Mbunge Nicodemas Maganga: Mama anacheza peke yake, tunaenda kupigwa

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,353
14,630
Mbunge Nicodemas Maganga wakati anachangia mpango wa taifa bungeni amewaonya mawaziri kuwa waache kuwa na mipango mingi isiyotekelezeka na sasa hivi wamemwachia rais Samia acheze peke yake na kila anapotoa pasi wanakutwa wamezubaa.

Mh Maganga ametolea mfano serikali iliwahakikishia wananchi kuwa vijiji vyote 2000 vilivyobaki vingekuwa vimepata umeme wa REA mpaka mwisho wa mwaka 2021 lakini mpaka sasa hakuna kinachofanyika zaidi ya kushuhudia makandarasi wa kichina wakipiga sarakasi za hapa na pale site!!.

Pia amesema tangu fedha za COVID 19 zifike majimboni hakuna kinachofanyika zaidi ya kushuhudia mabishano ya taratibu za manunuzi na kushuhudia upandaji wa bei wa kutisha wa vifaa vya ujenzi kwa sasa!.

..kila siku wanasema Mama katoa fedha kwa ajili ya mradi fulani, badala ya kusema serikali ndio imetoa fedha.

..itafika mahali wananchi wataamini mwenye msaada kwao ni raisi peke yake, na viongozi na watendaji wengine hawana maana.
 
Sasa ndege Mama ndo aliamua kuzinunua? Mama sasa hivi ana kazi kubwa ya kuondoa kwanza ukungu ulio kwenye vichwa huku anaufungua uchumi wetu.

Pili Mh. anaonekana ana jambo anataka kuongea ila mpangilio wake haujanyooka vizuri huenda ni kwasababu ya ugeni.
 
maguu ndo alieanza kuharibu mambo. kila kitu magu katoa. naona wale chawa bado wapoo.

wale wajinga wanaoishabikia ccm wanajua magu/Samia wanatoa hela mfukoni kwao. hawajui ni hela zao za kodi.
 
Sasa ndege Mama ndo aliamua kuzinunua? Mama sasa hivi ana kazi kubwa ya kuondoa kwanza ukungu ulio kwenye vichwa huku anaufungua uchumi wetu.

Pili Mh. anaonekana ana jambo anataka kuongea ila mpangilio wake haujanyooka vizuri huenda ni kwasababu ya ugeni.
Ni kweli,
Maana Chadema ndiyo waliufunga uchumi wetu.
 
Unafiki mtupu....wakati JPM ananunua ndege bila kufuata utaratibu..mlikuwa mnashangilia kama mazuzu... Nimemkumbuka 'Bwege'. ...una njaa, ndiyoo...umeshiba,ndiyoo
 
Mama Alisema Macho Yamelegea Lakini Yanaona Mbali
Pesa Zitaondoka Na Watu
 
Kila mtu kambale sasa, watu wanagombania mahindi tu sasa huku na kule...bila ukatili na Unyama hizi Pumbavu zitatusumbua na kutia hasara sana watanzania..
 
Sasa ndege Mama ndo aliamua kuzinunua? Mama sasa hivi ana kazi kubwa ya kuondoa kwanza ukungu ulio kwenye vichwa huku anaufungua uchumi wetu.

Pili Mh. anaonekana ana jambo anataka kuongea ila mpangilio wake haujanyooka vizuri huenda ni kwasababu ya ugeni.
sijakuelewa mkuu...uchumi si mlisema umepanda ? aliufunga nani na nani anaufungua ? ndege alinunua nani ? aliyenunua ndege alikosea ? wakati ananunua mama alikuwa wapi ?
 
Hawezi kukabidhiwa na kuendelea tuu bila kutafakari methodology ya mtangulizi wake maana tusisifie tuu kasi ya usambazaji, tujiulize je ilikuwa na value for money? (Lengo langu sio kuwa too much skeptical bali inabidi kujiridhisha namna bora ya moving forward).
Mjambiani tumekusikia
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom