Mbunge Sugu aelezea kukamatwa kwake na kinachoendelea Mbeya Mjini hivi sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge Sugu aelezea kukamatwa kwake na kinachoendelea Mbeya Mjini hivi sasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paparazi Muwazi, Jul 9, 2011.

 1. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2011
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu aka Mr II ametutumia taarifa hii kuhusu kukamatwa kwake jana na yanayoendelea Mbeya Mjini leo


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  Jana tarehe 8 Julai 2011 Polisi walinikamata kwa kile walichokiita kuwa ni kufanya mkutano bila kibali. Hata hivyo, mtiririko wa matukio unaonyesha kwamba polisi walisukumwa na sababu nyingine kwa kuwa suala la taarifa kupelekwa polisi kama sheria zinavyohitaji lilishashughulikiwa na viongozi wa CHADEMA mkoa na wilaya ya Mbeya Mjini.

  Leo tarehe 9 Julai 2011 pamoja na kutolewa kwa dhamana polisi wameonyesha nia ya kutaka kuzuia tamasha la wazi la bure ( ‘Burudani Nyumbani') ambalo wasanii mbalimbali walikuwa walifanye kwa mwito wangu kwa ajili ya kutoa burudani na kuhamasisha maendeleo. Polisi wameonyesha vitendo vya kutaka leo kufanyike tamasha la fiesta pekee wakati ambapo matamasha haya yote mawili yameandaliwa na wadau tofauti katika maeneo tofauti.

  Mpaka wakati huu ninapotoa taarifa hii wananchi wengi wamejikusanya katika uwanja wa Ruanda Nzovwe ambao ni maarufu kama Uwanja wa Dr Slaa wakisubiri tamasha hilo lakini polisi wameonyesha dhamira ya kutaka kuwatawanya.

  Maneno na vitendo vya Jeshi la Polisi vinaelekea kuwa na uhusiano na kauli ambayo niliitoa hivi karibuni kupitia mtandao wa Facebook ya kutohitaji tamasha la Fiesta kufanyika Mbeya.Katika mazingira haya ni muhimu nikaeleza tu kuwa kauli yangu kuhusu Fiesta ilikuwa na madhumuni ya kuanzisha mjadala kuhusiana na suala zima la wizi na unyonyaji uliopo kwenye Sanaa, ambao sio tu unawanyima haki Wasanii, bali pia kukosesha mapato kwa Serikali ambayo yangetokana na kodi kupitia Sanaa ikiwemo muziki.

  Nilifanya hivyo baada ya tamasha hilo kutangazwa kufanyika katika eneo ambalo wananchi wamenipa wajibu wa uongozi wa kuwatumikia na kuwawakilisha. Hivyo kwa niaba ya wananchi wa Mbeya Mjini wanaokosa mapato katika sanaa na wasanii wa Mbeya wanaokosa fursa kutokana na vikwazo nilichukua uamuzi wa kuwakilisha kupaza sauti kama ambavyo nimekuwa nikipaza sauti katika masuala mengine yanayogusa umma kama viwanda, kilimo, barabara za Mbeya Mjini na Haki za wanafunzi wa Elimu ya Juu pamoja na makundi mengine katika jamii.

  Niliamua kupaza sauti katika hili kupitia Fiesta, kwa kuwa waandaji wake kimsingi ni sehemu ya vyanzo vya maovu kwenye maendeleo ya muziki hapa nchini. Fiesta ikiwa kitovu cha uonezi kwani hata Wasanii wanaoshiriki halipwi ipasavyo au hawalipwi kabisa. Na hii ni kutokana na wao kutumia njia haramu kuhodhi (monopolise) biashara ya muziki hapa nchini, huku wakiwanyima nafasi watanzania wengi kutumia vipaji na ubunifu wao kwenye biashara ya muziki.Waandaji wa Fiesta ndio wenye redio ya Clouds, Kampuni ya promotion ya Primetime, na pia wanahusika na N.G.O ya THT, waandaji wa matamasha ya injili, ikiwemo kuwa na ushirika katika Tamasha la Pasaka.Huku wakiwa na ushawishi wa hila kwenye Kili Music Awards (One Call Promotion) na mambo mengine yote muhimu yanayohusu Sanaa. Ikiwemo ujumbe wa bodi kwenye Tamasha la majahazi, Zanzibar. Lisingekuwa jambo baya kama wangetumia nafasi hizo kwa haki na maendeleo ya sanaa.

  Kutokana na haya, kwa miaka mingi himaya ("empire") hii imetumia nafasi yake dhalimu kukandamiza watu wengine hasa Wasanii. Kwa mfano kama Msanii hayupo kwenye hiyo "himaya" yao basi hana nafasi ya kutimiza ndoto yake. Na iwapo Msanii hakubaliani na taratibu zao au malipo finyu wanayowalipa Wasanii, basi watahakikisha wanampiga vita na hatimaye kuhujumu usanii wake ili atoweke, kwa kuwa tu hakubaliani nao. Msanii hana haki ya kufanya majadiliano ya kibiashara mbele yao. "Empire" hii imehodhi mpaka makampuni ya udhamini hapa nchini, ambapo makampuni haya yamekuwa magumu kutoa udhamini kwa wadau wengine kwa kuwa tu wao ni washirika wa "Empire" hii.

  Walifikia hatua ya kuhodhi mpaka biashara ya usambazaji kwa "Wadosi" ambapo bila ya wao kuruhusu basi Msanii yeyote kazi yake haipewi nafasi ya kusambazwa wala kusikika. Hata kama nyimbo au album yake ni nzuri kwa kiasi gani.Kibaya zaidi wamehodhi mpaka nia njema ya Rais Kikwete katika kusaidia Sanaa na Wasanii. Mfano ni Studio ambayo Rais kupitia Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano alitangaza kuwa amewapa Wasanii wa Tanzania, lakini baadaye tukashangaa kusikia ipo mkononi! Pia Rais aliahidi na kutoa nyumba ya Serikali kwa Wasanii ambayo ingetumika kuendeshea Studio husika, lakini nyumba hiyo ya Serikali iliyotolewa na Rais sasa iko chini yao na ndio makao ya THT! Wamefanikiwa kumhadaa Rais kuwa wao ndio "Care takers" wa Sanaa ya Tanzania akawaamini na wao wanaitumia vibaya imani njema ya Rais kwao kufanya dhuluma.

  Yote niliyoyataja juu, japokuwa hayo ni kwa uchache tu! Yanalalamikiwa sana na wasanii wengi na wadau hapa nchini, japokuwa wengi wameshindwa kujitokeza waziwazi kutoka na vitisho vya watu hawa. Vitendo hivyo wanavyofanya vimeleta madhara katika tasnia ya sanaa na matokeo yake ni kudumaa kwa maendeleo ya muziki hapa nchini. Vijana wengi wanaojihusisha na sanaa wamepoteza matumaini. Wengi walipata tegemeo la ajira kupitia muziki, lakini hali haipo hivyo tena. Vijana wengi wasanii wamekata tamaa kwa ajili ya ukandamizaji wa "empire" hii.

  Na sio tu wasanii na wadau wengine wanawapoteza katika hili. Kwa watu hawa kuhodhi na kuvuruga kabisa biashara ya muziki, hata Serikali inapoteza fedha nyingi kupitia kodi. Kwa mujibu wa utafiti wa Dr. Jehovaness Aikaeli ambaye ni mchumi wa UDSM, hata katika hali hii mbaya ya biashara ya muziki, Serikali imepoteza Tsh. Milioni 18, kwa kutokusanya kodi kupitia muziki tu, ukiachilia mbali filamu na sanaa nyingine. Na iwapo hali itaboreshwa basi kodi hiyo itapanda mpaka wastani wa Tshs. Bilioni 50 kwa mwaka! Hizi sio pesa kidogo kwaserikali, hasa ukizingatia bajeti ya Wizara inayohusika na Utamadnuni ni Tsh bilioni 14, kwa mwaka, fedha ambazo mara nyingi hawapewi zote kutokana na Serikali kutokuwa na fedha ya kutosha! Lakini hapa utaona kukwa kodi ya mwaka peke yake ingetosha kwa bajeti ya Wizara na ziada kubwa ingebaki kwa miradi ya maendeleo kama kujenga Art Theatres n.k

  Napenda ieleweke wazi kwamba mimi binafsi ni "Mhanga" au "victim" wa uharamia wa "himaya" hii kwa miaka mingi, tukupitia migogoro kadhaa ya kibiashara lakini kilichonisikuma kuchukua hatua hii; sio nafsi yangu pekee bali wajibu nilionao hivi sasa kama mwakilishi umma.Izingatiwe kuwa baada ya mimi kuchaguliwa kuwa Mbunge na wananchi wa Mbeya tena kwa kishindo, Serikali kupitia Wizara inayohusika na utamaduni na pia Baraza la Sanaa (BASATA), walinipongeza kwa barua huku wakinitaka niendelee na harakati za kupigania sanaa na wasanii kwa kutumia nafsi au jukwaa langu jipya Bungeni na nje ya Bunge. Jukumu ambalo nililikubali kwa mikono miwili kwani harakati za muziki huu si kitu kipya kwangu, ulianza kabla ya Ubunge na ndio ninachokifanya na hasa ukizingatia mimi pia sasa ni Waziri Kivuli (Shadow Minister) wa Wizara ya Habari, Vijana na Michezo.

  Kwa lugha nyingine ujumbe nilioutoa wa kukataa Fiesta ni ishara ya mgomo wenye nia ya kutuma ujumbe wa madai ya msingi. Na historia inaonyesha kuwa, Wasanii wa Nigeria walianza kulipwa vizuri kama wanavyolipwa sasa baada ya kuanzisha migomo dhidi ya mapromota wanyonyaji wa nchini kwao.Na kama ni suala la kukuza uchumi na ajira, Ni nini mchango wa Fiesta na matamasha mengine kwa halmashauri za mji na majiji wanayopita na kuvuna mamilioni ya fedha kila siku?

  Wenu katika kutaka haki,

  Joseph Mbilinyi (Mb)
  9/7/2011-Mbeya Mjini
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hii ni kama alivyoandika mwenyewe Sugu au umeifanyia editing kidogo?

  Na huyu Mdosi ni nani kwa muktadha uliotumiwa na Bwana Sugu? Middle man? Wakala?
  Na hilo neno linapatikana kwenye kamusi yoyote au ni msamiati mpya?
   
 3. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Duh mkuu hii habari nzuri umeifanya kuwa ngumu kusomeka..,kwa manufaa ya wengine please weka paragraphs na kuongeza font kidogo; Natanguliza shukrani...
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mtu kama sio msanii, au kama si mpenzi kabisa wa sanaa hasa ya music unaweza ukamshangaa Mr sUGU.
  Lakini deep inside this article anabeba ujumbe mzito sana kwa future ya sanaa ya hawa dot.com
  Kwa namna yoyote wanahitaji kumsupport, japokuwa kama alivyoeleza Sugu, wanajiingiza kwenye vicious cycle ya matatizo, maana mfumo wote katika music-industry umeshahodhiwa na "EMPIRE"!
   
 5. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  hii imetulia hao kupe wametuulia muziki na wanamuziki wetu kuna vichwa vimepigwa chini wanagusikilizisha watu wao ambao pia talent yao ni very low
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Juu ya hivyo, hii ya herufi kubwa baada ya comma ndo naiona kwake!
   
 7. h

  hoyce JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kumbe Sugu si mhuni kama wengi hapa wanavyopenda aonekane. Ana hoja. Clouds wahuni kweli kweli, nashangaa rais kwa nini anawakumbatia...au kwa sababu walisaidia kampeni?
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Mbunge wa Mbeya Mjini, (Chadema), Joseph Mbilinyi, maarufu Mr. II Sugu

  Matukio ya Jeshi la Polisi kuwakamata Wabunge wa upinzani yameendelea, baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini, (Chadema), Joseph Mbilinyi, maarufu Mr. II Sugu, kukamatwa jana.
  Sugu alikamatwa na jeshi hilo mkoa wa Mbeya pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema) Mbeya Mjini, John Mwambigija, maarufu Mzee wa Upako na wanachama wengine watatu kwa tuhuma za kufanya mkutano wa hadhara bila ya kuwa na kibali.Sugu na wanachama hao wa Chadema walikamatwa jana majira ya saa 10:30 jioni, wakati akiendelea na mkutano wa hadhara katika eneo la Nzovwe, jijini Mbeya.

  Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Mbeya, Eddo Mwamalala Makata, alisema wakati Sugu akiwa jukwaani akiendelea na mkutano wake, majira ya saa 10:20 jioni alifuatwa na Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wapatao saba waliokuwa ndani ya gari aina ya Defender, huku wakiwa wameongozana na baadhi ya makachero.
  Alisema Sugu alikatisha hotuba yake baada ya kufuatwa na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mbeya Mjini ambaye alimpa dakika 10 za kufunga mkutano na alipofunga mkutano alikamatwa pamoja na wanachama wengine wanne wakapelekwa katika Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi, kwa ajili ya kuchukuliwa maelezo. Akizungumzia kukamatwa kwa Mbunge huyo, Mwamalala, alisema mkutano huo ulifuata utaratibu zote na kwamba inawezekana kilichofanyika ni kuzuia demokrasia ya uhuru wa Mbunge huyo wa kuzungumza na wananchi.

  “Tuna wasiwasi na kukamatwa kwake kuwa si suala la kibali, tunaamini kuwa lipo jambo lingine ambalo Jeshi la Polisi linajua…wangesubiri amalize kufanya mkutano kisha wakamchukua na kumuweka ndani,” alisema Mwamalala. Akizungumza na NIPASHE huku akiwa chini ya ulinzi, Mwambigija, alisema kabla ya kufanyika kwa mkutano huo, waliomba kibali jana yake na siku ya mkutano yeye mwenyewe alikwenda polisi kuthibitisha kama jeshi hilo linazo taarifa za mkutano na akahakikishiwa kuwa hakuna pingamizi lolote la mkutano huo. Alisema anashangazwa na polisi ambao ana amini kuwa walikuwa na taarifa juu ya mkutano huo, lakini wakawageuzia kibao na kuwakamata kwa madai kuwa hawana kibali cha mkutano huo.

  NIPASHE lilipowasiliana na Kamanda Nyombi, alithibitisha tukio hilo, lakini alisema atalitolea maelezo baadaye atakapokuwa amelifuatilia kwa kina.
  Hata hivyo, ilipofika saa 1:34 jana usiku, Sugu na wenzake walihamishiwa katika Kituo Cha Polisi cha Kati ambacho kilikuwa kinalindwa na polisi wenye silaha, ambao hawakutaka mtu yeyote asogelee. Kukamatwa kwa Sugu ni mwendelezo wa kukamatwa kwa Wabunge wa upinzani mwaka huu kwa tuhuma mbalimbali.

  Januari 5, mwaka huu, Mbunge wa Hai (Chadema), Freeman Mbowe; Mbunge wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo; Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini na Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, walikamatwa mjini Arusha wakati wa maandamano ya Chadema ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha.
  Mwezi uliopita, Mbowe, alikamatwa tena jijini Dar es Salaam na kupelekwa Arusha, baada ya kuruka dhamana ya kesi ya kuandamana bila kibali jijini Arusha Januari, mwaka huu.

