Mbunge mwingine wa CCM ndani ya Nigeria kwa TB Joshua!

Jul 21, 2011
25
3
Wanajamvi naona Edward Lowassa kafungua njia kwa wabunge wa CCM kuzidi kumwagika kwa TB Joshua kuombewa.

Leo kupitia Emmanuel TV inayomilikiwa na Synagogue Church la Nigeria nimemuona Mbunge wa Ngara kupitia CCM Mh. Deogratias Ntunkamazina akifanyiwa maombi maalum akidai kwamba ana matatizo ya shingo na alikuwa hawezi kutembea bila kutumia mkongojo, baadae akasimamishwa akaweza kutembea. Sasa sijajua kama ile ilikuwa ni script ya kuficha kinachowafanya wakimbile Nigeria ambacho wengi tunajua ni kufikiria re-election 2015.

Anaejua perfomance ya huyu mzee jimboni kwake naomba atumwagie hapa jamvini ili tujue kama ni hofu ya kumwagwa 2015 ndo imempeleka huko.
 
Hapo ndipo kwenye ujinga wa ngozi nyeusi, uliona watu walivyokuwa wana-miminika Loliondo kwa dawa ya Lowasa, aliyokuwa kapewa Nigeria kufanyia mazingaobwe!
 
Hapo ndipo kwenye ujinga wa ngozi nyeusi, uliona watu walivyokuwa wana-miminika Loliondo kwa dawa ya Lowasa, aliyokuwa kapewa Nigeria kufanyia mazingaobwe!

Hahaa naona Lowassa kama Bekham, akigusa kitu basi kila limbukeni anakikimbilia. Nahisi waiting list huko Nigeria itakuwa full.
 
Hapo ndipo kwenye ujinga wa ngozi nyeusi, uliona watu walivyokuwa wana-miminika Loliondo kwa dawa ya Lowasa, aliyokuwa kapewa Nigeria kufanyia mazingaobwe!

Duuh sijakusoma vizuri hapo
 
Huyo mbunge wa Ngara ni mgonjwa toka hata kipindi cha kampeni alikuwa India kwa matibabu!
 
Huyu mbunge alipata ajali katika kipindi fulani. Ila vya kuponyeshwa na huyo mchungaji katika kipindi cha sekunde mmmmhhhhhhhh!

Hata yeye msomi anaamini hivyo?
 
Kama anaumwa basi mwacheni ahangaike jamani ila kama ameenda kisiasa basi ajue CHADEMA tunaenda kuchukua jimbo letu 2015
 
Jamani mambo ya imani ni zaidi ya ufahamu wetu, maana ni mungu katikati yetu akijidhihirisha kwa wanaomwamini na wanaoamini katika uweza wake .
Na niseme kwa Mungu/Yesu yote yawezekana pale ambapo ufahamu na uwezo wa mwanadamu unapofika kikomo basi mungu hutenda yale tunaona hayawezekani BUT KAMA unamwamini au unaamini.

KWA hiyo kwa uponyaji unaotoka kwa mungu twaweza kujaribu kuelewa inakuwaje mtu kupona ndani ya dakika au sekunde jibu ni kwamba kwake yeye aaminiye yote yawezekana, aminini tu.

MWisho huyu mb aliyepona ni moja ya mamia wanaopona na waliopona kwa kuombewa na kila siku hushudia matendo makuu ya mungu'

............THINGS OF GOD ARE OF GOD AND THEY HAPPEN IN GODLY WAY AND POWER, so LET GOD BE GOD....
 
Kama anaumwa kwa muda mrefu hata kabla ya uchaguzi si aachie ngazi na apumzike ili wenge afya njema waendeleze libeneke.loliondo imehamia nigeria?
 
Hapo ndipo kwenye ujinga wa ngozi nyeusi, uliona watu walivyokuwa wana-miminika Loliondo kwa dawa ya Lowasa, aliyokuwa kapewa Nigeria kufanyia mazingaobwe!

yahani hawa wazee sijui nini, wamestaafu wakae chini wapumzike hapana. mzee wa miaka 60 eti anaenda kugombea ubunge, unategemea nini hapo? si ajabu huyo kwa babu alienda na sasa maombezi. Du tungoje kinachotokea
 
mbunge asiumwe kidogo hof ya kampen acha ujinga kuumwa ni jambo la kawaida kwa binadamu yyte kwa hiyo mnataka wasifanye tiba kisa tu wataambiwa kuwa ni hof za uchaguz kwel sasa mnakosa vya kuandika
 
mbunge asiumwe kidogo hof ya kampen acha ujinga kuumwa ni jambo la kawaida kwa binadamu yyte kwa hiyo mnataka wasifanye tiba kisa tu wataambiwa kuwa ni hof za uchaguz kwel sasa mnakosa vya kuandika
Na tiba zikishindikana unatoroka bunge unaenda Nigeria kuombewa sio, how classy!
 
aacheni majungu nyie watu msio na aibu. Kila mtu ana uhuru wa kuabudu na kuamini chochote. CDM you are onyo very cheap politics, grow up!Slaa hapo no mlemavu, kesho na keshokutwa tutamwona mahali fulani alitafuta uhai.....tutasemaje? aa
 
Back
Top Bottom