Mbunge Nusrat Hanje afunguka kuhusu Ubunge wake

My Next Thirty Years

JF-Expert Member
May 12, 2021
539
1,000
Hili suala la wabunge wa Viti Maalum Chadema lina sarakasi nyingi, ila yaelekea ni Mdee pekee mwenye maelezo halisi. Pitia mahojiano
haya.
===
1621233462911.png

The rest sijui kilichotokea na kilichoendelea,” ndivyo anavyoeleza mbunge wa viti maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Nusrati Hanje alipoulizwa swali la mazingira gani yaliwatoa jela.

“Nilikaa gerezani tangu Julai 7, 2020 mpaka Novemba 24, 2020,” alisema Hanje alipofanya mahojiano maalumu na gazeti hili mwishoni mwa wiki jijini hapa.

Hanje, ambaye ni kati ya wabunge 19 wa viti maalumu wa Chadema akitokea Mkoa wa Singida, wiki iliyopita alitoa hoja bungeni kuhusu hali ya elimu Tanzania na nini cha kufanya.

Namna walivyotoka jela “Unajua kuna utaratibu wa kulala kuanzia saa tisa na nusu (9.30 alasiri), mkichelewa sana saa kumi mnalala. Kwa hiyo siku hiyo ilikuwa saa 12 wakaja viongozi wa magereza kwamba mpo huru.”

Hanje alisema muda huo wa saa 12 jioni walipelekwa eneo la utawala la gereza na kuelezwa kuwa, Serikali haina nia ya kuendelea na kesi na wako huru.

“Basi tukawa huru na kwa kweli hakuna ambaye anapenda kukaa kule ndani, siyo sehemu nzuri,” alisema. Hanje alisema kulingana na mwenendo wa kesi yao, walikuwa hawana kosa kwa kuwa mara ya kwanza waliachiwa Mahakama Kuu ya Dodoma baada ya mlalamikaji kukosea sheria aliyotumia kuwakamata, lakini walipofika mahakamani Singida walifunguliwa tena kesi na aliongezwa mtuhumiwa mmoja.

“Kwa utaratibu wa ile kesi tulikuwa tunaenda kuachiwa kwa sababu kesi haikuwa upande wao. ‘Incident’ (tukio) ndiyo iliyokuwa hivyo.
“Kwa wazazi na ndugu, wanafanya dua, kwa kweli na mimi nilimshukuru Mungu sasa nimeachiwa basi nikaendelea na mambo yangu.
Kuhusu ubunge.

Akizungumzia kuhusu namna alivyoteuliwa ubunge wa viti maalumu kama alikuwa amejaza fomu za kuomba kwa mujibu wa taratibu za chama na lini aliambiwa ameteuliwa ubunge alisema, “kwenye hilo nafikiri si wakati wake kulizungumza, lakini Watanzania wanapaswa wajue maombi yao yalijibiwa. Walikuwa wanatuombea kila siku tuachiwe sasa tumeachiwa.

“Serikali inaposema haina nia ya kuendelea na kesi kitu ambacho nilikuwa naomba siku zote, kwa kweli ninajisikia mwenye furaha, vingine vyote vilivyotokea huko nje kwa kweli tena sijui nini kinaendelea kutokea,” alisema Hanje.

Safari ya kugombea ubunge
Hanje akizungumzia safari yake ya kutimiza ndoto yake ya kuwa mbunge aliyokuwa nayo tangu alipokuwa mwanafunzi wa sekondari, alisema aliingiza jina lake kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kwa kuomba nafasi mbili, ubunge wa jimbo na ule wa viti maalumu.
“Nilitangaza nia ya kugombea ubunge wa Jimbo la Singida Magharibi, wakati nachukua fomu kulikuwa na shamra shamra. Sasa nilikwenda kupandisha bendera kwenye kizimba nilichoandaliwa baada ya kchukua fomu.

“Wakati napandisha bendera watu ambao mimi siwajui waliimba Mungu ibariki Chadema, kitu ambacho tulionekana tumedhalilisha wimbo wa Taifa tukakamatwa.

“Nilichukua fomu mbili za ubunge wa jimbo na ubunge wa viti maalumu. Nilijaza fomu chini ya ulinzi, niliomba nikajaza fomu nikampa mtu ambaye ninamuamini ambaye ni dereva wangu kwenye chama,” alisema Hanje.

Pia, alsiema fomu na nyaraka zote ziliwasilishwa kwenye chama na utaratibu wa chama chao hata kama mgombea hayupo, lakini fomu yake ikiwasilishwa sehemu husika, msimamizi anamuombea kura.

