Mbunge Saasisha apendekeza Serikali iweke siku maalum ya Magufuli Day

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,482
9,242
Mbunge wa Jimbo la Hai (CCM), Saasisha Mafuwe ametoa mapendekezo leo Bungeni, Dodoma akiomba Tanzania iwe na siku maalum ya kumkumbuka Hayati Dr. John Pombe Magufuli (Magufuli Day) kwa ajili ya kuyaenzi mazuri aliyoyafanya Hayati Magufuli enzi za uhai wake.

“Napendekeza kuwe na Magufuli Day ili kumuenzi JPM lakini pia hapa Dodoma kujengwe kituo Maalum cha kutunza kumbukumbu za Hayati Magufuli na kwenye mtaala wetu kwenye somo ambalo Hayati alilipendekeza la Historia ya Tanzania, kuwe na Historia ya Magufuli”
 
Kwa jinsi alivyoinua uchumi wa nchi; kwa mara ya kwanza katika historia nchi ikaigia uchumi wa kati; kwa jinsi unafuu wa maisha na uchumi wa mwananchi mmoja mmoja ulivyoboreka nchini kuna haja sasa ya kuondokana na picha za wanyama kwenye coins na bank notes zetu; tuweke picha zake.
 
Huyo ndio kiongozi wa Wananchi, watu wamekaa kusifia Mwanaume mwenzake. Eti kwenye somo la Historian kuwe na Historia ya Magufuli.
 
Kwa sauti ya Tundu Lissu. Huyu Mh. Mbunge wa hai ni mtu wa ajabu saana.

Better huyu astep aside Mwenyewe arudi ktk nafasi yake.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom