Mbunge Sugu awasifu wanaohama CCM kwenda CHADEMA, azidi kuihenyesha CCM mkoani Mbeya

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,780
SIASA
Na Godfrey Kahango,Chunya

Posted Ijumaa,Decemba7 2012 saa 14:43 PM

KWA UFUPI

Mbunge Sugu azidi kuihenyesha CCM mkoani Mbeya


MBUNGE wa Jimbo la Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi maarufu "Sugu" amesema kuwa kutokana na mwamko mkubwa wa wananchi mkoani Mbeya, kuendelea kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM),na kukimbilia Chadema ni ishara kwamba majimbo yote 11 ya mkoani hapo yanakwenda kutawaliwa na Chadema mwaka 2015.

Sugu alisema kuwa wananchi wameendelea kujitambua kuwa kwa kipindi kirefu walikuwa wanapotea njia huku wakiendelea kudhulumiwa na CCM hivyo kuchukua uamuzi mgumu wa kukihama kwa kasi chama hicho.

Alisema hiyo ni dalili tosha kwamba katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 hawatafanya makosa tena ya kuendelea kuwachagua wabungeakupitia CCM na badala yake watakiunga mkono Chadema kwa kushika majimbo yote ya mkoani hapa.

Sugu alitoa kauli hiyo wakati akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Saza wilayani Chunya kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa mahususi kwa kampeni za chama hicho kwa mgombea wa kiti cha Mwenyikti wa kijiji hicho zinazotarajiwa kufanyika Desemba 9 mwaka huu.

Alisema kuwa CCM ilionekana kutawala kwa kipindi kirefu huku wananchi wakilazimika kufanya hivyo kwa kuwachagua viongozi wao kutokana na kutokuwapo kwa chama makini chenye uwezo wa kuwatetea wananchi wake ndiyo maana hadi leo hii wananchi wanazidi kuwa maskini wa kutupwa.


"Nataka kusema hivi ndugu zangu wa Saza, kuwa kutokana na mwamko wenu wa kijitambua kuwa CCM ndio adui namba moja wa kufilisi mali zenu, hivyo kuchukua uamuzi mgumu wa kukihama na kuja Chadema ni ishara kwamba hamtafanya makosa tena 2015,'' alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mbeya Mjini, John Davi Mwambigija maarufu "Mzee wa Upako" aliwarushia kijembe viongozi wa CCM, akisema kuwa chama hicho na watu wake ni maadui na wanatakiwa kuogopwa kama ukoma kwani ndio walioleta umaskini miongoni mwa

Watanzania wasiokuwa na hatia.

Alisema kwamba hakuna sababu ya kukimbia ukweli kwamba katika mazingira hayo wanachama wengi wa CCM wanatambua kwamba kwa sasa hatima ya chama hicho inaelekea ukingoni ambapo hakuna sababu ya kuendelea kung'ang'ania kuendelea kuwa ndani ya chama hicho ambacho kinaonekana kupoteza mwelekeo.

 

nemasisi

JF-Expert Member
Oct 4, 2012
1,957
566
Ndiyo sugu nenda hadi chunya, msisahau mbarali na ileje..kote wanawasubiri tunataka mbeya nzima itawaliwe na wabunge wa chadema tu wacha ccm nao wapumzike
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom