Mbunge Nassari: Video imeandikwa mwaka 2008 kwa kuwa ni mwaka kifaa kilitengenezwa

Kimsingi siasa za kununua watu ni siasa za kishamba na zinatakiwa kupigwa vita kwa nguvu zote, kila chama kijenge makada wake kitumikie watu wakichague kwa ridhaa yao.

Nasari kulalamika kuwa watu wake wananunuliwa ni dalili za utoto na ushamba, tungemwona wa maana angewatimua hao walionunuliwa na kujenga vijana wapya wasafi.
 
Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Mhe. Joshua Nassari, ametolea ufafanuzi kuhusiana na date zinazoonekana kwenye Video kuwa 2008 ni mwaka ambao kifaa kilitengenezwa.

"Video imeandikwa mwaka 2008 kwa kuwa ni mwaka kifaa kilitengenezwa, wakati nafanya ile kazi niliteseka sana kufuta na mnajua kuwa mimi sio mtu wa IT.

"Mwaka 2008 yule DAS anayeonekana alikuwa ni Mwanafunzi wa Sekondari, na huyo Mkurugenzi alikuwa Mtumishi wa Kada za chini alikuwa hajapata nafasi ya sasa.

Cha msingi ni kuwauliza hii sura ni ya kwako? Sauti na Ofisi ni yako?", alisema Joshua Nassari Mbunge wa Arumeru Mashariki.

Chanzo: Mwananchi
Huyu dogo atakuwa na dhambi kubwa sana. Hata camera yangu naweza kuset tarehe, ila yeye kashindwa
 
Nassari ameshazeeka kisiasa anapaswa kustaafu awaachie damu changa, hizi hoja za hovyo hazimjengi kisiasa zaidi ya kuonekana kumbe na wao ni bure tu
 
Mwaka achananao wakane picha na sauti kuwa si zao na watuthibitishie pasinashaka kuwa si zao
 
Kwa sisi tunaotumia vitu kama hivyo ni kweli kabisa huwa kuna kaugumu kwa set hiyo date. lakini ameeleweka vizuri. si Mkuuu na Yeye alisikika siku flani kuhusu hao madiwani. Mashaka ya nini. Hii inaweza kuwa kweli kabisa. Ingekuwa uongo Polepole ungemsikia. Lakini kwenye hili yupo kimyaaaaaaaaaa ninahisi anatunga uongo (propaganda).
 
video zote zilizoko you tube zinaonesha tarehe ya vifaa vilivyotumika kurecord!!
Hii inahitaji elimu ya IT?
Jana tuliambiwa ni settings!!
C ndo kwa maana ya setting aijafanyika mzee ingefanyika ingesoma vizur we unaweza ukawa unatumia time zone sio ya east africa mana kuset itakua shida sana nadhan kwako
 
Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Mhe. Joshua Nassari, ametolea ufafanuzi kuhusiana na date zinazoonekana kwenye Video kuwa 2008 ni mwaka ambao kifaa kilitengenezwa.

"Video imeandikwa mwaka 2008 kwa kuwa ni mwaka kifaa kilitengenezwa, wakati nafanya ile kazi niliteseka sana kufuta na mnajua kuwa mimi sio mtu wa IT.

"Mwaka 2008 yule DAS anayeonekana alikuwa ni Mwanafunzi wa Sekondari, na huyo Mkurugenzi alikuwa Mtumishi wa Kada za chini alikuwa hajapata nafasi ya sasa.

Cha msingi ni kuwauliza hii sura ni ya kwako? Sauti na Ofisi ni yako?", alisema Joshua Nassari Mbunge wa Arumeru Mashariki.

Chanzo: Mwananchi
Uovu unamwisho.Waovu wataadhibiwa hapa duniani mbele ya macho yetu.
 
Huko Ghana kuna sinto fahamu baada ya Ma judge kadhaa kubambwa wakipokea rushwa. Kama hii issue ya madiwani ni kweli basi CCM ni chama hatari kwa mustakabali wa taifa. Mimi ni mwana CCM lakini sipendi rushwa
 
hahahahahhahhahahahahah! who are you fooling????. Yani huyu mbunge anafikiri Watanzania hatujaenda shule, lol. Huyu jamaa akatumikie wananchi wake bana aache kutuletea uongo. Mambo megine unajiumbua tu jinsi gani na wewe ulivyo mbumbumbu. Dah! disapponted kwakweli
 
Ni vizuri kuset hiyo device yako ili watu wasipate mwanya wa ku-question kazi nzuri uliyofanya Mh Nassari. Unaweza pia kuweka off sehemu ya kuonyesha tarehe na muda. Otherwise, tunakushukuru kwa kuonyesha kuwa kuna watu wanafanya biashara ya kuwanunua madiwani kwa kutumia nyadhifa walizonazo. They don't even care how the tax-payers money will be used in the by-elections. Inauma sana
alipata shida sana wakati anafanya hiyo kazi na si mnajua yeye sio mtu wa IT kwa hiyo alishindwa kumtafuta mtu wa IT au
 
Mwaka achananao wakane picha na sauti kuwa si zao na watuthibitishie pasinashaka kuwa si zao
Mwenye jukumu la kuthibitisha au hizo sauti ni nani? La picha sio tatizo sana, mi nadhani cha kuthibitishwa hapo ni sauti na picha zinaoana? Binafsi kuna mahali pana nichanganya, lugha ya mwili na ya sauti hazikuwa zinaoana, kwa mtazamo wangu.
 
Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Mhe. Joshua Nassari, ametolea ufafanuzi kuhusiana na date zinazoonekana kwenye Video kuwa 2008 ni mwaka ambao kifaa kilitengenezwa.

"Video imeandikwa mwaka 2008 kwa kuwa ni mwaka kifaa kilitengenezwa, wakati nafanya ile kazi niliteseka sana kufuta na mnajua kuwa mimi sio mtu wa IT.

"Mwaka 2008 yule DAS anayeonekana alikuwa ni Mwanafunzi wa Sekondari, na huyo Mkurugenzi alikuwa Mtumishi wa Kada za chini alikuwa hajapata nafasi ya sasa.

Cha msingi ni kuwauliza hii sura ni ya kwako? Sauti na Ofisi ni yako?", alisema Joshua Nassari Mbunge wa Arumeru Mashariki.

Chanzo: Mwananchi
Bila shaka ni setting tu ndo ilikosewa,kwan mbona hata sim zetu za smart tunazotumia huwa hatuset time au calendar lakin sim inapiga kazi km kawa tu. Muhimu hapo kile kikicholengwa si mwaka wala saa.

Bila shaka mambo yako sawa tu
 
Back
Top Bottom