Mbunge mwingine apata ajali gari yaparamia mawe yaliyotegwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge mwingine apata ajali gari yaparamia mawe yaliyotegwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtanzania, May 31, 2009.

 1. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Nafikiri Lowassa alipanga mawe barabarani kwi kwi kwi!!!

  Mbunge mwingine apata ajali gari yaparamia mawe yaliyotegwa

  Ally Sonda na Rehema Matowo, Mwanga
  MBUNGE wa Jimbo la Vunjo, Aloyce Kimaro amenusurika kufa baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kuparamia mawe yaliyopangwa barabarani na kupata ajali usiku wa kuamkia jana.

  Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na Kimaro na polisi zinasema kuwa, ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Mikongeni kata ya Lembeni wilayani Mwanga, Kilimanjaro kwenye barabara kuu ya Moshi-Tanga, akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kwenda jimboni kwake.

  Kwa mujibu wa habari hizo, wakati ajali hiyo inatokea, Kimaro alikuwa na rafiki yake Joseph Temu ambaye ndiye aliyekuwa anaendesha gari hilo aina ya Mercedes Benz akiwa na mkewe na watoto wake watatu. Katika ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa.

  Kimaro alisema baada ya ajali hiyo mfanyabiashara wa Mwanga, Shafii Hasanal alitoa msaada wa kulivuta gari hilo hadi kwenye kituo cha mafuta Kisangara.

  Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Lucas Ng
  'oboko alisema kuwa ajali hiyo ilitokea saa 2:30 usiku, chanzo kikiwa ni mawe makubwa na matofali yaliyokuwa yamepangwa barabarani katika eneo lenye kona na mlima.

  Kamanda Ng'oboko alisema kuwa watu wanaosadikiwa kuwa ni wezi, walipanga mawe hayo barabarani kwa lengo la kusababisha ajali ili kuwaibia abiria.

  G
  ari ya mbunge huyo ilipofika katika eneo hilo likiwa katika mwendo wa kawaida na mbele yao kukiwa na lori ambalo liliweza kuyapita mawe hayo bila tatizo, wao walipojaribu kuyapita tairi la mbele upande wa kulia na 憇ampo?ya gari hilo vilipasuka wakashindwa kuendelea na safari," alisema Ng'oboko.

  Kamanda huyo alisema kuwa miaka ya nyuma eneo hilo lilikuwa na matukio mengi ya aina hiyo ambayo yameanza kujitokeza upya, kwa kuwa awali wananchi wa eneo hilo kwa kushirikiana na polisi walikuwa wameyamaliza.

  Alibainisha kuwa polisi wanafanya operesheni ili kuwadhibiti wezi hao na kuwasaka waliohusika na tukio hilo ili wafikishwe mbele ya sheria.

  Kimaro ni miongoni mwa wabunge waliojitokeza hadharani kupambana na vitendo vya ufisadi. Mwaka jana aliibua hoja bungeni kutaka, Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa ashitakiwe kwa kutumia madaraka vibaya ya kufanya biashara akiwa ikulu.

  Hii ni ajali ya pili inayohusisha wabunge kutokea ndani ya wiki mbili baada ya ajali iliyomhusisha mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe iliyotokea eneo la Ihemi, Ifunda mkoani Iringa.

  Dk Mwakyembe, alinusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Kyela kwenda Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka.

  Ripoti ya polisi iliyotolewa wiki hii ilieleza kwamba ajali hiyo ilitokana na uzembe wa dereva, lakini mbunge huyo ameiponda na kuifananisha na ripoti ya mpiga ramli kwa vile haikuzingatia vigezo na utaalamu katika uchunguzi
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Na kwa kuwa naye Kimaro kapona kutokana na "mpango" kwenda kombo, basi sasa hivi tutaanza kuona madudu ya polisi -- yaani maagizo kutoka kwa Masha kupitia "script" aliyotayarisha kujaribu kuupumbaza umma kuhusu hasa kilichojiri.

  Kinachoshtua ni kwamba kama walikuwa ni majambazi tu wa barabarani (highway robbers), kwa nini hawakuporwa kitu chochote? Na kwa nini mawe yaliondolewa ghafla na watu wasiojulikana? Polepole "umafiosi" unaingia katika utawala wa JK bila ya yeye kuwa na uwezo wowote wa kuzuia kwa woga kwamba atakosa kuula tena mwaka ujao! Hivi anaula nini sasa hivi? Siamini iwapo anauendesha kwa raha na amani ya moyoni huo "urais" alioutaka kwa udi na uvumba -- iwapo wanaotawala ni watu wengine kabisa. Siamini, na ninadiriki kusema hata usingizi anaupata kwa kutumia valium.
   
 3. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  ....Lets be a bit serious guys,i think JF is bigger than that.
  Mods.....tafadhali.
   
 4. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...definately, ila hawa wabunge nao sasa wamezidi. Ajali ni 'halali' kwa wananchi, akipata Mbunge ni jaribio la 'kuuwawa!' ...inaboa!

   
 5. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Kamanda Alfred Ng'ohoboko naye atadai Mh.Kimaro naye alikuwa amelala kama Kamanda Advocate Nyombi wa Iringa alivyodai kuwa Mh.Mwakyembe alikuwa amelala...!!!:(:(:(
   
 6. D

  David Nkulu Member

  #6
  May 31, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inawezekana kuwa hizo ni coincidents tu!
  Hakuna haja ya ku-over react. Cha msingi, wabunge hawa (Kimaro, Mwakyembe) na wenzao wengine waendelee kuwapiga vita mafisadi na viongozi wengine wanaohujumu wananchi na nchi kwa ujumla. Ikiwa pataendelea kujitokeza matukio kama hayo, ambayo kwa sasa hatuna ushahidi wa kujitosheleza (naondoa ujinga wa kamati maalum ya polisi! Ushahidi wa upumbavu wao uko wazi!), basi tutachukua hatua za kujitosheleza!
   
 7. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  ....
  Teh teh teh wacha na wao waonje laza ya maumivi! Acheni kuwadekeza hao wote ni mafisadi tu! Utalipwaje 12m katika nchii bwana! Halafu ujidai unahurumia wananchi? wapangieni mawe, wa chimbieni mashimo, yag0‹2geni na mabenzi yao! teh teh teh
   
 8. K

  KIFULUFUMBI Member

  #8
  May 31, 2009
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli tunampa pole saana lakini tusubiri nguvu ya mafisadi ni kubwa sana na wana act by remote control but with all of their mischievious act and dubious deals time will come and tell them and will be open for even blinds to see the naked truth.haya jamani nashukuru tuendelee kujulishana. Na hapa Morogoro jamaa yetu Lowasa anajenga hotel ya kisasa kwenye eneo la magereza ambapo pana mabwawa ya samaki ya magereza lakini sijui amewezaje kumilikishwa eneo la serikali.ndo hivyo!!!!
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,613
  Likes Received: 2,020
  Trophy Points: 280
  Mtanzania,hata ajali za kupangwa ama mauwaji ya kupangwa huonekana kama ni tukio ama ajali ya kawaida tu,ndio maana hata kama ni mauwaji ya kupangwa,bado neno ajali litakuwa pale pale,ajali husababishwa na mambo mengi,na ni kazi ya mwenye kupanga mauwaji/ajali kuchagua sababu ama means za utekelezaji wa mission ama ajali hiyo based on possiblities of non traceable plans,bado tu itakuwa ni ajali licha ya kwamba imepangwa.

  Na pia utambuwe kuwa issue kama hizo usitegemee kupata very unique situation ama evedence,itasikika tu ni majambazi,bado ni mpango wa mauwaji,lakini bado pia ni majambazi.
  Hata mara nyingi wanaotumwa kufanya mauwaji ni pet criminals tu,miongoni mwa hao vibaka inawezekana kuna anyejuwa anachokifanya.

  Mara ngapi umeshasikia majambazi wamevamia wameuwa lakini hawajachukua kitu? Je kama wakichukua kitu utadai kuna consiparacy ama utaconclude kuwa ni just tukio jingine la "Ujambazi?"
  Uzuri wa hapa si wote wanasiasa.
   
 10. M

  Masatu JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Itakuwa Rostam Aziz kapanga mawe...
   
 11. O

  Ogah JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Really?....sasa mods wanaingiaje hapo......hawa Mods mwaka huu...duuhh
   
 12. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #12
  May 31, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wakuu,

  kweli mimi nimeanza kuchoka na haya ya mkono wa mtu. Mheshimiwa Kimaro alikuwa anaendesha gari lake inaelekea kwa mwendo wa kawaida na madhara yake hayajakuwa makubwa sana. Kwa hili dereva wa mheshimiwa kaonyesha mfano.

  Ifike mahali tujiangalie sisi kwanza kwa kufuata sheria na taratibu kabla ya kuwanyoshea vidole wale wa upande wa pili. Kama unavunja sheria kwa kuendesha kwa mwendo mkali, jilaumu wewe mwenyewe kwanza kabla hata ya kufikiria kuna mkono wa mtu.

  Pia ni kweli polisi wasifanye ujinga kwenye haya mambo ya ajali; njia ya kuua majungu ni kufanya uchunguzi wa kina na ulio sahihi. Kukukurupuka na kuacha mapengo mengi kama kwenye ile ajali ya Mwakyembe kunaweza kuliingiza taifa kwenye maafa makubwa.

  Watu wakishaanza kuamini vichwani mwao kwamba ajali za wanasiasa zinapangwa, wanaweza wakaanza kufanya kweli na kuanza kupanga kuua wanasiasa. Haya mambo yanajengwa na imani kichwani. Ukiona jambo hili linaweza kufanyika kuna watu watajaribu kulifanya.

  Mfano mzuri ni kwa watu wa USA mmeona ile advert ya kumlinganisha rais Obama na hao viongozi wengine ambao wote waliuawa. Dunia ina vichaa wengi, mtu anaweza kutaka umaarufu baada ya kusikia tu jambo linaongelewa.

  Mimi naamini kabla ya kumlaumu mtu mwingine ni muhimu kujiangalia mwenyewe je nimefanya kila kitu according to the rules or spirit of the rules? Kama kuna mambo umekiuka, wewe unakaribisha polisi nyumbani na kwenye hizi nchi za watu, polisi wakija nyumbani watakuta jambo tu.
   
 13. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #13
  May 31, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  error
   
  Last edited: May 31, 2009
 14. s

  skasuku Senior Member

  #14
  May 31, 2009
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kama kuna ukweli kwamba hii ajali inatatanisha, hivi kwa nini hawa walioamua kujitoa mhanga wakupambana na mafisadi hawachukui tahadhari ya kujilinda usalama wao..? Kwa nini safiri usiku, unless safari yake was top secret...

  BInafsi ninaona kutakua na watu watataka kuji publicise kwamba wapo targeted na mafisadi... will do anything kupata kura 2010.....
   
 15. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #15
  May 31, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  hii story naona hapa ni wazembe sasa kimaro na dereva kwani walichukua risk kubwa kupita kwenye hayo mawe baada kuona lori limepita.walitakiwa wajue tofauti ya lori na gari wanayoendesha wao unless kama walikuwa wanaogopa kusimama na kuyatoa yale mawe kuofia kuvamiwa na majambazi .lakini wamefanya kosa kujaribu kupita kwa vile waliyaona yale mawe kabla.
   
 16. M

  Msindima JF-Expert Member

  #16
  Jun 1, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  waunde tume ingine maana ya kuchunguza chanzo cha ajali maana mkubwa akipatwa na jambo tume zinaundwa.Wao hawastahili kupata ajali,wengine ndo wanastahili.
   
 17. fiksiman

  fiksiman JF-Expert Member

  #17
  Jun 1, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 402
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  wacha wafe ndo akili itawarudia na sheria zao butu za usalama. Wewe unaingia bungeni kazi kulala na kusoma magezti tu...muswada wa sheria ukiletwa unaiponda afu unasema naungana mkono mswada. halafu spika anasimama na kuuliza wanaounga mkono wasema ndio na wasiounga mkono waseme hapana...waliosema ndio wameshinda. Nasema wacha wafe tena wote ili watie adabu mbele ya safari.
   
 18. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #18
  Jun 1, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Safari hii kidogo wamejaribu hata kufikiria ila situation at the moment inatisha uko nyumbani alafu hizo lorry ndio kila siku uwepo hapo hapo karibu na matukio, kwanza si yamepigwa marufuku kutembea usiku au? inavyoonekana hayo mawe yalikua upande anoelekea yeye mungu hawa nusuru na aendelee kuwalinda viongozi wetu mashujaa wa kweli.

  inasikitisha kwa sababu hawa watu wana-waume na watoto au wake na watoto ukishatoa bread winners bwana Lowassa nani awasaidie tena familia zao we binti yako ushampa maisha mazuri mpaka kufa.

  swali ni moja watanzania tufanyeje kuwalinda viongozi wetu mashujaa, mimi na amini wako wabunge wengi tu wasiopenda mwelekeo wa madaraka ya sasa serikalini ila na wao ni binadamu na wanafamilia na utakua ni u-selfish in a sense kwa mtu ku-risk maisha yake wakati ana responbilities ya fimilia aliyoileta duniani,. narudia tena hawa jamaa awapo duniani inabidi watanzania tuwajibike, magazati yetu yatoe ruksa ya kuwapa publicity ya kutosha viongozi wetu wanaopigana na ufisadi. nadahani sasa muda umefika wa wakazi wa dar-es-salaam kuandamana ikulu na wakazi wa dodoma kuandamana bungeni sauti yetu lazima isikilizwe wengi wapewe. aiwezekani mtu mmoja mwenye busara za uchoyo (EL) na rais mmoja mpuuzi watishie maisha ya viongozi wetu hivi. kwa sababu ya, maslahi ya wachache. Wasituondolee watu amboa wanaweza kuwa washauri mpaka kwa viongozi wa miaka ishirini ijayo kwa sababu ya ufisadi wao.

  Mungu Ibariki Tanzania
   
Loading...