Mbunge Peter Lijualikali akamatwa baada ya kupost picha ya mtu aliyedai ni Afisa wa Usalama wa Taifa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Habari wakuu,

Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kuweka picha mtandaoni ikimuonyesha mtu aliyedai ni afisa usalama wa taifa hivyo akipata tatizo lolote aulizwe yeye.

Lijualikali alitiwa nguvuni mahakamani punde baada ya Kesi ya uchaguzi iliyompeleka kuahirishwa.

Leo alikuwa kwenye kesi yake mahakamani, ilipoahirishwa akakamatwa hapo hapo. Taarifa zinadai tuhuma inayomkabili ni kuhatarisha maisha ya mtu alieweka picha yake.

Lijualikali anaingia Tena korokoroni ikiwa ni siku chache tangu alipotoka ambapo alikaa kwa zaidi ya siku 23.

Stay tuned..
 
Back
Top Bottom