Mbunge: Vibaka walinikaba hivi...... Apigwa Salender Bridge; Nilidhaini kulikuwa na CAMERA POLICE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge: Vibaka walinikaba hivi...... Apigwa Salender Bridge; Nilidhaini kulikuwa na CAMERA POLICE

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 29, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145

  JUMATATU, OCTOBA 29, 2012 05:23 NA GABRIEL MUSHI, DAR ES SALAAM

  [​IMG]

  Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa


  MBUNGE wa Iringa Mjini, (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa, ameeleza namna alivyovamiwa, kupigwa na kuporwa na vibaka maeneo ya Daraja la Salenda, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

  Akisimulia mkasa huo jana, Mchungaji Msigwa alisema, alikabwa na vibaka juzi, saa moja usiku wakati akitokea katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

  "Siku hiyo Kamati yetu ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira, tulikuwa tumekwenda kutembelea Msitu wa Ruvu Kusini na wakati narudi nilipitia ile Barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

  "Nilipofika maeneo ya Daraja la Salenda Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, ghafla gari yangu ilipata hitilafu katika upande wa tairi, ndipo nikashuka pamoja na dereva wangu ili kukagua.

  "Kabla ya kushuka, nilimwambia dereva wangu anayeitwa Baraka, apaki pembeni kidogo ili asisababishe foleni. Tulipolikagua gari, tukakuta kuna kasoro zilizosababisha tairi zisiweze kuzunguka vizuri.

  "Dereva wangu alichukua jeki na kuanza kutengeneza gari, wakati huo mimi nikawa nazungumza na mtu kwenye simu yangu, pembeni ya ukuta wa daraja. Ghafla mbele yangu wakatokea vijana kama nane hivi, wakawa wananisogelea, mimi nikaamini wale labda wamekuja kunisaidia kumbe sio.

  "Waliponikaribia, nikawauliza wanataka nini, wakaniambia kaa kimya, kwa kuwa mimi ni mbishi, nikaendelea kuzungumza na simu, lakini mmoja wao akaanza kuninyang'anya ile simu nikawa naing'ang'ania, kwa sababu najua ina namba nyingi za watu.

  "Nilipozidi kuonyesha ubishi walizidi kunikaba, wakati huo baadhi yao waliendelea kumminya dereva wangu ambaye tayari alikuwa kule chini ya gari akilitengeneza.

  "Lakini mimi nikapambana na wawili niliokuwa nao nikawa nakaribia kuwashinda, hata hivyo wakaongezeka tena, ndipo wakafanikiwa kunidhibiti na kuninyang'anya simu yangu na nyingine zilikuwa kwenye gari, wakachukua pia na fedha taslimu Sh 400,000 na baadhi ya vitu vidogo vidogo vilivyokuwa kwenye gari, isipokuwa Ipad hawakufanikiwa kuiona kwa sababu ilikuwa kwenye kioo cha mbele cha gari.

  "Kusema kweli walinipiga kisawasawa, wakaniumiza mguu kidogo na jicho, wakaniharibia na meno yangu mawili ya bandia.

  "Wakati wananikaba, wengine walimkamata dereva wangu na kumtupa baharini, lakini nashukuru hakudhurika. Baadaye tukapata msaada kwa askari polisi waliofika eneo la tukio, ingawa walichelewa kufika.

  "Hata hivyo, sasa hali yangu inaendelea vizuri kwa sababu hapo awali nilikuwa na tatizo la mguu, ambao mwezi uliopita nilikwenda Ujerumani nikaanguka na kufanyiwa uchunguzi, lakini niliporudi nchini Oktoba tisa, nilifanyiwa upasuaji na sasa naendelea vizuri kwa sababu nategemea kutoa hili hogo kesho," alisema Mchungaji Msigwa.

  Akizungumzia eneo hilo jinsi lilivyo, alisema limekuwa na historia ya watu kukabwa na kuibiwa fedha na vitu mbalimbali.

  "Kwanza ni aibu sana kwa sababu ni eneo ambalo lipo karibu na Kituo cha Polisi, lakini ukiwauliza askari wanadai eti wakitaka kuwakamata hao vibaka huwa wanakimbilia baharini.

  "Wapo pia wabunge mbalimbali nimesikia walishawahi kukabwa hapo na kuibiwa Sh milioni moja, ingawa hawakutaka kusema, mimi ni msema kweli nimesema kwamba walinikaba.

  "Vivyo hivyo, nilishawahi kusikia huyu Kigogo wa JWTZ anayeitwa Shimbo, naye alishawahi kukabwa baada ya kufika eneo hilo baada ya kushuka kwenye gari na kuanza kujisadia haja ndogo," alisema.

  Kwa mujibu wa habari iliyochapishwa na gazeti moja linalochapishwa kila siku toleo la jana (siyo MTANZANIA), Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Komba, alisema vibaka wawili wameshakamatwa na leo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.


