Mbunge Shabiby aibua ufisadi wa kutisha EWURA, Waziri wa Nishati Kalemani asema walishavunja mkataba na kampuni fisadi

Kama hujui, miaka mi5 ya magufuli hajawahi tumbua ewura iliyo chini ya mbunge wa chato.

Mradi wa wakubwa huo.
Mbunge wa Gairo mh Shabiby amesema kuna kampuni inalipwa kati ya sh bilioni 5 hadi 7 kila mwezi kwa kazi ya kuweka rangi kwenye mafuta yanayotumika nchini.

Shabiby amesema fee hizo ni nyingi mno kulinganisha na kazi ndogo sana inayofanywa na kwamba kazi hiyo ingeweza kufanywa bure na TBS

Shabiby kasema kazi hiyo wamepewa kampuni binafsi ambayo inatupiga haswa.

Waziri wa nishati mh Kalemani alitoa taarifa kwamba mkataba wa kampuni hiyo ya kifisadi ulishasitishwa lakini mh Shabiby aliikataa taarifa hiyo na kusema hata jana aliiwaona watendaji wa kampuni hiyo wakiendelea na kazi hiyo ya kitapeli

Source: ITV habari

Ramadhan Kareem!
 
Huo Mkataba ulikuwa enzi za Utawala wa Kijerumani 1824! Tuendelee kuchapakazi ndugu zangu! HapaKazi tu!
 
Ndiyo anasemaje kuhusu petrol? Kuna watu humu wanaishi kwa kufuata mawazo ya vibaraka wa mabeberu - Lissu, Mbowe, et al. bila hao hawawezi kuwa na msimamo.
sasa mtu hayuko bungeni unataka aseme nn?
hamna mtu anajali mawazo yanatoka mbinguni au kuzimu. kila mtu ashinde mechi yake
 
Mimi nikiwa raisi masaa wiki tu watadunga sumu.

Kuna vitu vinatia hasira.
Siasa ni mfumo mbovu kwa nchini yetu.

MUNGU TUINULIE MZALENDO WA KWELI TOKEA POPOTE ATAKAYETUPA KATIBA MPYA.Amina
 
Ni kuweka vinasaba na sio rangi, jibu la kalemani lilinitia mashaka sana kwanini alikimbilia haraka kusema mkataba wa kampuni hiyo umesitishwa? Kwanini sasa? Je alijua kuwa kweli ulikuwa ni wa kifisadi? Hii issue haijakaa sawa pia Shabby alisema ana majina ya wabunge waliopewa rushwa na huyo agent ili EWURA wampe kandarasi Agent huyo.

Hivi sasa Chama cha Mataga ni full kuumbuana. Waziri mzima kuumbuliwa na Mbunge tena wa Chama kimoja ni hatari sana.

Naona kila dalili ya baadhi ya Wizara kutopitishiwa badgets zao. Siyo kwakuwa si rafiki kwa Wanachi la hasha. Bali ni kuonekana kwa Mawaziri wake ni Mizigo kwenye Wizara hizo. Sababu nyingine ni chuki iliyojengeka kati ya baadhi ya Mawaziri na Wabunge. Hii itawapelekea baadhi ya Wabunge kuwakomoa Mawaziri hao.
 
Duuh bongo kiboko kuchanganya rangi tuu watu wanalipwa mabilion ya kutosha na waziri anakili kuwa hao jamaa ni mafisadi vijana wapo mtaani hamtaki kuwapa ajira kisa ubinafsi na roho mbaya...
 
Kalemani ni Mbunge wa chato na Watu wa chato wanajulikana kwa upigaji wa pesa za walipa kodi? Kampuni ya nani hii yenye huu mkataba!? Usikute ni kampuni ya Jiwe? Na huu mkataba umesitishwa lini? Details ziwekwe hadharani tangu mwanzo wa mkataba hadi kusitishwa kwake.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom