Mbunge na madiwani wa kariakoo tunamba ufafanuzi kuhusu hili

Speculator

Member
Mar 30, 2012
56
4
Wafanyabiashara wa kariakoo walio wengi wanatumia usafiri wa makontena kwa mizigo yao, nadhani ni sahihi kwa magari makubwa ya kontena kuzuiliwa kuingia katikati ya jiji sababu ya msongamano mabarabarani wakati wa mchana, wakapewa muda wa kushusha mizigo uwe usiku wakati ambao hakuna msongamano kabisa au kulipia ushuru(gharama za ziada) manispaa ili aweze kuruhusiwa kushusha mchana.(Tatizo letu ni usiku tu)
Swali letu na hasa chakushangaza tunaposhusha mizigo usiku bado watu wanajitokeza wa kila aina (manispaa,mgambo, polisi,TRA n.k) vitisho kibao ? Hamruhusi ? ni makosa ? kulipiswa faini ?
Je ni wakati gani muafaka na halali wa kushusha mizigo ya biashara ?
Je ushuru tunaopaswa kulipa ni kwa ajili gani ? usiku au mchana ?
Je ni kweli kuwa hakuna haki nchi hii kwa wafanyabiashara ? kwanini munawatoza mikodi kibao ?
Tukizingatia kuwa hizo ndizo shughuli za kiuchumi zinazowezesha serikali na wanachi wake kwani tunalipa kodi zote za TRA, Manispaa,n.k Halali kabisa toka huko nje hatupati shida hadi nyumba ndio taabu nyingi sana , rushwa nyingi , kila mtu mkubwa..
 
kuwa positive siku zingine sio lazima ukae negative.

sheria ya kodi haitaji ulipaji wa kodi unatokana na mda unaofanya kazi bila kipato unachokipata katika biashara yako hivyo hoja ya usiku au mchana haina mashiko.
Pia kama ni mfanyabiashara kuna vyama vya wafanyabiashara ndo sehemu ya kuweka kero hizi hadharani,chagua kiongozi atakayesaidia kutatua kero zako.
TZ ina aina zaidi ya 30 za kodi inategemea na aina ya biashara na aina ya kipato unachopata.
 
inatia moyo kuona kuwa wafanya biashara wa wk koo wako ghadi JF ..ker9o yenu lazima itawafikia walengwa
 
Back
Top Bottom