Mbunge na Meya wa Moshi Mjini, wanyimwa kuingia Ikulu ndogo kuonana na Rais Magufuli

Kisu Cha Ngariba

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
22,137
48,808
Mbunge wa Moshi Mjini Jaffar Michael na Meya wa Moshi wazuiwa kuingia Ikulu ndogo kuonana na Rais Magufuli kwa madai hawakuwa na mwaliko-
C-t0WEOWAAA8vZq.jpg


=======

Andika ndugu Japhary Michael Mbunge wa Mbunge Moshi Mjini

Kwa masikitiko makubwa napenda kuwaarifu kwamba siku ya Jumapili tarehe 30/04/2017, Mimi Mbunge wa Moshi mjini pamoja na Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi tumetimuliwa na watu wa usalama tukiwa kwenye foleni kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha Mh Rais na Viongozi wa Dini katika Ikulu ndogo ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro.

Mstahiki Meya aliniarifu kwamba tumepata mwaliko kutoka ofisi ya Mkoa kupitia kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi ili kushiriki katika Kikao ambacho Mh Rais alikuwa anaongea na viongozi wa Dini wa Mkoa Kilimanjaro.

Kwa heshima kubwa Kwa Mh Rais wetu hususani anapokutana na viongozi wetu wa Imani na ukizingatia kwamba mh Rais yupo katika eneo letu la uwakilishi nikaona ni busara niitikie wito wa kikao cha Mkuu wetu wa Kaya.

Mnamo saa sita na Nusu nilikuwa nimeshafika kwenye Geti la Ikulu ndogo nikamkuta Mstahiki Meya alishatangulia na tayari yupo kwenye foleni.

Na Mimi nikaruhusiwa kuingia kwenye foleni kuelekea kwenye eneo la ukaguzi .
Jambo la kusikitisha wakati nipo kwenye foleni pamoja na viongozi wa Dini,viongozi wa CCM wa ngazi mbalimbali na watendaji wengine wa serikali nikachomolewa mimi na Mstahiki Meya tukaambiwa hatukustahili kushiriki kwenye kikao kile.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi akajaribu kutoa utetezi kwamba yeye ndio ametupa mwaliko kwa Maelekezo ya Katibu Tawala wa Mkoa lakini hakusikilizwa kabisa.

Hatimaye tukaamriwa kuondoka katika eneo la ikulu ndogo tukaendelee na shughuli zetu.

Mimi Mbunge wa Moshi mjini sijaumizwa kwakuwa nimetimuliwa bali ninasikitika kwakuwa tunatiwa woga wa kushirki shughuli za viongozi wetu wa Kitaifa haswa wanapofanya ziara katika maeneo tunayoyawakilisha.

Huenda tutakapoacha kushiriki katika ziara za viongozi wetu wa kitaifa jamii itatujengea taswira mbaya kwamba hatuheshimu viongozi wetu wa nchi ambapo sisi hatuna nia hiyo ya kuonyesha utovu wa nidhamu kwa viongozi wetu wa nchi.
Aidha ndugu zangu kwakuwa kikao kile kilikuwa kikao cha viongozi wa Dini wala mimi nisingesikitika kutimuliwa bali kilichonikwaza ni kwavile viongozi wa CCM, Wakuu wa Wilaya, wakurugenzi na baadhi ya watendaji wengine walikuwepo na kubwa zaidi nilipata mualiko kupitia kwa Mkurugenzi wangu,

hivyo kutimuliwa kwangu nimeonekana kama mvamizi wa kikao cha Mh Rais.
Mimi binafsi nimetafsiri tukio hilo lililonipata kama Ubaguzi wa kiitikadi kwa mambo ambayo ni ya kitaifa yenye sura ya kiserikali.
 
Back
Top Bottom