TANZIA Mbunge na Mkurugenzi wa Fedha wa zamani, Khadija Makontena afariki dunia

wanzagitalewa

Senior Member
Jan 25, 2018
128
84
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Samia Suluhu Hassan amemtumia salaam za pole Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF ) Profesa Ibrahim Lipumba, familia, ndugu na jamaa kufuatia kifo cha Mbunge wa zamani wa Chama Cha Wananchi (CUF) na Mkurugenzi wa Fedha na Mipango Bi Khadija Makontena kilichotokea Alhamisi 14 Julai, 2022.

“Bi Khadija tokea kuanzishwa mfumo wa Vyama Vingi vya siasa amekuwa akishiriki kikamilifu katika uwanja wa siasa za ndani na nje ya chama chake huku akiamini siasa za umoja na maelewano.” Ndugu Samia Suluhu Hassan.

Makontena.jpg

Bi. Khadija Salum (Makontena) enzi za uhai wake
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom