Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,190
- 4,103
Mbunge pekee wa CHADEMA, Aida Khenan wa Jimbo la Nkasi Kaskazini ahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Dk John Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Aida Khenan ametoa msimamo mwingine kuwa hawezi kuwasaliti wananchi waliomchagua kuwawakilisha hivyo anasubiri kuapishwa aingie bungeni. Awali Mbunge huyu alitoa msimamo kwamba watakachosema viongozi wa chama chake ndicho atakachofuata.
"Chama kiliniamini kikarudisha mamlaka kwa wananchi na wananchi wamenipa mamlaka. Kama niliapa Chadema siwezi isaliti hali kadhalika siwezi wasaliti wananchi wa Nkasi Kaskazini.
Naomba nitoe msimamo wangu, mimi Aida nimechaguliwa kwa mujibu wa sheria na ni mbunge halali wa Nkasi Kaskazini, ninasubiri kuapishwa na hakuna jambo jingine, sina mabadiliko mengine".
Aidha Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema kuwa kamati kuu itakaa na kutoa msimamo wa chama wa jumla kama kuendelea na msimamo wa awali uliotolewa na viongozi wakuu wa chama au vinginevyo.
Lakini pia ameongeza kuwa kama kamati kuu ya chama ikibariki maamuzi ya viongozi wakuu wa chama basi Aida kama atabaki na msimamo wake wa kwenda bungeni itabidi atafute namna nyingine ya kuwatumikia wananchi wa Nkasi.