* AITAKA SERIKALI KUCHUKUA HATUA MAHUSUSI KUSHUGHULIKIA HALI YA AFYA YA WANANCHI GEITA
Katika mchango wake jana bungeni Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Geita kwa tiketi ya CHADEMA Mh. Upendo Peneza katoa changamoto lukuki kwa serikali kwa kushindwa kutatua matatizo katika wizara ya afya. Hii ni pamoja na kuitaka serikali kuboresha hosptali ya Mkoa wa Geita na kuwa na hadhi ya hosptali ya rufaa... Pamoja na hilo, Mbunge huyo kagusia maeneo yafuatayo.....
Uhaba wa Fedha katika wizara ya afya:. Kutokana na uhaba wa fedha iliyotolewa katika wizara hiyo, Mh. Peneza kaishauri serikali kuangalia misamaha ya kodi ili kuongeza mapato ya nchi. Na pale unapoongeza mapato ni vyema sekta muhimu kama ya afya iangaliwa zaidi, kwa lengo nzima la kuboresha afya na maisha ya wananchi..
Usawa wa Kijinsia:.. Mbunge Peneza katoa wito kwa serikali hasa wizara husika kuendelea kuhamasisha ushiriki wa pamoja baina ya mke na mme katika suala zima la kuleta maendele0. Na hii itasaidia kuchochea kasi ya maendeleo ndani ya jamii. Mh. Peneza katoa mifano ya jinsi ya wanawake ambao kwa sasa ni wabunge walivyofanikiwa baada ya kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa waume zao... Na wazazi wao...!
Vifo kwa wajawazito:.. Mheshimiwa Peneza kaishauri serikali kuchukua hatua mahususi ili kupunguza kiwango cha vifo vya wajawazito. "Vifo vingi na kwa asilimia kubwa utokana na wasichana kubeba mimba wakati wako chini ya umri halisi ya kubeba mimba. Hivyo ni wakati wa serikali kukaa pamoja na wadau wengine ili kuangalia ni jinsi gani ya kuwasaidia watoto wa namna hii... Ili kunusuru kundi hilo la wasichana na Taifa kwa ujumla
Lakini pia, kuna changamoto ya elimu kwa watoto wetu ndio maana wakati mwingine wanashindwa kwenda shule. Na hii inachangiwa kwa kiasi kikubwa pale wanapokosa sanitary towels "vifaa vya kujistili kipindi cha hedhi". Unakuta mtoto anashindwa kwenda shule kwa zaidi ya siku 4~7...
Pamoja na serikali kuweka misamaha ya kodi katika "sanitary towels" lakini bado zinapatikana kwa bei za juu, kiasi kwamba msichana wa kawaida hasa wanafunzi hawawezi kumudu. Hivyo nitoe wito kwa serikali itengeneze chombo maalum, cha kuangalia kila product inayopewa msamaha wa kodi ifike kwa walengwa kama ilivyodhamiriwa. Na hii ni pamoja na dawa....
Pia, Mh. Peneza aliiendelea kutoa wito kwa serikali hasa wizara ya afya kuangalia suala zima la ushiriki wa wanawake katika sekta ya kilimo. "Lazima tutambue kuwa asilimia 80% ya wanawake ndio nguvu kazi katika kilimo". Hii inatoa tafsiri kwamba, usipoangalia kundi hili kwa makini kilimo kitashuka.
Mbunge huo pia, kaiomba serikali kuangalia uwezekano wa kupeleka umeme wa sola katika zahanati katika Mkoa wa Geita. Pamoja na changamoto kubwa ya kutokuwepo umeme, kaiomba wizara kuangalia uwezekano huo ili kunusuru maisha ya wananchi hasa wakina mama wanaojifungua kwa tabu sana.
Mheshimiwa Mbunge huo pia kaiomba wizara ya afya kuangalia ni namna gani Mkoa wa Geita uweza kupatiwa boti ya mwendo kasi ili kunusuru wagonjwa walio katika hali mbaya na ambao wanahitaji huduma za haraka katika hosptali kubwa kama Bugando... "
Na mwisho Mh. Peneza kaiomba serikali kupanua wigo katika huduma ya CHF. Ili mwananchi wa hali ya chini apate huduma katika maeneo mbalimbali au popote pale atakapoenda na isiwe tu kwenye kata husika aliyokatia kadi yake ya CHF na vile vile, kaitaka serikali kuhakikisha kunakuwepo na dawa katika zahanati/vituo vyake vya afya. Ili kuondoa usumbufu unaojitokeza kwa wananchi wenye kadi za CHF, ambao mara kwa mara ukosa dawa.