Mbunge Vicky Kamata augua ghafla masaa machache kabla ya ndoa yake, Mume aingia mitini!

Status
Not open for further replies.

Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,780
3,208
Dodoma/Dar es Salaam. Ni matukio nadra kutokea katika maisha, lakini haya ndiyo yaliyomkuta Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Vicky Kamata, baada ya kuugua ghafla saa 36 kabla ya harusi yake.

Kuugua kwa bibi harusi huyo mtarajiwa, kumezua gumzo katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma na maeneo mengine nchini, kutokana na kile kilichoelezwa kwamba harusi hiyo ilipangwa kuwa ya kifahari ikitarajiwa kutumia Sh96 milioni.

Kamata ilikuwa afunge ndoa leo katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi, Sinza Dar es Salaam na tayari kadi za mialiko zilishasambazwa kwa watu mbalimbali wakiwamo wabunge.

Habari za kuugua ghafla kwa mbunge huyo ambaye pia ni msanii wa muziki aliyetamba na kibao chake cha ‘Wanawake na Maendeleo' zilianza kuzagaa kwa kasi juzi jioni nchini.

Kamata ambaye pia ni mtetezi wa haki za wanawake, aliugua usiku wa kuamkia jana na kupelekwa katika Hospitali ya Tabata General, iliyopo Segerea ambapo amelazwa.

"Niliugua tumbo ghafla, nilipata maumivu makali sana nikampigia daktari wangu na nilipomweleza jinsi ninavyojisikia, aliniambia niende hospitali haraka na kutokana na hali ilivyo, waliamua nilazwe," alisema Kamata akiwa kitandani katika hospitali hiyo.

Kamata alifafanua kuwa, pamoja na mambo mengine, hali yake ya ujauzito imekuwa ikimsumbua na kuchangia yeye kulazwa kwa mara ya pili sasa katika kipindi cha wiki mbili. Mbunge huyo ambaye alitakiwa kufunga ndoa leo, alisema kuwa kutokana na maradhi hayo, haelewi hatima ya ndoa yake, ingawa wanafamilia na wanakamati wanaendelea na mipango ya harusi kama ilivyopangwa.

"Mama anaenda nyumbani sasa hivi kuniandalia nguo na kila kitu, lakini sijui itakuwaje kwa sababu daktari amesema kutokana na hali yangu ilivyo, itakuwa vigumu kuvaa viatu virefu na kupata usumbufu wote wa purukushani za harusi," alisema.

Aliongeza kuwa mipango yote ya harusi ipo tayari kinachosubiriwa na siku yenyewe, lakini kwa bahati mbaya jambo hilo limetokea na haliwezi kuepukika.

Vicky alisema wanakamati wa Dar es Salaam na wale wa Dodoma, wanaendelea na vikao ingawa, wamechanganyikiwa kutokana na sintofahamu iliyopo, kama harusi itafanyika au haitafanyika.

Ndugu wa mbunge huyo akiwemo mama yake mzazi Kamata walionekana hospitalini hapo wakiendelea kumfariji na kujadili kuhusu hatima ya harusi hiyo, iliyokuwa ikingojewa kwa hamu na wanafamilia wote.

Daktari wa Kamata, aliyefahamika kwa jina la Diwani Msemo, alieleza kuwa mbunge huyo alifika hospitalini hapo akiwa na maumivu makali ya tumbo yaliyofanana na uchungu wa kuzaa, hali iliyoonyesha kuwa ujauzito wake unatishia kutoka.

"Ukipata yale maumivu kama mimba ni changa inakuwa kama tishio la mimba kutoka, siyo hivyo tu, bali alikuwa anatapika na presha ikashuka. Kwa kweli mimba yake ipo katika hatari," alisema

Alisema pamoja na kumpa matibabu, walishauriana kuwa apumzike kwa siku tano ili kuhakikisha kiumbe kilichopo tumboni kipo salama.

"Ilikuwa ni uamuzi mgumu kwa sababu ni siku yake ya harusi, lakini tunaangalia umuhimu wa kiumbe na kama ataenda, itabidi asaini ili ijulikane kuwa hatukumkubalia. Kwa kifupi hayuko fiti kwa shughuli hiyo," alisema.

Harusi ya Kamata iliandikwa pia na mitandao mbalimbali ya kijamii nchini na jana redio moja ilitangaza kuugua kwake, ikisema kumetokana na matatizo ya ujauzito.

Kumekuwa na uvumi unaosambazwa kwa kasi juu ya sababu za kuahirishwa kwa harusi hiyo, lakini kwa sababu ya maadili ya uandishi hatutaweza kuziandika katika gazeti hili.

Paroko aliyekuwa afungishe ndoa anena

Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi , Sinza Dar es Salaam, Cuthbert Maganga alipohojiwa kuhusu taarifa za kufungwa kwa ndoa hiyo, alikiri kwamba iliandikishwa ili ifungwe kanisani hapo.

Hata hivyo akasema ilishindikana, baada ya wahusika kukwama kuwasilisha baadhi ya nyaraka muhimu zilizohitajika, ili kukamilisha sakramenti hiyo.

"Ilitarajiwa kufungwa Mei 24 mwaka huu yaani kesho (leo), lakini kwa taratibu za kanisa letu ilishindikana kwa sababu bibi harusi alishindwa kuwasilisha cheti chake cha ubatizo, pia hakuwa amepata kipaimara, vitu hivyo ni miongoni mwa vitu muhimu vinavyohitajika ili kukamilisha Sakramenti ya Ndoa," alisema Padri Maganga.

Alisema Kamata ndiye aliyekwenda kuandikisha ndoa hiyo, kwa kuwa ni muumini wa kanisa hilo anayetokea Kanda D.

Juhudi za kumtafuta bwana harusi, Charles Gardner hazikuweza kufanikiwa baada ya simu yake kuita bila kupokelewa, hata alipotumiwa ujumbe wa maandishi hakuwa tayari kujibu.

Hata hivyo, baadhi ya rafiki wa karibu wa Gardner walieleza kuwa wamejulishwa kuwa ndoa hiyo haipo na kwamba jana bwana harusi huyo mtarajiwa alionekana akiwa katika hali isiyo ya kawaida.

"Nilijaribu kumuuliza kuhusu harusi yake, lakini hakuwa tayari kunieleza bayana, ila hayupo katika hali yake ya kawaida," alisema mmoja wa rafiki zake.

Source: Mwananchi

ILE ndoa inayodaiwa ikifungwa harusi yake itatafuna shilingi milioni 96 kati ya Mbunge wa Viti Maalum Geita kwa tiketi ya CCM, Vicky Paschal Kamata na mwanaume aliyejulikana kwa jina la Charles iko katika hatihati ya kufungwa kutokana na kuibuka kwa mizengwe.

Habari za ndani zinadai kuwa mizengwe iliyoibuka katika hatua za mwisho zimemfanya mwanaume huyo kuamua kubatilisha ndoa ambayo ilikuwa ifungwe Mei 24, mwaka huu jijini Dar es Salaam. "Kuna mizengwe mingi sana kwenye hii ndoa japokuwa iko katika hatua za mwisho lakini hatihati. Wapo watu wanasema kuwa mwanaume anadaiwa ana mwanamke mwingine, wengine wanasema ana mchumba ameshamlipia mahari kwa wazazi wake kwa
hiyo mambo yameshajulikana na jamaa akaona aachane na ndoa hiyo.

"Lakini katika yote hayo, ukweli ni kwamba kuna asilimia tisini ya ndoa kutofungwa hiyo Mei 24 ndicho ninachokijua mimi," alisema mtu mmoja wa karibu na familia ya wachumba hao. Vicky alipotafutwa kwa njia ya simu Jumamosi iliyopita iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa. Hata hivyo, Uwazi bado linayafanyia kazi madai hayo ambayo ni mazito na ya ndani.

