peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 12,809
- 21,411
Mbunge wa CCM Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro, Mh. Saashisha Mafue anadaiwa kuwalipa vijana walioajiriwa ajira ya muda ya Postikodi Tsh 15,000 kwa siku badala ya Tsh 30,000 kwa siku kama ilivyopangwa nss as Serikali ya Rais Samia.
Pili, Mbunge huyo anadaiwa amewaambia vijana hao kuwa ajira hiyo ni ya muda wa siku 15 badala ya siku 45 kama ilivyoainishwa na serikali ili zoezi lifanyike kwa Uangalifu na kwa umakini mkubwa.
Vijana hao wameamua kufanya kazi hiyo bila ufanisi kutokana na kulipwa malipo tofauti na mpango wa serikali, ila siku ya jumamosi tarehe 19.3.2022 wataandamana kumpokea mwenyekiti wa chadema Taifa ambaye atahutubia Jimbo la Hai mjini ikiwa ni mara ya kwanza tangu atoke gerezani na watafikisha kilio hicho mbele yake kwa mabango.
Mkuu wa Wilaya ya Hai alivyotafutwa kuzungimzia malipo hayo na siku za kufanya kazi hakutaka kusema chochote bali alisema hausiki na zoezi hilo na hakushirikishwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Hai , Dionis Myinga alivyotwafutwa ofisini kwake palikuwa pamefungwa.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai, tulivyompigia simu ,kumuuliza kuhusu stahiki ya malipo kwa hao vijana wanaofanya kazi kwa mkataba, kwa kila siku na muda wa kazi hadi kumalizika alisema yuko kwenye kikao.
Vijana hao wanakiomba Chama cha mapinduzi ngazi ya wilaya, mkoa, Taifa kuingilia kati hatima ya malipo yao na siku za kufanya kazi hiyo kama ilivyopangwa na serikali ya CCM. Vijana wamekata tamaa iliyosababishwa na mtu mmoja au kikundi cha watu.