Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,187
- 670
kulikoni mpaka akatakiwa wangwe asichachawe kwa ziara jimboni mwake? na kwa nn kaka yake nae yumo ktk msafara utaoenda huko?
Mbunge Tarime atakiwa asihofu ziara ya CCM Makubo Haruni, Musoma
Daily News; Thursday,March 27, 2008 @00:04
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mara kimemtaka Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, kuacha hofu kwamba wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) waliopangwa kufanya ziara wilaya za Tarime na Rorya, wamefanya hivyo kumdhoofisha.
''Lengo letu ni kuimarisha chama chetu na wajumbe wako mkoa mzima, alisema Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Makongoro Nyerere alipozungumza na waandishi wa habari jana kuhusiana na vikao vya NEC vinavyoanza hapa keshokutwa.
Wajumbe 80 wa NEC wamepangwa kutembelea wilaya za Tarime na Rorya, ambako ndiko kwenye jimbo la Wangwe ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Miongoni mwa wajumbe wa NEC waliopangwa katika wilaya hizo ni Profesa Samwel Wangwe ambaye ni kaka wa mbunge huyo wa Chadema.
Makongoro alisema wajumbe wa NEC wapatao 260 wamefika mkoani hapa siku mbili kabla ya kikao chao na leo wamegawanyika katika wilaya za Musoma, Tarime, Rorya, Bunda na Serengeti, wakiwa na lengo hilo sambamba na kuzungumza na wananchi kujua matatizo yanayowakabili.
Alisema baada ya kukamilisha hatua hiyo ambayo pia itatoa fursa ya kuimarisha chama hicho kwa kupokea wanachama wapya, wajumbe hao kwa ujumla wake, kesho watakwenda Jimbo la Musoma Vijijini kwa ajili ya kutembelea miradi iliyotekelezwa na Mbunge wa huko, Nimrod Mkono.
Alisema baada ya kumaliza, watakwenda Butiama keshokutwa na kuanza kikao chao kitakachofunguliwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete, katika mkutano utakaofanyika mahali alipozaliwa na kuzikwa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.
source habarileo.com