Mbunge Tabasamu amtumia Rais Samia video ya ufisadi unaoendelea Sengerema

Mbunge wa jimbo la Sengerema mh Khamis Tabasamu amemtumia video Rais Samia Suluhu inayoonyesha ufisadi wa zaidi ya billioni 70.3 zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la halimashauri hiyo.
Picha zinaonyesha ujenzi wa ghorofa hilo unaendelea huku kumbe msingi haukujengewa wala kuchimbwa kama inavyotakiwa badala yake ni nondo tu zimesukwa kwa juu yake!
Mh Tabasamu amsema si Takukuru, wala mkuu wa mkoa wala wilaya wanaohangaika na ufisadi huo.
.https://youtu.be/loKyT6CareI
Mfumo mbovu hii hahiitaji Raisi
 
Mfumo mbovu hii hahiitaji Raisi
Mliberali hapa umenena. Watanzania bila kujitambua tumelemazwa akili vibaya sana hata walio na mfumo wa kilfalme hawajalemaa kiasi tulicholemazwa. Huwezi kusikia Uingereza, Canada, Japan nk jambo kama hili likimsubiri au akipelekewa Malkia/Mfalme kuombwa awashughulikie wahusika. Ni aibu iliyoje. Halafu kiongozi mwingine anafanya jambo la hovyo anapoulizwa sababu anawajibu wananchi ni maagizo kutoka juu! Mfumo mbovu sasa umezaa akili mbovu na sasa, Mungu atuepushe, tunaelekea ushetanini kabisa. INASIKITISHA!
 
Hii ndiyo ccm ya Ikweta na wanaomshambulia Polepole!. Hii ndiyo ccm ya siku zote. Kutenda haki ni jinai,. Uaminifu ni ujinga, na ukweli ni uharifu. Hukumu yako n i korimba.

Mbunge wa jimbo la Sengerema mh Khamis Tabasamu amemtumia video Rais Samia Suluhu inayoonyesha ufisadi wa zaidi ya billioni 70.3 zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la halimashauri hiyo.
Picha zinaonyesha ujenzi wa ghorofa hilo unaendelea huku kumbe msingi haukujengewa wala kuchimbwa kama inavyotakiwa badala yake ni nondo tu zimesukwa kwa juu yake!
Mh Tabasamu amsema si Takukuru, wala mkuu wa mkoa wala wilaya wanaohangaika na ufisadi huo.
.https://youtu.be/loKyT6CareI
My lord

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Katika hii awamu hizo billion zinatajwa kama njugu yani! Wacha tusubirie ripoti ya CAG
 
Sisi huku kijijini tunajiuliza hivi: kwanini wakati wa Magufuli umeme haukukatika hivi, kwanini wezi na wabadhilifu walianikwa wazi wazi na wakaondolewa ofisini (tunasikia wengine wamerudishwa kazini), kwanini ni sasa hivi daktari wa mifugo wa Wilaya kila tukienda ofisini kwake tunaambiwa yupo Dodoma tangu mwezi agost hadi leo? Kwanini????
 
Mbona mleta mada amepotosha jamaa amedai 700 milioni na si bilioni. Mama ajitahidi kurekebisha haya madudu kabla mambo hayajaharibika.
 
Mbunge wa jimbo la Sengerema mh Khamis Tabasamu amemtumia video Rais Samia Suluhu inayoonyesha ufisadi wa zaidi ya billioni 70.3 zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la halimashauri hiyo.
Picha zinaonyesha ujenzi wa ghorofa hilo unaendelea huku kumbe msingi haukujengewa wala kuchimbwa kama inavyotakiwa badala yake ni nondo tu zimesukwa kwa juu yake!
Mh Tabasamu amsema si Takukuru, wala mkuu wa mkoa wala wilaya wanaohangaika na ufisadi huo.
.https://youtu.be/loKyT6CareI
Kwa nini kamtumia Rais?
 
Back
Top Bottom