Mbunge Susan Lyimo: Kama kweli hostel za UDSM zimejengwa kwa Mil 500, nitatoa hela zijengwe zingine

Milion 500 unajenga nyumba ya room kumi hela inaishia kwenye lenta..... Hiyo hela bado ndogo sana
Mkuu wanaweza wakajenga hizo ghorofa kwa hiyo hela lakini zikawa substandard. Nasikia wachina walikataa kujenga kwa hiyo hela. Kuna rumours kuwa zimeshaanza kuharibika. Wasiwasi wangu ni zisije zikaanguka wakati vijana wetu wameanza kukaa ndani. Zingechekiwa ubora kabla ili kuepusha madhara ya baadae ya "loss of human lives".
 
View attachment 510866 “Naomba CAG afanye ukaguzi maalum katika hostel mpya UDSM na kama kweli jengo moja linalochukua wanafunzi takribani 390 linagharimu Milioni 500 basi mimi nitatoa Milioni 500 serikali ijenge jengo lingine la ghorofa tatu ili tuweke vijana wengine”. - Susan Lyimo (Mbunge-Chadema)

Toa maoni yako




Susan ana bahati anatoka upinzani, angekuwa anatoka tawala angeitwa msaliti na kutumwa India kwenye matibabu! Kweli hosteli zile ni abracadabra!
 
mtu mzima akisema uongo unamkubalia lakini ukiendelea kuishi ukweli.
usithubutu kumkosoa kwamba amesema uongo.!
 
Hakuna kinachoshindikana.

Kujenga kwa billion kumi ni kitu kinachowezekana kabisa na chenji inaeza kubaki. Ni sawa na kumshangaa mtu anae-survive kwa mshahara wa laki tatu kwa mwezi na ana familia. Wakati wewe una mshahara wa milioni tatu uko bachelor na haukutoshi.

Kama TBA wana ma-engineer wao permanent kabla hata ya mradi, au labda tuseme waongeze wachache kukidhi mahitaji. Posho za vibarua wa Tanzania kila mtu anajua ilivokua aibu hata kuzitaja, japo ndo wanalipwa hivo. Design kuanzia architectural mpaka structural pamoja na usimamizi BICO ya CoET ipo (wasioijua BICO, ni engineering Consulting firm ya UDSM), wana wafanyakazi wanalipwa always wawe wamefanya kazi au lah, na kazi ni ya chuo chao wenyewe ni suala la kutoa maagizo tu hiyo kazi inafanyika.

Ukija kwenye material, Serikali ina share 30% twiga cement, possibility ya kupata Cement kwa bei chee upo. Kokoto na nondo ndio pekee wanaweza kununua kwa bei ya soko. Furniture zote, kuanzia vitanda, makabati yote yametoka workshop za CoET. Kwanini pesa hiyo isitoshe.

Katika mfumo wa kawaida architect atatafutwa atafanya kazi na bado atasimamia. Structural engineer atafutwa na atasimamia kazi, Contractors watatafutwa kuanzia structure yenyewe mpaka services zote (maji, umeme n.k) hapo wote inapaswa wafanye kazi kwa faida na wahakikishe pia wanakuepo site muda wote wanaohitajika. Hapo bado misunderstanding kibao zinazosababisha mradi uchelewe.

Tatizo la nchi hii ni moja tu, haijulikani imeegemea mfumo gani kama ni ubepari au ujamaa. Na kamani vuguvugu basi ijulikane, ili kila mtu kuanzia raisi mpaka housegirl ajue hilo na wote tuishi na kuzoea aina hiyo ya maisha. Ili kusudi kiongozi akija kivingine tumshangae wote kwa Pamoja. Lakini saiv hatujui tuko upande gani, makampuni mengine yanafunga biashara kwasababu wakati wanakuja waliamini sisi tunaelekea kwenye ubepari, sasa raisi Mjamaa kaja hawana chao tena, sharti wafunge virago.

JK aliendesha nchi kipebari na yale yote yaliyotokea katika utawala wake yalitokana na mfumo huo. Kaja JPM nchi inaenda kijamaa na matokeo yake ndo haya mambo yanafanyika kijamaa ile pesa iliyokua inatakiwa iingie kwenye mifuko ya watu inaenda kwenye real things. Hapo lazima watu walie tu.
 
Mkuu wanaweza wakajenga hizo ghorofa kwa hiyo hela lakini zikawa substandard. Nasikia wachina walikataa kujenga kwa hiyo hela. Kuna rumours kuwa zimeshaanza kuharibika. Wasiwasi wangu ni zisije zikaanguka wakati vijana wetu wameanza kukaa ndani. Zingechekiwa ubora kabla ili kuepusha madhara ya baadae ya "loss of human lives".


Yakitokea hayo basi utakuwa ni uzembe wa UDSM wenyewe, kwani si kuna wataalaamm pale. Wameshindwa kukagua nyummba zao wenyewe?
 
Hakuna mbunge wa chadema mwenye hoja ya msingi sasa hivi wote ni kuropoka tu wake kwa waume. Sijui wamekumbwa na zimu gani, hadi wamemuambukiza na Zito Kabwe na mropokaji siku hizi badala ya kujenga hoja
Hebu nenda kwenye hoja mkuu achana na wabunge wa upinzani hawakuhusu kabisa... Twambie mil 500 zinaweza kujenga hilo jingo... Kama hujui kaa kimya...
 
Back
Top Bottom