   
 2. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,636
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Pole Mh, lakini ujifunze kutii amri hata kama ni vibaka ungewapa wanachotaka wasingekutoa manundu umeona sasa faida ya ubishi?
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Juzi Jumamosi, nimeshuhudia 'live' kibaka akimuibia mama mmoja hapo hapo Selandar Bridge.

  Ni hivi, kulikuwa na foleni, na mama wa watu akiwa peke yake kwenye gari alikuwa anaendesha toka mjini kuja upande wa ubalozi wa ufaransa. Alikuwa kwenye lane ya kushoto. Kwenye hako ka-msitu, ukishavuka daraja (toka mjini) kuna kijana anapenda kutembeatembea huku akiwa mchafu utadhani ni kichaa. Ukimuona tia lock milango ya gari maana huyu ndiyo kibaka-kiongozi.

  Alichokifanya juzi baada ya kuona magari yanatembea taratibu kwa sababu ya foleni, alianza kusogelea magari na kuchungulia ndani kuna nini. Kwenye gari ya huyo mama aliona mkoba (handbag), ghafla tukaona kafungua mlango wa gari na kuchuku mkoba kisha akatomea kwenye hicho ki-msitu. Nadhani kuna wenzake humo porini. Pilice walikuwepo na watu wengi walijitahidi kumkimbiza lakini kwa bahati mbaya kuna tope na yeye mwenyewe (mwizi) alishafanya 'training' ya kukimbia kwenye tope.

  Nadhani kuna haja ya kuongeza doria eneo hilo. Hata ombaomba wa hapo si wa kuamini tena. Ukimuona huyo kibaka hutashtuka hata kidogo maana anaonekana kama kichaa kumbe yuko kikazi zaidi.
   
 4. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  yaani nipo radhi nitembelee rim pale salenda kama gari ikipata pancha, kuliko kukutana na ma-agent wa polisi! haiwezekani washindwe kudhibiti kikundi kidogo cha wezi, sasa hao ni polisi au ni sungu sungu??? pathetic, pole mchungaji! mjini mipango baba!
   
 5. Advicer

  Advicer JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 429
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  msigwa bwana anafurahisha sana mbunge wangu huyu anamuumbua kakabraza kuwa alikabwa wakati anachafua mazingira(anakojoa)!!!!!)(pole kiongozi getwell soon

   
 6. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Pole sana mh acha ubishi katia bima vitu vyako vyote, wakija siku ingine unawapa tu bila ubishi na wewe utaenda dai bima.
   
 7. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  wewe always unaongea pumba! sijui na wewe unaitwa great thinker au great fool! utasalimu je amri kirahisi hivo mwanaume unapambana hata ijapo kufa ni heri kufa ukiwa unapambana kuliko kufa ukiwa umepiga magoti unaomba msamamaha, msigwa amedemonstrate kwa vitendo ule ujasiri anaohubiri bungeni na kwingineko, huenda na wewe ni kibaka ndio maana unashabikia vibaka!!
   
 8. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  anadai walimtandika kweli kweli
   
 9. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ingekuwa kule Japan IGP Saidi Mwema kazi basi, haiwezekani IGP anayelipwa mshahara mkubwa,marupurupu kibao anashindwa kuwasimamia polisi wake. Hao polisi wanafuga wezi mita chache kutoka eneo la ikulu,wanachukua rushwa mchana kweupee.
   
 10. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
   
 11. y

  yaya JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, pamoja na zile namba za simu pia atazipata?
  Mimi nadhani badala ya kukomalia ubishi wa Mhe. Msigwa, ilitakiwa polisi waoneshwe aibu yao kwa kuwaruhusu vibaka kuwa na uwanja mpana wa kutamba hadi upenuni mwa ofisi zao pale Salender bridge.
   
 12. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sijaona mahali Mbunge ameitaja hiyo "Camera Police" kwani ulikuwa unamaanisha CCTV?
   
 13. M

  Mshind Member

  #13
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole! principle of security don't trust any one at any time!
   
 14. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  602323_517882858222633_1815971871_n.jpg
  kwikwiiwki hii ndio khali halisi mwambie asilie anyamaze kimya
   
 15. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Hapo ndo unaona umhimu wa kutembea na wapambe ndani ya gari
   
 16. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
   
 17. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
   
 18. S

  Shembago JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni aibu daraja lipo very close na kituo nadhani hii ni network ya Polisi
   
 19. n

  natangaduaki Member

  #19
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Pole sana mheshimiwa. Tuwaombee wakamatwe na vile vile wageuke tabia zao waokoke nakuamua kumfuata yesu kristo aliye hai.
   
 20. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #20
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe kwamba hao ni ma agent wa polisi. Haiingii akilini inakuwaje uhalifu ufanyike hapo just few meters kutoka kito cha polisi?

  Tiba
   
Loading...