Mbunge na Mwanamuziki, MwanaFA apinga sheria mpya ya BASATA ya kutaka kusikiliza nyimbo kabla ya Msanii kuipeleka redioni. Asema ni ya ‘kidwanzi’

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,402
Mbunge wa Muheza, Hamis Mwinjuma ambaye pia ni mwanamuziki maarufu wa Bongofleva ‘MwanaFA’ ameipinga vikali sheria mpya iliyowekwa na BASATA. Sheria hiyo inamtaka msanii kupeleka kwanza nyimbo BASATA ikasikilizwe kabla ya kuipeleka kupigwa redioni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika:


“Naomba niandike kuhusu hili la huu utaratibu mpya wa BASATA. Binafsi sikubaliani nalo na ntalipinga kwa nguvu nyingi. Sidhani kama Sheria hii inafaa hata kuwepo achia mbali kutumika. HAINA TIJA YEYOTE, HAIMSAIDII MSANII KWA NAMNA YEYOTE. Ni ya kidwanzi. Inatakiwa kurekebishwa kama sio kuondolewa kabisa.

Tutafute namna nyingine za ku’censor sanaa matusi yasisikike kwa kadri inavyowezekana na sio kwa utaratibu huu dhaifu na wa kikandamizaji. Siungi mkono nyimbo “chafu” lakini kutengeneza urasimu usio na msingi kwa kisingizio cha kuwepo kwa nyimbo zisizofaa ni jaribio la kuzorotesha tu sanaa.

Kama BASATA na COSOTA wanataka kutekeleza KILA Sheria inayowahusu wangeanza na Sheria namba 7 ya mwaka 1999 inayowapa Cosota haki ya kutoa leseni kwa maeneo ya hadhara yanayotumia kazi za sanaa, kukusanya MIRABAHA toka maeneo/leseni hizo na kuwalipa wasanii makusanyo hayo.

HIZI NDIO SHERIA ZITAKAZOMSAIDIA MSANII NA WAMEZIFUMBIA MACHO KWA MIAKA MINGI, wasanii wanaendelea kupoteza hela zao NYINGI stahiki na mnawaletea sheria zisizo na kichwa wala miguu kuja kuwakandamiza. BASATA kama mlezi wa wasanii lilitakiwa kusimama kidete mpaka hili la MIRABAHA lifanikiwe.

Bahati nzuri tuna Waziri na Katibu Mkuu wasikivu, tutalisemea kwa namna nyingi hili na tunaamini kero hii itaondolewa haraka.

Msifanye kutoa wimbo iwe kama kuomba passport au VIZA, mnaonea wasanii,tunakwamisha sanaa.

Kwa heshima nyingi nawaambia Basata, mambo ya namna hii ndio haswa yanayotupa kazi kubwa kuwaelezea wapenzi wa kawaida wa sanaa kuwa Baraza hili lina kazi nyingine zaidi ya kufungia na kufungulia tu nyimbo na wasanii.

Na kuweka kumbukumbu sawa, jambo liliwahi kuja kwa majadiliano kwenye Bodi ya Basata wakati nikiwa nahudumu kama MJUMBE wa Bodi,NA NILILIPINGA SANA kwa wakati ule kama nnavyoendelea kulipinga sasa.

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”
 
Wanataka kuleta mambo ya Mwaka 47aa ya Radio Tanzania Dar es Salaam, Pugu Road!
 
Mbona kuna nyimbo nyingi kwa mfano za WCB zimejaa matusi na huwezi kusikiliza hata na Mzazi ama mtoto wako na hawajazifungia.
 
huyu si CCM? matusi wanayaona kwenye hiphop tu wakiimba siasa. ila kina daimond wanaimba upuuzi huwa hawaoni
 
Haya mambo yapo Tanzania tu mamaqe. Hivi aliyeturoga nani? Kabisaaaa eti ukitoa wimbo peleka BASATA!! Hahahahah mbona tumerudi kwenye Ujima na Ujamaa.
 
Hivi hao BASATA tofauti na mambo kufuatilia nyimbo za wasanii kama kuna matusi au laa ni majukumu yapi mengine kisheria wanayopaswa kutekeleza?
Mkuu kweli kabisa..hawa jamaa kwa jina lao tu la Baraza la Sanaa walipaswa wawe na shuguli nyingi za kuipeleka mbele Sanaa..lakini wao wamejibanza hapohapo kwenye bongo fleva..
Pumbafff kabisa.
 
huyu si CCM? matusi wanayaona kwenye hiphop tu wakiimba siasa. ila kina daimond wanaimba upuuzi huwa hawaoni
Hizo ndio nyimbo zilitakiwa baadhi ya maneno wayatoe sababu ni matusi ya wazi hizi naunga mkono hazitakiwi kupigwa radioni. Mimi nadhani waachie tu ikitokea mtu kaimba matusi basi nikuzi ban katika radio na Tv na wananchi wataunga mkono sababu ni matusi kila mtu kasikia na atasema kweli hizi hazistahili. Na wana nyimbo zaidi ya moja na sio WCB hasa katika haya makundi mawili WCB na Konde japo WCB wamezidi kidogo matusi ya wazi kabisa.
 
Back
Top Bottom