Hanje alisema fomu yake ilipigiwa kura huku yeye akiwa hayupo na kwenye kura za maoni alikuwa wa mwisho kati ya wagombea watatu wa Singida Magharibi, lakini Kamati Kuu ya Chadema ilimpitisha Hemedi Kulungu aliyeshinda kura za maoni.

“Lakini kwenye viti maalumu niligombea peke yangu, hakuna mtu mwingine aliyechukua fomu. Kwa hiyo fomu yangu ilipigiwa kura na kwa maelezo yao, nilipata asilimia 100 za viti maalumu Singida.

“Kwa hiyo viongozi wa mkoa wa baraza la wanawake wakaandika ripoti ya matokeo ya majimbo yote Singida maana kuna majimbo manane. Jina langu lilikuwepo. `So far process’ (mchakato ulivyokwenda) ilikuwa hivyo kwa maana yake kwamba sikugombea, niligombea na utaratibu ulikuwa hivyo,” alisema.

Hoja yake bungeni
Akizungumzia kuhusu mchango wake bungeni kwenye bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Hanje alisema kuna haja kama Taifa kufanyia mabadiliko mitalaa.

“Sasa hivi tunazungumza miaka 60 ya Uhuru, kizazi kimebadilika. Watoto wanaozaliwa leo wana namna yao ya kuelewa mambo, hata elimu unaweza kukuta miaka mitano anaongea Kiingereza kizuri kabisa.

“Kwa mfano Kenya mfumo ambao waliubadilisha tangu mwaka 1985, hasa muda wa kukaa darasani wa miaka saba (shule ya msingi), miaka minne (sekondari), miaka miwili (kidato cha tano na sita) na miaka mitatu (chuo kikuu), Wakenya waliubadilisha mwaka 1985, sisi bado tunatumia ule ule.”

Alisema kuna umuhimu mkubwa wa kubadilisha mfumo wa elimu kutokana na mabadiliko na mahitaji ya sasa ya nchi.
“Mimi kitaaluma ni mwalimu, na bahati nzuri nafundisha masomo ya arts na nimefundisha somo ambalo lina topic moja inaitwa ‘life skills’, mbinu za kimaisha na ambalo nasomesha kuanzia ‘fomu one’ (kidato cha kwanza) hadi ‘fomu three’ (kidato cha tatu), akienda kidato cha tano atasoma ‘development studies’ na ‘general studies.”

Alisema mfumo wa elimu ya Tanzania hauna ‘package’ (kifurushi) kinachomuandaa mwanafunzi kutoka kwenye maarifa na kumfanya aweze kujiongeza kwa kufanya kitu chochote kwa kukiongezea thamani na kumnufaisha.

Pia, alisema elimu yetu inakosa ‘personal development’ (elimu rika) ambacho kinamuandaa kijana aweze kufanya vitu anavyovitamani na sio kupangiwa.

“Mtoto anatakiwa ajue kuhusiana na elimu rika, changamoto gani atakutana nazo wakati anakua na namna gani ya kupambana nazo kama mtu ili badala ya kuanza kuhangaika na mimba za utotoni, kijana wa kike anatakiwa apewe mafunzo mapema,” alisema Hanje.
Alisema kijana anapaswa aelezwe kwamba, akiharibu kwenye mfumo wa maisha wa aina hii kuna changamoto hizi.

“Lakini, pia mtoto ajifunze ‘problem solving’, ajue utatuzi wa matatizo kwenye jamii, yaani hata utake pesa hakuna mtu atakuita akupe pesa, utatakiwa utatue tatizo la mtu ili akupatie pesa,” alisema Hanje.

Pia, alisema kwenye utatuzi wa matatizo nako kunahitaji kufikiria kwa kina (critical thinking), kujua namna ya kuchanganua mambo, lakini vitabu vilivyopo sasa vinamfanya mtoto asome ili aende kujibu mtihani.
 

Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,739
2,000
Amesema mwenyewe kwenye hilo hana la kuzungumza, maana yake hao wote 19 ni wahujumu uchumi kule bungeni.
Uko sawa mkuu, hana la kusema maanake nini??
Wote wanaibia watanzania kodi zao waziwazi huku muhimili na mihimili mingine ikipotezea.
Ridiculous! Angekaa kimya tuu!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 

Nyambi Sr

JF-Expert Member
Apr 17, 2021
538
1,000
H
... inaelekea roho inamsuta sana Nusrat kwa jinsi alivyopatiwa hiyo nafasi. Kama katika wale Covid-19 kuna wa kusamehewa na Chama basi ni huyu; nobody else. Ila mzuri sana.
Hata Mimi ameukonga moyo wangu ni mrembo hasa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom