Mbunge Nicholaus Ngassa: Mkandarasi zingatia ratiba ya utekelezaji wa mradi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,862
930
MBUNGE NICHOLAUS NGASSA: "MKANDARASI ZINGATIA RATIBA YA UTEKELEZAJI WA MRADI" - JIMBO LA IGUNGA

Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Nicholaus George Ngassa, amemtaka Mkandarasi wa Mradi wa Usambazaji wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Vijiji vya Kata za Mwamashiga, Mbutu, Isakamaliwa, Kining'inila, Mwamashimba, Mwamakona, Igurubi na Kinungu kuzingatia muda na ratiba ya utekekelezaji wa mradi kama ilivyopangwa kwenye Mkataba.

Mheshimiwa Ngassa (MB) ametoa rai kwa mkandarasi Leo tarehe 20 Februari 2023 baada ya kufanya Ziara kwenye eneo la utekekelezaji wa mradi na kuona maendeleo ya mradi.

Aidha Mheshimiwa Ngassa (MB) ameendelea kutoa shukrani kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kutoa Fedha kwa mkandarasi anaetekeleza mradi mkubwa wa Usambazaji wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Jimbo la Igunga. Mradi unatarajiwa kukamilika Mwezi Disemba 2023.

"Kazi na Maendeleo"

Imetolewa na:
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Igunga

WhatsApp Image 2023-02-20 at 16.15.57(1).jpeg

WhatsApp Image 2023-02-20 at 16.15.58(1).jpeg

WhatsApp Image 2023-02-20 at 16.15.58(2).jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom