Mbunge Tarimba Abbas (CCM) je, wana Kinondoni tulikutuma Bungeni kuzungumza matatizo yetu au kuizungumzia Yanga SC yako tu?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,871
Leo ni mara ya Pili (kama siyo ya Tatu) nakuona kila ukipewa muda wa Kuongea Bungeni Wewe Kazi yako ni Kuisemea tu Yanga SC yako na Kuonyesha pia chuki zako za wazi wazi kwa Rais wa TFF Wallace Karia na Klabu Hasimu Kwako ya Simba SC.

Hivi Wewe Mbunge wa Kinondoni Tarimba Abbas (CCM) ulipigiwa Kura zile na wana Yanga SC wa Kinondoni au na wana Kinondoni wote ili ukienda huko Bungeni Dodoma ukawasemee Matatizo yao?

Mbunge Tarimba Abbas (CCM) ni nani aliyekudanganya kuwa kila unapopata muda wa Kuongea Bungeni basi ukiwa unaongelea Soka la Bongo, unaisema (unainanga) sana Simba SC na Kuonyesha wazi wazi chuki zako kwa Rais wa TFF Karia ndiyo Ubunge wako unakubalika na unapata Sifa kwa Watu?

Ina maana Tarimba Abbas (Mbunge CCM Kinondoni) umesahau kuwa Kero zetu Kuu wana Kinondoni kama Uwizi (Ujambazi), Biashara holela ya Dawa za Kulevya, Kuongezeka kwa idadi ya Mabwabwa ( Mashoga ), Kufurika kwa Gereji Bubu nyingi zinazohatarisha Afya za Wakazi, Kuongezeka kwa Madanguro na Mitaro mibovu ya Maji inayosababisha Mafuriko makubwa maeneo ya Kinondoni kipindi cha Mvua ndizo tumekutuma ukaziwakilishe huko ili zisikike na Serikali iyapatie ufumbuzi wa haraka na wa Kudumu?

Leo hii bila hata haya (aibu) Mbunge wa Kinondoni CCM Abbas Tarimba unashutumu Soka la Tanzania kuwa limejaa ' Ubabaishaji ' mwingi na ' Kuinanga ' sijui TFF na Karia wake kwa kuibeba Simba SC na ukiwa unajisahaulisha ni katika Uongozi wako ulipokuwa Yanga SC kwa Kushirikiana na Rais wa TFF wakati huo (tena mwana Yanga SC Mwenzako) ndiyo mliuharibu Mpira wa Tanzania kwa Kuhonga Timu Pinzani, Kufanya ' Umafia ' wa Kuionea Simba SC kwa Baraka zote za aliyekuwa Rais wa TFF Kipindi chako.

Mbunge Tarimba Abbas (CCM Kinondoni) utawadanganya tu ' Wapuuzi' na ' Wanafiki ' Wenzako ila kwa Mimi GENTAMYCINE ninayekujua vyema na hasa ile Michezo yako (iliyopelekea Kuharibu Kikazi Kikubwa) cha Vijana na Mabinti wa Kinondoni wala hunipi taabu ila nakustahi tu kwakuwa ni mwana CCM Mwenzangu ila ukiendelea na huu Upuuzi na Unafiki wako sitosita sasa kuanza ' Kukuanika ' uliyokuwa ukiyafanya na uyafanyayo pia.

Najua kuwa unamchukia sana Rais wa TFF Wallace Karia kwakuwa kuna ' Dili ' la Kampuni yako ya ' Betting ' ulitaka upige nae (kwa njia za Panya) Yeye akakukatalia na kukutaka ufuate Utaratibu.

Najua kuwa unaichukia Klabu ya Simba kwakuwa imeshaonyesha kuwa inaweza isiendee Kudhaminiwa na ' Spoti Pesa ' yako baada ya Simba SC kugundua kuwa haifadiki ipasavyo na ' Sponsorship ' yenu (tena mnainyonya) vilivyo na kufikiria kuingia ' deal ' na Kampuni nyingine Kubwa tu duniani.

Nina mengi tu juu yako Mbunge wa Kinondoni CCM (Abbas Tarimba) ila nakuomba acha kucheza na Akili za Wapumbavu wengi wanaokuamini na ukidhani Sisi Werevu wachache akina GENTAMYCINE hatupo au tumelala bali tunakuangalia tu huku tukikupuuza huku tukijua pia mwisho wako wa Kisiasa upo wapi.

Humo Bungeni ulipo Simba SC ina Wabunge wengi kuliko Yanga SC yako (na tena wenye Vyeo vikubwa tu Serikalini ) Kukuzidi je, umeshawahi kuwaona wakiwa na Ushamba (Umbwiga) kama ulionao wa Kuizungumzia Simba SC yao kila wapatapo muda wa Kuchangia hapo Bungeni?

Sasa kama Wewe Tarimba Abbas (Mbunge CCM Kinondoni) kila ukipewa nafasi ya Kuongea Kazi ni Kuzungumzia tu Mpira wa Miguu na Yanga SC hivi Waziri wa Michezo Bashungwa na Naibu wake wao wakisimama wawe wanazungumzia nini? au unazungumzia sana Michezo ili 'umshawishi' Rais (Mama) Samia akupe Ubunge kisha akupe Uwaziri wa Michezo ulipize Kisasi na uendelee Kuibeba ( Kuipendelea) Yanga SC yako? Unaboa sana Mnafiki Wewe.

Wewe endelea tu 'Kuibwabwajia' Yanga SC yako hapo Bungeni na kuacha Kuzungumzia Kero za Kinondoni ukidhani 2025 ni mbali na kwamba hata hiyo 2025 ule Mchezo wa ' Kimafia ' ulioratibiwa vyema na aliyelala Kimoja Chato utajirejea na kupita kirahisi hapo Kinondoni.

Tena na hivi ulivyoanza Kutuudhi na Kutukera wana Kinondoni ni Mimi GENTAMYCINE na Kamati yangu ya Roho Mbaya kama iliyomuangusha Mpuuzi Mwenzako mwingine kule Kigamboni (japo tulihatarisha hadi Uhai Wetu) na leo haamini tutakufanyia nawe ' Fitna ' zile zile na wala ' hutotoboa ' hata 'Uhonge ' vipi na japokuwa ni wana CCM ila tutaamua hilo Jimbo bora tu liende kwa Upinzani (Mpinzani) na hapa ninamaanisha hivyo taratibu anza sasa kujiandaa Kisaikolojia

Sindano yangu hii ikuingie vyema sana.
 
Watu wananishangaza sana, unataka kuniambia huyu mtu alishinda ubunge? hawa ni wale walichaguliwa na wakurugenzi kwa maagizo na amri ya alie kwa shetani sasa hivi, unamufahamu, so ile iko subiri miaka 5 iishe ndio mbunge wa kweli ambae atachaguliwa na watu wa kinondoni atakuwa pale dodoma, asante
 
Mkuu mimi nili kua namskiliza.uku mwili wote unanitetemeka kwa hasira,jamaa mpuuzi sana. Na bwana kitenge na mwenzie mkule wakaishupalia sana eti wabunge wakosoa uendeshaji wa soka nchini.

Uzuri edo akamwambia lakini hao wote waliongea ni yanga,jamaa anakoma hilo umesema wewe edo.

Nahisi hii ni agenda ya utopolo.
 
Mkuu mimi nili kua namskiliza.uku mwili wote unanitetemeka kwa hasira,jamaa mpuuzi sana....
Wananchi wenyewe wa Kinondoni, labda matatizo ya msingi jimboni yameisha, hivyo sasa hayo anayokomalia zaidi ndo vipaumbele mlivyomtuma siye tutajuaje.

Mbunge mwenyewe hivi bado vilevile, si huwa kama sikosei ni mkurugenzi wa Bahati Nasibu ya Taifa or shirika la Betting nk.....kazi iendelee.
 
Katika aliyoseama tarimba ni kipi cha uongo? Kwakuwa yeye ni yanga, basi akae kimya jinsi hao waovu na huyo muovu mkuu,wanavyofanya dhudi ya Yanga?

Kwa akili yako fupi, unadhani kuwa tarimba hana analofanya kuhusu kero za jimbo lake? Acha udwanzi
 
Mimi nashauri timu yangu ya Simba tuipige chini mazima sport pesa yake bora hiyo space tuendelee kuitangaza nchi yetu Tanzania hata bure kabisa, kama vipi tuchangie kama tulivyofanya kwenye fans card.
 
Yaani Mimi nilishangaa sana kumbe hata mijitu mikubwa ya utopolo Ina akili za ovyo ovyo kama za mashabiki zao. Ile timu ukiishabikia unakua umeamua kuharibu akili zako asee.

Nilikua siamini kwenye kudemka ila jana nimeshuhudia wabunge wale wakidemka. Mama shikamoo ulivyosema mwanzoni sikukuelewa ila sasa nimeelewa kudemka ni namna gani.
 
Kwani imesemwa SIMBA au TFF ya KARIA?
Mbona simba ndo mnawashwa kwani hampendi maendeleo ya michezo nchini?
Inajulikana sasa hivi ni korona lakini wanamlazimisha Karia aanze kushikana mikono na watu tofauti na protoko za covid na Karia anajua impact ya yeye kufanya hivo ni sawa na kuzika protoko hizo kwenye Soka letu.

Mbona hawajalalamika raisi madam kutoshika watu mikono? Hawa wabunge wamuombe Karia msamaha wamemuonea tena kumtaja sehemu ambayo hawezi kujitetea hiyo sio sawa.
 
Inajulikana sasa hivi ni korona lakini wanamlazimisha Karia aanze kushikana mikono na watu tofauti na protoko za covid na Karia anajua impact ya yeye kufanya hivo ni sawa na kuzika protoko hizo kwenye Soka letu.
Mbona hawajalalamika raisi madam kutoshika watu mikono? Hawa wabunge wamuombe Karia msamaha wamemuonea tena kumtaja sehemu ambayo hawezi kujitetea hiyo sio sawa.
Kwa hiyo ni KARIA tu anayefuata protocol? Vipi wengine pale jukwaa kuu?
Kungekuwa na hiyo protocol ingetangzwa kwa wote kwenye tukio lile!
Karia kashiba mpaka kavimbiwa , anadharua wadau!
 
Kwa hiyo ni KARIA tu anayefuata protocol? Vipi wengine pale jukwaa kuu?
Kungekuwa na hiyo protocol ingetangzwa kwa wote kwenye tukio lile!
Karia kashiba mpaka kavimbiwa , anadharua wadau
Hujui kuwa jukumu la kujilinda afya yako ni lako binafsi?
 
Back
Top Bottom