Chona
JF-Expert Member
- Mar 8, 2010
- 523
- 360
Ndakilawe Lissu alisimamia haki, aliwaeleza wabunge haoni sababu ya wananchi wake kuchangishwa pesa za ujenzi wa madarasa iwapo kila mwaka hela iliyotengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo inarudishwa hazina kana kwamba kazi za kufanya hazipo. Huo ni uzembe mkubwa na hakuna sababu ya kuwaongezea wananchi mzigo wakati hela inarudishwa na kuliwa na wachache. Ipelekwe kwa wananchi ijenge shule, zahanati barabara na kununua madawa, madawati na kadhalika.
Mbunge makini huwajali watu wake na si kuwabebesha mizigo watu wake wakati kuna njia ya kuwapunguzia mizigo.
Hakuna michango isiyo na ulazima iwapo kila mmoja atatimiza wajibu wake ipasavyo. Unadhani serikali inashindwa kujenga shule? Lakini pia hali ni mbaya zaidi kwa yale majimbo tiifu kwa CCM. Watu wakiamua kukuletea picha za shule, zahanati, barabara na jinsi wananchi wanavyopata shida utashangaa kama hii ni tanzania ambayo wabunge wake wanaunga mkono hoja 100%. Miaka zaidi ya 50 watu mmnaunga mkono hoja!!!!!!! Lakini jambo la kujiuliza je watoto wao wanasoma katika shule hizo.
Kama umechomwa na mwiba na umevunjikia mguuni, huna sababu ya kunywa panadol ili kupunguza maumivu. Suluhisho kukabiliana na maumivu na kuutoa mwiba mguuni. Lissu anawaambia wananchi wake hakuna sababu ya kujiadhibu eti mnachangia shule wakati pesa za kufanya hivyo kila mwaka zinarudishwa hazina kana kwamba hakuna vitu vya kufanya, ni kuieleza serikali ijenge shule maana yenyewe ndo inakusanya kodi toka kwa hao wananchi. Wananchi waachwe wafikirie kuleta maendeleo yao na huku serikali ikitimiza wajibu wake. Wangechangia iwapo kweli serikali imeshindwa na haina jinsi ya kufanya hivyo. Hata wananchi hilo wamgeliona na wangejihamasisha bila kuhamasishwa.

Last edited by a moderator: