buswelu moja
JF-Expert Member
- Aug 24, 2014
- 226
- 147
Mbunge Ole Milya amtuhumu Rc Mnyeti kuhusu rushwa,ahoji ukaribu wake na kampuni ya Tz One , Rc Mnyeti Ajibu mapigo
Mwandishi Wetu,Mirerani
Mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, James Ole Milya amemtuhumu mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti kwamba anapokea rushwa ili kuwakandamiza wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite walioko eneo la Mirerani mkoani Manyara.
Ole Milya ametoa kauli hiyo Leo Julai 28 mwaka huu katika mji mdogo wa Mirerani mbele ya kamati ya kuchunguza na kutatua mipaka baina ya wachimbaji wadogo na kampuni ya Tanzanite One.
Hatahivyo, Ole Milya alienda mbali zaidi na kuhoji ukaribu baina ya kiongozi huyo wa serikali na kampuni hiyo huku akisema kwamba hatakubali kuona haki za wanyonge zinakandamizwa pindi akiwa madarakani.
"Nimwombe Mheshimiwa mkuu wa mkoa urafiki wake na Tanzanite One ufikie mwisho, usiliingize taifa hili kwenye migogoro isiyostahili "alisema Ole Milya
Alisisistiza kwamba kampuni hiyo inapaswa kutoa ajira kwa wachimbaji wadogo waliopo katika eneo hilo bila upendeleo na kukemea tabia inayofanywa na viongozi wa kampuni hiyo kuwabughudhi wachimbaji wadogo wasitafute riziki katika eneo hilo.
Alimtaka Rc Mnyeti kutekeleza majukumu yake kwa haki na kumkemea kwamba asiwasumbue wachimbaji wadogo kwa kuwa anapokea rushwa kutoka kwa kampuni hiyo.
Akajibu mapigo Rc Mnyeti alisema kwamba kitendo cha yeye kusimamia maslahi ya wachimbaji wadogo kama kuwa na mikataba kimemponza lakini haki itasimama pale pale.
Mnyeti alisema kwamba ataendelea kuwabana wamiliki wa migodi mbalimbali ili waweze kuwapatia mikataba ya ajira Watumishi wao kwa kuwa ndio matakwa ya kisheria.
Naye Waziri wa madini, Dotto Biteko aliwataka viongozi hao kumaliza tofauti zao kwa kuwa kazi ya wizara yake ni kuona wachimbaji wadogo nchini wanainuka kimapato ikiwa ni pamoja na kukuza mitaji yao hususani katika uchimbaji wa madini.
Mwisho