Mbunge ni nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge ni nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Noel, Jan 25, 2010.

 1. N

  Noel Member

  #1
  Jan 25, 2010
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF


  Wakati tunaenda kuchagua wabunge ni vizuri tukijadili nani anatufaa na tunahitaji nini kutoka kwa hawa tunaowaajiri.

  Kwa mtazamo wangu mimi nafikiri Mbunge ni kama meneja wa mahali husika na hivyo anahusika moja kwa moja na kuibua mikakati ya maendeleo mahali husika.Haimlazimu mbunge wa mahali husika kuwa tajiri wa mali aidha utajiri unaotakiwa ni wa mawazo yatakayoleta tofauti.Sasa wabunge wetu wanawaza tofauti ukienda kwenye vijiji vyetu sasa hivi utakuta vumbi kibao,kila mbunge anakimbilia kulima barabara (na sio kutengeneza) muda huu wa mwishoni ili aweze kuwahadaa wananchi.Hali kama hiyo inanipa maswali mengi ya kujiuliza! Utakuta wananchi mafua kibao kisa vumbi.Kwa kiwango cha ulipuaji wa namna hiyo kunasababisha barabara kuharibika baada ya muda mfupi baadae.Barabara hata isipowekwa lami lakini ikachimbwa,kuwekwa maji na kushindiliwa vizuri inaweza kuchukua muda kuharibika na kupunguza matatizo kwa wananchi.

  Tunategemea kwenda kusikiliza wagombea ubunge wakijinadi ili wapati wakati mwingine wa kutawala.Ni lazima kuwa makini.Ni vizuri kuwahoji ni nini hasa wamechangia kuibua maendeleo katika sehemu husika.Inasikitisha sehemu kama moshi vijijini mbunge hasemi lolote kunusuru mradi mkubwa wa umwagiliaji wa lower moshi,yupo kimya akianza kuongea atakuta wengine wameshaongea na pengine wameshaeleweka.Tunataka mikataba na wabunge akiahidi kitu kiwekwe kwenye maandishi.Kwa jinsi hii ungekuta kuna kesi kibao mahakamani dhidi ya wabunge walaghai.

  Inakuwaje mbunge anashindwa hata kuwakusanya vijana kuwachochea waanzishe mikakati yao wenyewe ya kukusanya mitaji na baada ya muda wanaweza wakaanza kitu fulani au kutumia nguvu zao wenyewe labda kufyetua matofali then wakauza vizuri tu.Ipo miradi mingi tu cha kujiuliza nani akiopata ubunge anakaa karibu na wananchi? Kila mtu anakimbilia dar es salaam.

  tusipojitahidi kuwa makini nchi hii itajeuzwa ya kuongeaongea tu na vitendo never.Ubunge ni ajira na mwajiriwa lazima awajibike.
   
 2. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Noel unauliza Mbunge ni nani.........Mbunge ni yule asiyekosa majibu yafuatayo..
  • Barabara haikujengwa kutokana na bajeti ndogo iliyotengwa na serikali
  • Mradi wa maji haujakamilika kutokana na mfadhili kujitoa
  • Hospitali haina dawa lakini kuna zahanati za watu binafsi mnaweza kwenda
  • Niliwaahidi kujenga shule nimeshaongea na wizara ili waje wapime eneo
  • Hili ni jimbo langu nawashangaa wanaojipitisha pitisha
  • Baada ya uchaguzi nitamalizia miradi yote
  • Mishahara yetu ni midogo mno hailingani na hadhi yetu
  • Mwaka juzi niliwaahidi sasa naona muda umekwenda sana hautoshi kutekeleza
  • Wanaofikiri mimi ni mzee hawana hoja ni wavuta bangi
  • Mwaka huu tumepiga hatua kubwa ukilinganisha na mwaka 1975 wakati nikiwa mbunge
  • Unajua sikai sana jimboni muda mwingi niko Dar nafuatilia matatizo yenu wizarani
  • Mkinichagua rais ameniahidi kunipa uwaziri kwa hiyo itakuwa rahisi kuwasaidia
  • Mtuvumilie kasungura ni kadogo(bajeti) kila mtu anataka
  • .............
  • .............
  Ndugu Noel huyo ndiye Mbunge wa Tanzania zaidi ya huyo labda siyo kutoka Tanzania ni wa kuchonga au kufikirika.
   
Loading...