Mbuty
JF-Expert Member
- Sep 16, 2011
- 411
- 237
Habari, nimepitia topic moja na hoja ilikuwa ni juu ya mazingira ya utumishi wa Mbunge, huyu ni Mtumishi wa Umma ama ikoje? Kuna baadhi wamesema sio muajiriwa wa Serikali, hapa nahitaji kuelewa maana Serikali ndio unalipa mishahara yao kwa namna ninavyofahamu. Au mazingira ya utumishi kwa ngazi ya Ubunge ikoje, ukiachilia mazingira ya kipindi isiyozidi miaka 5 bila ya kufanya uchaguzi wa nafasi hiyo. Wenye uelewa tafadhali tusaidiane kuongeza uelewa.