Mbunge Peter Msigwa wa CHADEMA amsifia Rais Magufuli kwamba anajali vyama vyote

Emc2

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,808
16,834
Hakika nyota ya Rais wetu inazidi kuwakuna wapinzani. Hatimaye Peter Msigwa ameona juhudi nzuri za rais wetu na kuamua kusifu. Msigwa alimwaga sifa hizo Mei 2, 2018 mbele ya Rais Magufuli aliyejawa na tabasamu muda wote.



Msigwa: Mhe. Rais umekuwa ukisisitiza katika hotuba zako kuwa wewe hujali mambo ya vyama, na hii imedhirika kuwa kweli hujali vyama, umesaidia sana, hela za kutoka kwako zimekuja nyingi, kama alivyosema Mhe. Mahiga, kuna barabara nzuri katika kipindi chako ambacho umekuwa Rais, umejenga barabara ya lami kutoka Mlandege mpaka kwa Mkuu wa Wilaya karibu Shilingi Bilioni 3.5, tuna stendi nzuri ipo Ipogoro ya karibu Shilingi Bilioni 3, tuna maji, kwa hiyo kuna vitu vimefanyika kwa kweli Mhe. Rais hupendelei, hela zinakuja hata sisi ambao ni wa CHADEMA unaleta hela, kwa hiyo tunakupongeza sana.

Kama mchungaji Msigwa amesifu wewe ni nani uendelee kupinga juhudi hizi?
 
Nani kakwambia Msigwa ndie ana hodhi ya akili na mawazo ya kila mtu hapa?! Msigwa ni akili kubwa, kama kamsifia ni baada ya uchambuzi sisisi; sio kirahisirahisi hivi hivi, au kwa woga yule mtu ni kichwa hata JPM anajua na ndio maana alimtambua hadharani kwa jina lake kati ya wabunge wote wa mkoa wa Iringa
 
Kwani tunakataa hakuna mazuri yanayofanyika? Kwenye kupongezwa ni vema apongezwe ila pia penye kukoselewa akubali..

Hiyo hutoba haijaisha, imekatishwa.. ni dhahiri kuna vitu pia kamkosoa hapo ila hamutaviweka ndio mana clip ineishia sekunde 51..

Muungwana yeyote kabla ya kukosoa lazima akupongeze kwanza..
 
Mbona sioni alipo pongezwa hapo kutoka kwa Petter Msigwa ?..

Au kwa sababau Jina la Msemaji wa Magogoni linafanana na Mbunge Petter Msigwa ndio unataka kuchanganya Watu hapa ?

Tumuamini Msigwa huyu huyu anaesema bila ya bre....k ?
 
Hakika nyota ya Rais wetu inazidi kuwakuna wapinzani. Hatimaye Peter Msigwa ameona juhudi nzuri za rais wetu na kuamua kusifu.




Kama mchungaji Msigwa amesifu wewe ni nani uendelee kupinga juhudi hizi?



amefanya sehemu yake, kupongeza si jambo baya
 
Hakika nyota ya Rais wetu inazidi kuwakuna wapinzani. Hatimaye Peter Msigwa ameona juhudi nzuri za rais wetu na kuamua kusifu.




Kama mchungaji Msigwa amesifu wewe ni nani uendelee kupinga juhudi hizi?

Kwa hiyo Msigwa ana hati miliki ya sisi kufikiri? Akili za Lumumba wanazijuaga wenyewe!
 
Magufuli ni haki yake kupongezwa kwa kuwa kaingia eneo la mfalme mwingine na Msigwa pia ni haki yake kumpongeza kwa kuwa Magufuli ni mgeni wake.

Hii haina tofauti na kutoa pongezi kwa marehemu siku ya mazishi ambaye hata kama alikuwa jambazi,mwizi na mchawi wa aina gani siku ya mazishi yake huwezi ukasikia ikisomwa risala ya maovu yake,siku hiyo kitakachosomwa ni mambo mazuri hata kama marehemu hakuwa na mazuri siku hiyo yatatafutizwa ili ionekane marehemu naye alikuwa ni binadamu.
 
Back
Top Bottom