na nyumba ya Naibu Waziri wa Maji, Gerryson Lwenge, ambako kuna ulinzi mkali.

Kadhalika, alisema ingawa wakati jambazi hilo linaingia eneo hilo, waliona gari la polisi la doria limepita, lakini iliwachukua polisi muda wa saa moja kufika eneo la tukio baada ya kupigiwa simu juu ya tukio hilo.

Walipoulizwa kwa nini walichelewa hivyo, walisema walikuwa wamekwenda nje ya mji baada ya kupata taarifa kuwa kulikuwa na mume na mke wamepigana visu.

Naye majeruhi, Kubula, akizungumza katika wodi ya hospitali ya Dodoma alikolazwa, alitofautiana maelezo na polisi na Mbunge, akisema tukio hilo lilitokea usiku wa saa nane.

Alisema kuwa alikuwa kwenye baa hiyo akimsubiri bosi wake kwenda kufunga baa hiyo, ndipo mkasa huo ulipotokea na wakati huo kulikuwa na watu wanne tu kwenye baa hiyo, ambao ni yeye, Mbunge, rafiki yake pamoja na bosi wake.

Majeruhi anasema kuwa bado anasumbuliwa maumivu makali kutokana na kujeruhiwa mguuni kwa risasi.
Tukio hilo lilitokea wakati wabunge wakiwa mjini Dodoma.

Mkutano wa Saba wa Bunge la 10 uliahirishwa Jumatatu jioni na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, lakini juzi wabunge wote walibaki mjini Dodoma kwa ajili ya semina ya kujadili mapendekezo ya Mfumo wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2012/2013.

Kutokana na ulazima wa semina hiyo, wabunge walitakiwa kuanza kuondoka mjini Dodoma jana.
Kwa kawaida, wakati wa vikao vya Bunge Polisi Mkoani Dodoma huimarisha ulinzi kwa ajili ya usalama wa wabunge na maofisa
wengine wa serikali.



CHANZO: NIPASHE
 
Litakuwa limemwibia buzi lake sijui atamwambia nn mmewe kikao gani cha kukaa mpaka saa nane usiku?
 
Mbunge ni mtu kama wewe tu wakati mwingi. Sasa tukiweka matukio ya watu wooote humu sijui vipi. WAKE UP!
 
Hapo usikute alikuwa anapiga nyagi manake wabunge wa hiki chama hawachagui vinywaji iwe wanawake au wanaume.Ila sio mbaya fedha za wananchi zimerudi kwa wananchi.
 
mbunge wa viti maalum ccm kutoka mkoa anakotokea Pinda ameibiwa baa usiku wa saa nane za usiku akila bata huko Dodoma.
Source: wapo Radio.

nawap hongera wenye njaa kufanikisha hilo. naye alikuwa na SMG? Alikuwa na dola za kimarekani? pesa za ktz zilikuwa bei gani?
 
Nafikiri wakiendelea kufanyiwa tuvitendo km utwo basi watapunguza starehe na kuwa makin huku wakitambua kuwa wao ni kioo cha jamii.
 
mbunge wa viti maalum ccm kutoka mkoa anakotokea Pinda ameibiwa baa usiku wa saa nane za usiku akila bata huko Dodoma.
Source: wapo Radio.

Kwa mantiki ya Kiswahili, mtu hawezi "kuibiwa". Kimsingi, hakuna kitu chochote "kinachoibiwa", ila, mali huibwa.

Ulipaswa kuandika "mali za mbunge wa viti maalum zaibwa akiwa bar...."

Kiswahili ni kigumu, tusiwe wepesi kuendelea kukubali makosa makubwa, kama vile wanaosema "nyimbo hii" wakati walipaswa kusema "wimbo huu".
 
mkuu acha zako mbunge hawezi akawa kama wewe yeye ni kioo cha jamii tumweleweje sasa sisi watu wa katavi.

tatizo hapo ni WEZI, sio mbunge. Unamaanisha ukiibiwa wewe sio ishu, ila akiibiwa mbunge ndo ishu? Wabongo tuna matatizo.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom