Mbunge mzalendo, maumivu yakizidi mwone | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge mzalendo, maumivu yakizidi mwone

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by babykailama, Apr 20, 2012.

 1. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  MBUNGE MZALENDO, MAUMIVU YAKIZIDI MWONE………..:embarrassed:


  Mara tatu jana Bungeni, tumesikia toka kwa Wabunge (wale dada zetu) wa CCM kuwa ama wakiwa katika ziara za Kamati au waliposoma taarifa za Kamati ama vichwa viliwauma au walipata kizunguzungu, au presha zilipanda au yote.


  Sikilizeni hayo ni maradhi. Mmekuwa mnaumwa mnatulizwa kwa vikao vya chama kama tembe (analgesic), sasa kwa vile maumivu yamezidi nendeni kwa Daktari yaani mwoneni Zitto muorodheshe saini zenu ili uongozi mpya uundwe na kwa kufuata vigezo vya sifa bora kwa ushindani kuokoa nafsi zetu na Taifa hili kwa ujumla.  Kamati za kudumu za Bunge zilifanya kazi zake vyema kama ilivyo katika hadidu rejea za Kamati zao.

  CAG naye akatumia kalamu yake akiongozwa na kanuni za Uhasibu kuanika madudu yote ya Watendaji wa Serikali kuu na Serikali za mitaa.

  Baada ya majumuisho ya mawasilisho ya Wenyeviti wa Kamati za kudumu za Bunge, Wabunge wote (bila kujali idikadi zao) kwa huzuni na uchungu mkubwa wakawakawaunga mikono hoja kwa 100% juu ya mapendekezo mbalimbali ambayo yote yanajikita katika KUIFANYA SERIKALI IWAJIBIKE KWA AJILI YA MAENDELEO NA SI KUSHIRIKI KUWAIBIA WANANCHI.

  Kuunganisha machungu mioyoni na kwa kuzingatia Uzalendo, mwishoni Zito Kabwe (kwa niaba ya wote wanaolitakia mema Taifa hili) akawasilisha waziwazi pasipo kificho mpango tarajiwa wa kutafuta angalau saini za Wabunge 70 tu ili tuwasilishe Bungeni hoja ya KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU.

  Nami kama Mbunge wa CCM- Mzalendo, sina haja ya kulia lia tu kuwa ninaona sijui kizunguzungu maana nina mamlaka na hivyo nasema nitaweka saini yangu haraka sana. Zito naboresha mkakati huu kuwa. Endapo tutafika 70 basi tunasogea mbele kwa mbele, Waziri Mkuu ajiuzuru na Baraza la Mawaziri livunjwe mara moja. Endapo hazitafika (kitu ambacho hatutegemei), basi majina ya WABUNGE wote ambao hawakuunga hoja huu yajulikane kwa maandishi makubwa ya wino mwekundu na tutayasambaza mitaani kote kwa Wapiga kura waweze kuchambue NI NANI YUKO AU HAYUKO KWA JAJILI YAO WAPIGA KURA ili wao (Wananchi) wajiandae nani wa kupigiwa kura na nani wa kuzomewa 2015.

  Kwa mstakhabari wa Taifa letu, JF Mods tafadhali sana hii thread muiache hapa na wala msiiunganishe na nyingine ili Wabunge wote wasome na kuelewa kuwa sasa hakuna kukalia wigo (sitting on the fence) ! :hail:
   
 2. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2012
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hii lini tena!!
   
 3. j

  jeneneke JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 760
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Nimeelewa 30%
   
 4. F

  Fursa Pesa JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 2,324
  Likes Received: 787
  Trophy Points: 280
  Wabunge wetu wa siku hizi;
  74%=maslai binafsi
  13%=chama chake
  9%= wananchi waolionchagua.
  4%= kwa taifa lake.
  Hapa hakuna uzalendo wowote,siku zote mzalendo ujiwajibisha mwenyewe pale apokosea/kushindwa jambo furani a.k.a kung'atuka.
  a.k.a
   
Loading...