beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Mbunge wa Kinondoni, Tarimba Gulam Abbas amehoji ikiwa Serikali haioni ni muda mwafaka wa kulifumua Shirika la Umeme (TANESCO) ili kuwe na Kampuni tatu kwa ajili ya kufanya Generation Uzalishaji, Usafirishaji na Usambazaji kama ilivyo Nchi nyingine.
Akimjibu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kukatwa na kutolewa kwa maeneo hayo kwa watu tofauti kunaweza kuleta athari kwenye Usalama wa Nchi pale Umeme unapohitajika wakati wote na mmoja ya waliopewa jukumu awe anaenda kinyume na mipango, hivyo malengo kushindwa kufikiwa.
Amesema kwa Hali iliyopo Nchini, maeneo yote ya Uzalishaji umeme yanaendelea kufanya hivyo lakini changamoto ni miundombinu ambayo hata sasa inapeleka baadhi ya maeneo kukatiwa Umeme.