  Naye Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, alikamatwa mkoani Singida kwa tuhuma za kupitisha muda wa mkutano.
  Mbunge wa Meatu (Chadema) Meshack Opulukwa, alikamatwa Mei, mwaka huu na Polisi jimboni kwake na kupelekwa mjini Shinyanga na kufunguliwa mashitaka ya kupitiliza muda wa mkutano wakati wa ziara yake ya kuwashukuru wapigakura wake kwa kumchagua. Mei, mwaka huu, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu na Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Ester Matiko, alikamatwa wilayani Tarime, mkoani Mara na kufunguliwa kesi ya uchochezi kutaka miili ya watu waliouawa na polisi katika mgodi wa North Mara ifanyiwe uchunguzi.Aidha, Juni mwaka huu, Mbunge wa Viti Maalum (CUF) Magdalena Sakaya, alikamatwa na kuwekwa mahabusu kwa wiki mbili wilayani Urambo, mkoani Tabora na kufunguliwa kesi ya uchochezi na kuwazuia polisi kufanya kazi zao.

  IPPMedia
   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  Jul 9, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Watu na fani zao!

  Jamani hamuoni ujumbe, mnaona discrepancies tu?
  My hairs!
   
 10. C

  Che-lee JF-Expert Member

  #10
  Jul 9, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ujumbe mzito sana! Heko sugu!
   
 11. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #11
  Jul 9, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ingawa haina paragraphs nime imaliza,na
  sugu naku support katika harakati zako,...

  sielewi ni kwanini mnyimwe kufanya tamasha,ila wakibana
  zaidi ingieni kwenye hilo la fiesta atakae tukana shukeni nae
   
 12. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #12
  Jul 9, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  yaani we acha tu,wasanii wengine wanakaa kimya sababu wakiongea
  ndo hivo tena itakula kwao,bora walambe wakubwa viatu tu
   
 13. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #13
  Jul 9, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Mdosi ni neno linalomaanisha muhindi kwa street language ya Tz ingawa KE inamanisha boss, kwa bongo mdosi ni neno linalotumiwa kumwita msambazaji wa muziki, wanaitwa wadosi sababu kazi ya usambazji muziki toka kitambo ilikuwa inafanywa na wahindi thats why wasambazaji wakaitwa wadosi hata wasambazaji wakubwa mamu na GMC ni wahindi a.k.a wadosi hawa ndo wanyonyaji na wezi wakubwa
   
 14. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #14
  Jul 9, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ujumbe mzito sana. Naanza kuona mwanga kwa wasanii wanaokandamizwa na "Empire" dhalimu.
  Keep on moving Sugu!!
   
 15. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #15
  Jul 9, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  huyu kaipeste hapa fasta bila kuiweka sawa....iweke habari vizur bana..........aiseee!!!!
   
 16. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #16
  Jul 9, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  pole sugu...lazima tupambane kwa wahujumu uchumi kwa gharama yeyote ile aluta...
   
 17. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #17
  Jul 9, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  nia yao ni nini hasa? wanataka watu wengi waende fiesta na sio burudani nyumbani?? au wanataka nako damu imwagike?? nchi ya kisanii kweli hii
   
 18. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #18
  Jul 9, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ningefarijika zaidi kama wasanii wooooote wanyonywaji wangesoma taarifa ya Sugu!
   
 19. t

  toxic JF-Expert Member

  #19
  Jul 9, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 773
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  JK,is not a serious guy,hvyo basi ni rahisi kuhadaika na kughilibika.reasoning ya baba riz ipo too low.Ninajisikia aibu kutambulishwa na rais wa viwango hv vya jk.
   
 20. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #20
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu kweli tunamshukuru kwa kuleta ujumbe, lakini tunamuomba kwa baadae awe anajaribu kidogo kuweka habari iwe rahisi kusomeka am sure kila mtu angekuwa anapost kama huyu ndugu ingebidi watu tuwe tunameza panadol kila baada ya kusoma post nne, sababu ya kupata headache..

  Back to the Topic..
  Nampa support Sugu kwa kuwatetea Wasanii na hakuna mtu better kuelezea mambo yanayowakwaza wasanii kama Sugu, sababu he has been there.
   
Loading...