Nimeiona hii kwenye Gazeti la Mwananchi online kwamba Mheshimiwa Vick ameugua ghafla muda mchache kabla ya harusi yake kufanyika. Mlioko karibu huko fuatilieni zaidi na mtujuze zaidi
attachment.php

Mfahamu Charles Gadner wa Vicky Kamata
Huyu jamaa nimemfahamu kipindi anafanya kazi sasatel miaka ya 2009.

Alikua meneja kitengo cha customer care...

Ni mtu mmoja mjanja mjanja sana na muongo wa kile anachokizungumza,anapenda sifa na ana sura ya kulazimisha ukubali anachokwambia kwa sasa sifahamu anafanyia wapi kazi japo nimepata tetesi yupo tiGo.

Aliwahi kutengeneza madai ya kuumwa sana akiwa sasatel (ugonjwa kapuni) na kudai anatakiwa akatibiwe India wengi walichanga na inasemekana alikwenda lakini ilikua janja ya nyani.

Kwa yaliyotokea kwa asilimia kubwa aliyajua before ila ni mtu asiejali kwa kifupi ni mtu wa habari za mujini na m-kitonga hasa!!!

wengine watajazia

Afya ya Mh. Vicky Kamata yazidi kuimarika
AFYA YA MH. VICKY KAMATA YAZIDI KUIMARIKA. NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WAMIMINIKA HOSPITALINI KUMJULIA HALI.

Na Steven Mruma.

Hali ya Kiafya ya Mh. Vicky Kamata aliyelazwa siku chache zilizopita, baada ya kuugua saa chache kabla ya Ndoa yake inazidi kuimarika huku ndugu jamaa na marafiki wakifika hospitalini kumjulia hali..
Asubui na mapema nilifika tena hospitali na kukuta baadhi ya ndugu jamaa na marafiki waliofika hospitalini hapo kumjulia hali Mh. Vicky..
Akiongelea afya yake Mh. aliendela kuwashukuru wote wanao muombea akiamini Mungu amesikia maombi yao na kwasasa hali yake imezidi kuimarika na anaweza kuruhusiwa wakati wowote kuanzia sasa.
Baadhi ya ndugu zake [wadogo zake] waliofika kumjulia hali
Mh. Vicky akiwa mwenye furaha baada ya kuwaona baadhi ya ndugu zake waliofika hospitali kumjulia hali
Kwa ufupi hiyo suti nyeusi ikipambwa na shati jeupe na tai ya dhambarau ndio ilikua ivaliwe siku ya harusi ya Mh. Vicky Kamata. [Pembeni kulia ni mdogo wake Mh. Vicky akiwa na gauni la Dhambarau [pupple] ilikuwa ni sare ya harusi

Mh. Ummy Mwalimu akiwa hospitali alipokuja kumuona rafki yake kipenzi Mh. Vicky Kamata
Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na Mh. Vicky alipomtembelea hospitli mapema Leo
Mh. A. Mshama nae alifika hospitali kumjulia hali rafki yake wa karibu Mh. vicky Kamata

Ijapokuwa alikua Hospitali watu mbalimbali walifika na zawadi zao kuonyesha upendo
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    47.9 KB · Views: 5,665
This goes to vicky, pole sana kuna mambo ambayo money can not buy, while mambo yote uliyokuwa unafanya yilikuwa fun, now reality comes in- majuto ni mjukuu!!!!
 
Ni matukio nadra kutokea katika maisha, lakini haya ndiyo yaliyomkuta Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Vicky Kamata, baada ya kuugua ghafla saa 36 kabla ya harusi yake.
Kuugua kwa bibi harusi huyo mtarajiwa, kumezua gumzo katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma na maeneo mengine nchini, kutokana na kile kilichoelezwa kwamba harusi hiyo ilipangwa kuwa ya kifahari ikitarajiwa kutumia Sh96 milioni.

Kamata ilikuwa afunge ndoa leo katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi, Sinza Dar es Salaam na tayari kadi za mialiko zilishasambazwa kwa watu mbalimbali wakiwamo wabunge.

Habari za kuugua ghafla kwa mbunge huyo ambaye pia ni msanii wa muziki aliyetamba na kibao chake cha ‘Wanawake na Maendeleo' zilianza kuzagaa kwa kasi juzi jioni nchini.

Kamata ambaye pia ni mtetezi wa haki za wanawake, aliugua usiku wa kuamkia jana na kupelekwa katika Hospitali ya Tabata General, iliyopo Segerea ambapo amelazwa.

"Niliugua tumbo ghafla, nilipata maumivu makali sana nikampigia daktari wangu na nilipomweleza jinsi ninavyojisikia, aliniambia niende hospitali haraka na kutokana na hali ilivyo, waliamua nilazwe," alisema Kamata akiwa kitandani katika hospitali hiyo.

Kamata alifafanua kuwa, pamoja na mambo mengine, hali yake ya ujauzito imekuwa ikimsumbua na kuchangia yeye kulazwa kwa mara ya pili sasa katika kipindi cha wiki mbili. Mbunge huyo ambaye alitakiwa kufunga ndoa leo, alisema kuwa kutokana na maradhi hayo, haelewi hatima ya ndoa yake, ingawa wanafamilia na wanakamati wanaendelea na mipango ya harusi kama ilivyopangwa.

"Mama anaenda nyumbani sasa hivi kuniandalia nguo na kila kitu, lakini sijui itakuwaje kwa sababu daktari amesema kutokana na hali yangu ilivyo, itakuwa vigumu kuvaa viatu virefu na kupata usumbufu wote wa purukushani za harusi," alisema.

Aliongeza kuwa mipango yote ya harusi ipo tayari kinachosubiriwa na siku yenyewe, lakini kwa bahati mbaya jambo hilo limetokea na haliwezi kuepukika.

Vicky alisema wanakamati wa Dar es Salaam na wale wa Dodoma, wanaendelea na vikao ingawa, wamechanganyikiwa kutokana na sintofahamu iliyopo, kama harusi itafanyika au haitafanyika.

Ndugu wa mbunge huyo akiwemo mama yake mzazi Kamata walionekana hospitalini hapo wakiendelea kumfariji na kujadili kuhusu hatima ya harusi hiyo, iliyokuwa ikingojewa kwa hamu na wanafamilia wote.

Daktari wa Kamata, aliyefahamika kwa jina la Diwani Msemo, alieleza kuwa mbunge huyo alifika hospitalini hapo akiwa na maumivu makali ya tumbo yaliyofanana na uchungu wa kuzaa, hali iliyoonyesha kuwa ujauzito wake unatishia kutoka.

"Ukipata yale maumivu kama mimba ni changa inakuwa kama tishio la mimba kutoka, siyo hivyo tu, bali alikuwa anatapika na presha ikashuka. Kwa kweli mimba yake ipo katika hatari," alisema

Alisema pamoja na kumpa matibabu, walishauriana kuwa apumzike kwa siku tano ili kuhakikisha kiumbe kilichopo tumboni kipo salama.

"Ilikuwa ni uamuzi mgumu kwa sababu ni siku yake ya harusi, lakini tunaangalia umuhimu wa kiumbe na kama ataenda, itabidi asaini ili ijulikane kuwa hatukumkubalia. Kwa kifupi hayuko fiti kwa shughuli hiyo," alisema.

Harusi ya Kamata iliandikwa pia na mitandao mbalimbali ya kijamii nchini na jana redio moja ilitangaza kuugua kwake, ikisema kumetokana na matatizo ya ujauzito.

Kumekuwa na uvumi unaosambazwa kwa kasi juu ya sababu za kuahirishwa kwa harusi hiyo, lakini kwa sababu ya maadili ya uandishi hatutaweza kuziandika katika gazeti hili.

Paroko aliyekuwa afungishe ndoa anena

Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi , Sinza Dar es Salaam, Cuthbert Maganga alipohojiwa kuhusu taarifa za kufungwa kwa ndoa hiyo, alikiri kwamba iliandikishwa ili ifungwe kanisani hapo.

Hata hivyo akasema ilishindikana, baada ya wahusika kukwama kuwasilisha baadhi ya nyaraka muhimu zilizohitajika, ili kukamilisha sakramenti hiyo.

"Ilitarajiwa kufungwa Mei 24 mwaka huu yaani kesho (leo), lakini kwa taratibu za kanisa letu ilishindikana kwa sababu bibi harusi alishindwa kuwasilisha cheti chake cha ubatizo, pia hakuwa amepata kipaimara, vitu hivyo ni miongoni mwa vitu muhimu vinavyohitajika ili kukamilisha Sakramenti ya Ndoa," alisema Padri Maganga.

Alisema Kamata ndiye aliyekwenda kuandikisha ndoa hiyo, kwa kuwa ni muumini wa kanisa hilo anayetokea Kanda D.

Juhudi za kumtafuta bwana harusi, Charles Gardner hazikuweza kufanikiwa baada ya simu yake kuita bila kupokelewa, hata alipotumiwa ujumbe wa maandishi hakuwa tayari kujibu.

Hata hivyo, baadhi ya rafiki wa karibu wa Gardner walieleza kuwa wamejulishwa kuwa ndoa hiyo haipo na kwamba jana bwana harusi huyo mtarajiwa alionekana akiwa katika hali isiyo ya kawaida.

"Nilijaribu kumuuliza kuhusu harusi yake, lakini hakuwa tayari kunieleza bayana, ila hayupo katika hali yake ya kawaida," alisema mmoja wa rafiki zake.

Imeandikwa na Florence Majani, Daniel Mjema na Beatrice Moses
Mbunge Vicky Kamata augua - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
Hivi kanisa wakijua Bi harusi tayari mjamzito hivi watafungisha ndoa kweli?.......Hapo nahisi si ungonjwa ila kuna kitu nyuma ya pazia ila pole yake jamaa yuko fasta ashaweka kitu hatari
 
Mbona nasikia imeota mbawa watu wanadhani unaoa tu vimegharamiwa hivyo mpk vikafika hapo.
 
Pole yake.
Kwa maana hiyo hata asingeugua kuna kuna nyaraka ambazo hakuwakilisha pia!!!
Kuna lisilosemwa hapo!!!
 
Jana Clouds walikuwa Hewani na Daktari wake wanasema kalazwa yupo hoi na mimba ya miezi 4 inataka kutoka ! kipindi cha Leo tena Regina Mwalekwa ndio aliokuwa anarusha hiyo Taarifa ! na kwamba Harusi Haitakuwepo leo
 
Kiu fupi kawekewa pingamizi na wanaume aliozaa nao watoto watatu wa kwanza , hayo ya vyeti ni kumlindia heshima tu .......haka ka dada ni kuchafua sana .....
 
Mhh sasa swala la vyeti ndio linatokea dakika za mwisho ? wangefunga zao Serikalini au kwa Mama Lwakatare Basiii hakuna Msafi anyway .....
 
Maskini Vicky yamekuwa haya basi vyakula hivi wapelekewe watoto yatima Mungu amunusuru. Hapa kuna mguu wa MTU. Haiwezekani mbwembwe zote 96 mil ziishie hivi.
 
Jana Clouds walikuwa Hewani na Daktari wake wanasema kalazwa yupo hoi na mimba ya miezi 4 inataka kutoka ! kipindi cha Leo tena Regina Mwalekwa ndio aliokuwa anarusha hiyo Taarifa ! na kwamba Harusi Haitakuwepo leo

Gazeti la mwananchi linasema eti paroko anasema haikidhi vigezo au ni kwa sababu hii kwenye red? au mwoaji kalala mitini amegundua anataka kubambikiwa mimba?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom