Mbunge Taletale: Rais Magufuli nakushukuru kwa kunitoa chini kabisa na kunifikisha juu nikiwa kijana mdogo kabisa bungeni

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,785
141,680
Mbunge wa Morogoro kusini mashariki Khamis Taletale aka Babu Tale amemshukuru Rais Magufuli kwa namna alivyombeba kutoka chini na kumpandisha akiwa kijana mdogo kabisa kule bungeni.

Babu Tale amesema hayo kwenye uzinduzi wa kiwanda cha Mahashree Agro Processing Ltd mjini Morogoro.

Babu Tale amemwomba Rais Magufuli amjengee barabara ya Bigwa kwani yeye hana uwezo.

Chanzo: ITV

Maendeleo hayana vyama!

“Rais Magufuli, Mimi ni mmoja kati ya Watu wanaotembea kifua mbele nikiona maajabu yako kwangu, kwasababu umenitoa chini kuniweka juu na kunipa heshima, hizi zote ni nguvu zako kupitia CCM, Mimi kuanzia leo ni Chawa wa John Pombe Magufuli”-Tale mbele ya JPM
 
Hivi hata malaika akiingia ccm anajitoa akili sio?
 
“Rais Magufuli, Mimi ni mmoja kati ya Watu wanaotembea kifua mbele nikiona maajabu yako kwangu, kwasababu umenitoa chini kuniweka juu na kunipa heshima, hizi zote ni nguvu zako kupitia CCM, Mimi kuanzia leo ni Chawa wa John Pombe Magufuli”-Tale mbele ya JPM
Ila Morogoro bwana, anyway!
 
Mimi sijamuelewa kabisa Babu Tale..kulikuwa na mengi tu ya kumuomba Rais kwa ajili ya wananchi wake kuliko hizo sifa alizokuwa anataka kujitengenezea
 
Back
Top Bottom