Mbunge Nyalandu ndoa na Faraja Kota

Status
Not open for further replies.

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
614
Mbunge Kijana wa Singida Kaskazini, kupitia CCM, Lazaro Nyalandu, anatarajiwa kufunga ndoa na mrembo, Faraja Kota, katika Kanisa la KKKT Azania Front na baadaye Reception, Diamond Jubilee, kwa waalikwa tu. Itatanguliwa na Sendoff, Msasani Beach Club Novemba 30
 
Mbunge Kijana wa Singida Kaskazini, kupitia CCM, Lazaro Nyalandu, anatarajiwa kufunga ndoa na mrembo, Faraja Kota, katika Kanisa la KKKT Azania Front na baadaye Reception, Diamond Jubilee, kwa waalikwa tu. Itatanguliwa na Sendoff, Msasani Beach Club Novemba 30

Naona tapeli Nyalandu ameamua kuhalarisha ndoa yake na Faraja!! Hongera sana na kwa heri kambi ya makapera.Wasi wasi wangu wataweza dumu? maana Lazaro ni kiazi sana na Faraja is a smart lady....kazi ipo!!
 
Duh! Kiazi! Simfahmu vizuri Nyalandu lakini kumuita kiazi ni 'too much' ndungu Ushirombo.

"Isekhuu Nyalandu onghoa wang'u antu viekhe unong'ona."

Kila la heri Lazaro & Faraja.
 
Duh! Kiazi! Simfahmu vizuri Nyalandu lakini kumuita kiazi ni 'too much' ndungu Ushirombo. "Isekhuu Nyalandu onghoa wang'u antu viekhe unong'ona."
Kila la heri Lazaro & Faraja.

Mh TzPride, huyo dogo ni Kiazi sana ulizia hata jamaa walio IOWA wanakubaliana na hilo....ni mjanja wa kuuza maneno, unajua alivyomuingia mama Anna Mkapa, akajiweka mbele mbele akapata mbereko ya kugombea Ubunge 2000...hata shule yake ninawasi wasi nayo sana...
 
Naona tapeli Nyalandu ameamua kuhalarisha ndoa yake na Faraja!! Hongera sana na kwa heri kambi ya makapera.Wasi wasi wangu wataweza dumu? maana Lazaro ni kiazi sana na Faraja is a smart lady....kazi ipo!!


Chagua jibu kati ya haya yafuatayo:

HAYA YAMETOLEWA NA MICHUZI SASA KAZI KWAKO MWENYE SWALI

ROMANCE MATHEMATICS

Smart man + smart woman = romance

Smart man + dumb woman = affair

Dumb man + smart woman = marriage

Dumb man + dumb woman = pregnancy
 
Duh! Kiazi! Simfahmu vizuri Nyalandu lakini kumuita kiazi ni 'too much' ndungu Ushirombo.

"Isekhuu Nyalandu onghoa wang'u antu viekhe unong'ona."

Kila la heri Lazaro & Faraja.

Hebu nigee maana yake maana nimewekwa pembeni hapo.
 
Hiyo ni nzuri, Hongera sana Nyarandu kama kweli umeamua kuoa hilo ni jambo jema hata mbele za Mungu.

Mmh Ushirombo sijui unamaanisha nini kumuita Lazaro 'Kiazi' Anyway kwa ninavyomfahu Nyarandu ni very talkative na anapenda kuwa karibu na watu wote bila kujali jins, na Nyarandu huyo huyo amewahi kuwa kiongozi wangu miaka fulani ya nyuma so ninamfahamu vizuri, tabia aliyokuwa nayo wakati ule wala haijabadilika

Kila la heri Lazaro & Faraja!
 
mimi nimeshawahi kukutana naye nilikuwa simjui,ila demu wangu akaniambia kuna jamaa mmoja anamfanyia mpango wa kwenda marekani kwa hiyo amemwambia wakutane holiday inn kuanzia saa moja jioni.
Machale yakanicheza iweje wakutane hotelini tena jioni,wakati huo huo alinisimulia juu ya rafiki yake ambaye alichukuliwa na huyo huyo lazaro wakaenda wote marekani jinsi lazaro alivyomfanyia maana hataki hata kumuona,basi nikamwambia mpigie smu mwambie tutakwenda wote ili na mimi nimfahamu, basi baada ya kupigiwa simu jamaa akachomoa hiyo miadi.
Hazi kupita siku nikakutana naye kipepeo anakademu kengine kadogo sana na mimi nipo na huyo demu wangu basi hakanitambulisha kwa lazaro kumbe ni mtu ambaye tunafaamiana maana alsoma na mdogo wangu ohoo jamaa alijisikia vibaya, lakini huo ndio ujana maji yamoto tuliowengi tumepitia huko.
tatizo ni pale unapokuwa kiongozi ktk jamii hiyo tabia uwa haikubaliki.
nampa hongera kwa kuamua kuoa
 
mungu awajaalie harusi ya heri.

ndoa mara nyingi hubadilisha sana watu.

tumuombeeni iwe ndio njia njema ya kujenga maisha ya furaha na yalio bora kwao.

wangapi kabla ya n doa wal;ikuwa ni watu wazuri na baada ya kuoa wamekuwa viazi na wangapi walikuwa viazi baada ya kuoa wamekuwa muhogo?
 
Mbunge wa Singida kaskazini Lazaro Nyalandu (38) anafunga Pingu za maisha Jumamosi ya Novemba.30.Anamuoa Mrembo Mtoto wa wa Brigedia Kota anayeitwa Faraja (25).Aliwahi kushiriki mashindano ya Urembo Tanzania.
Lazaro Nyalandu ni Miongoni mwa Wabunge Vijana ktk Bunge la Jamhuri ya Muungano.Watu wengi haswa wale waliokuja USA na Uk katikati ya miaka ya 90 na mwanzoni mwa 2000,watamkumbuka huyu Bwana kwani alikuwa Fundi wa kuuza I-20 na kuwatafutia watu Summer Camps.Vijana wengi waliokuja Michigan kwenye Mji wa Pontiac walikuja kwa mgongo wa Lazaro,kuna Group kubwa la watu huko Winona (IA) pia ni watu wa Lazaro,Lazaro pia alisoma huko Iowa kabla ya kurudi nyumbani na kupata Ubunge.Aliupata Ubunge wa Singida kwa sababu ya kuwa karibu na Mama Mkapa ambaye nae ana Honorary Degree kutoka kwenye Chuo alichosoma Nyalandu,hakuna uhakika kama Ubunge wa Nyalandu una mahusiano yoyote na Honorary Degree ya Mama Mkapa.Hata hivyo Nyalandu ana mahusiano ya karibu na Ndugu wa Mama Mkapa waishio Iowa,Minnesota na Nebraska.

Kwa wale wanaomfahamu Lazaro wanadai kuwa ni Mlokole,aliwahi kuwa M/kiti wa Taifa wa Ukwata enzi hizo akiwa shule,Lakini pia ni fundi wa kutafuta akina mama,kwani kuna wanadada wanne kama sio watano walishaahidiwa pete ya Uchumba kutoka kwa Mh.Mbunge.Wimbi la Lazaro na rafiki zake kuamua kuoa lilianza June/2007 alipooa Ndugu yake Joel,na Weekend iliyopita Mzee Mzima Jackson Mollel alifunga Pingu za maisha huko Minneapolis,MN.

Kila la Heri Mh.Nyalandu, hiyo ni hatua kubwa ktk maisha yako.Jamaa wote toka Phoenix mpaka Seattle tunakutakia kila la Heri ktk Harusi yako.Kwa kuwa ni mdau humu tunaomba picha za Harusi yako,kama alivyofanya Said Janguo.
 
duh kama hadi wadogo zetu wanaanza kuchukua jumla jumla, nadhani na sisi wazee wengine inabidi tuanza kukusanya mahari. Hivi bado watu wanalipa mahari? Ukimpatia mtu kalaptop na tukadi kwa intaneti vinaweza kuwa sehemu ya mahari au bado ni yale yale ya Ng'ombe, Mbuzi, na kondoo na tuchenji kidogo?

Hongera.
 
nasikia huyu jamaa ana kashfa ya kuuza dada zetu huko State sasa huyu sijui atamuuza pia au vipi. tusubiri tuona hatima yao lakini namuombea Mungu aibariki ndoa yao maana jamaa amebadilika sana siku hizi
 
Naona tapeli Nyalandu ameamua kuhalarisha ndoa yake na Faraja!! Hongera sana na kwa heri kambi ya makapera.Wasi wasi wangu wataweza dumu? maana Lazaro ni kiazi sana na Faraja is a smart lady....kazi ipo!!

Ushirombo,
Kama unalolisema ni kweli basi huyu Lazaro amepata mke haswa!

Kwa taarifa yako ndoa za namna hiyo ndizo zinazodumu, yaani zenye smart woman + dumb man (au kiazi kama ulivyomuita Lazaro). Mwanamke akiwa smart kuliko mwanaume, anaitunza ndoa yake vizuri sana provided anampenda huyo mwanaume. Mwanamke smart anazijua management skills, jinsi ya kum-meneji huyo mwanaume katika aspect zote, na kuvipata vyote anavyovitaka (mwanamke) kutoka kwake huku mwanaume akijisikia kwamba yeye ndiye anayefaidi zaidi. Panakuwa na mutual happiness. Yaani hiyo ni raha kamili.
 
Why kiazi? kiazi mbona kitamu sana. Pale Mlimani TULIWAITA WATU KAMA HAI vilza au KILAZA.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom