Mbunge mwenye Uzalendo ni yule nitakayemuona pamoja na mambo mengine, akipigania Fao la Kujitoa, kwa ukombozi wa waajiriwa wa sekta binafsi

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,776
2,000
Hakuna mtu muelewa na mpenda haki asiyetambua kwamba Serikali imefanya ukatili wa Hali ya juu kwa kitendo cha kuondoa fao la kujitoa katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

Ipo idadi kubwa sana ya Watanzania ambao wameajiriwa katika sekta binafsi, na kama tunavyofahamu, mara nyingi sekta binafsi hazina mikataba ya kudumu kama ilivyo kwa Serikali, hivyo basi mtu anaweza kufanya kazi miezi kadhaa, mwaka, miaka kadhaa na mkataba wake ukafika kikomo.

Lakini kwa sheria mpya ya fao la kujitoa, mtu huyo huyo mkataba wake ukimalizika hataweza kupata pesa yake yote ya pensheni bali sheria inamlazimisha asubiri kufikisha umri wa miaka 60 hata kama mkataba umeisha akiwa na miaka 20 au 30😀😀😀 (what a joke)
Tunatambua kwamba lengo la Serikali ni kupora pesa hizi ili zitumike kwenye miradi ya Serikali.

Huu ni unyanyasaji mkubwa. Sheria kandamizi kama hii zinapaswa kufutiliwa mbali na wapenda haki wote bila kujali itikadi za kisiasa.

Wabunge wengi pamoja na kwamba wengi wao wana umri mkubwa hii sheria ingekuwa inawahusu kwenye mafao yao, sidhani kama wangekubaliana na upuuzi huu.

Ifike hatua wabunge mpiganie kile mnachokiamini huku mkiacha unafiki pembeni, na hapa ndipo nitakapomuona Mbunge mzalendo na mwenye nia ya dhati.
 

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
24,318
2,000
Zamu hii wote walioingia bungeni wanajalia maslahi yao hamna mbunge kwenye uchungu bunge la sasa
 

mzabzab

JF-Expert Member
Aug 18, 2011
10,599
2,000
Yaani wanadhani watu tuna mkataba na Mungu....unaweza dedi kabla ya hiyo 60
 

papason

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
3,808
2,000
Wapo wafanyakazi na watumishi wengi tuu walio tetea na kufurahia wizi wa kura na udanganyifu uliofanywa na jiwe na genge lake, sasa tunaenda umia wote, tena mnyamaze kimyaa kabisa tuibiwe mazao yetu vizuri.
 

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,776
2,000
wapo wafanyakazi na watumishi wengi tuu walio tetea na kufurahia wizi wa kura na udanganyifu uliofanywa na jiwe na genge lake, sasa tunaenda umia wote, tena mnyamaze kimyaa kabisa tuibiwe mazao yetu vizuri ……………..
Wapo lakini siyo wote mkuu
 

MoseKing

JF-Expert Member
Jul 5, 2017
1,632
2,000
Ni sheria ya kipumbavu na ya kikoloni sana
Tena kibaya zaidi Tanzania imekuwa ya system mbili.

Yaani sheria inatungwa kwaajili ya watu fulani tu.

Sheria ya mafao haiwahusu wabunge na watawala.

Kilichofanyika ni Rushwa, walipewa muswada wa kikandamizaji wapitishe Kwasababu wao kama wabunge hautawahusu.

One Nation. Two Systems.
 

B'REAL

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
4,054
2,000
Mkuu amini maneno yangu hakuna mbunge anaeweza kuongelea hili Jambo,wote niwachumia tumbo nawao hiyo sheria haiwabani
 

Akili 2

JF-Expert Member
Jul 2, 2018
780
1,000
Ndiyo maana nasemaga kwa Tanzania kufanya kazi ni kupoteza mda tuu bora ujiajili tuu upatage hata 80,000 au laki au laki na nusu kwa siku kuliko kufanya kazi ,unakuwa uko smart mda wote na salary ulipwe laki 8 harafu ukatwe
1.Paye
2. Nssf
3.Wcf
4.Bima
5. Chama Cha ujinga ujinga mfano Cwt kwa walimu
6.Hslb
7.crdb mkopo ,ulichukuwa kununuwa IST au Vtz
😂😂😂 Sasa ujinga gani huo mtu unazeeka ety unasubili pension ndiyo ujenge na uanze biashara
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom