Mbunge Mwambalaswa (jimbo la Lupa Chunya)

RubenM

Senior Member
Apr 15, 2009
131
10
:eek: Ni uvumi au kweli kuhusu mbunge wa jimbo la lupa katika wilaya ya chunya mkoani Mbeya? mbunge wa zamani wa jimbo hili Kasaka anaandaa makombara ya kum-defeat Mwambalaswa ili arudi tena DODOMA..
 
Kama kazi yake kupiga domo Dodoma kule kwake kunaangamia, ni wazi wengine watakuja na wanaweza kunyakua jimbo lake. Mtu mchapa kazi hata siku moja hawezi kuhofia wanaotaka kugombea jimboni kwake. Hakuna mwenye hati miliki, hivyo wambeya wa JF tuombee tu itokee mipambano ya nguvu na watu kudondoshwa.
 
:eek: Ni uvumi au kweli kuhusu mbunge wa jimbo la lupa katika wilaya ya chunya mkoani Mbeya? mbunge wa zamani wa jimbo hili Kasaka anaandaa makombara ya kum-defeat Mwambalaswa ili arudi tena DODOMA..

Mi nadhani Kasaka anajisumbua kama ni kweli anafanya hayo, maana hata wakati uliopita alifanya juhudi kubwa ili arudi bungeni kupitia sisi Maf... na aliposhindwa kura za maoni alikimbilia upinzani lakini akabwagwa! Na amerudi sisi Maf... akidhani itamwia rahisi. Anajidanganya maana enzi zake zaisha ivo! akae atulie kama hakupiga hesabu vizuri kwa zile 12 m alizokuwa akipata plus marupu rupu ya 20 m aliyopata mwishoni basi, kwa sasa amechelewa.
 
Kasaka is history! Alicheza vibaya karata zake na kwa kuhamia upinzani amejionyesha kuwa ni mtu wa kupenda madaraka tu na si chama chake (CCM au chama alichohamia)wala wananchi wa Chunya.
Oppurtunists hawajawahi kufanikiwa, na oppurtunity ikipita baada ya hapo ni maigizo tu.
Anajisumbua.
 
d

Unaongea kama hukijui hicho chama. Hebu taja mtu mmoja hapa ambaye si opportunist ndani ya sisiemu. Kwa chama cha majambazi lolote linawezekana. Yule kada wa NCCR nsanzugwanko sasa hivi si ni mbunge? Kwa nini isiwe Kasaka? Kama amezikusanya pesa za kutosha kuhonga na ameshaanda mabawser yenye maji taka ya kutosha kumchafua mtu yeyote atakayekuja mbele yake achilia huo Mwambalaswa basi atarudi tu mjengoni.
 
Mkuu watu kama jamaa uliyemtaja hapo juu ni kama mamluki.Hawaaminiwi na mtu yeyote.Fuatilia sana wanishia kubeba mafaili tu.Cheki kina Tambwe Hiza na wengine, hela zao zitaliwa lakini kuaminika hapana.
 
Kwani huyo Mwambalaswa amelifanyia nini jimbo lake na hata kustahili kutokupingwa na wanachama wenzake? Je, Chunya ni Kasaka na Mwambalaswa tu?
 
Namkubali sana Mwambalaswa, bila shaka hata wapiga kura waker kule Chunya wanamkubali. Napenda wabunge wanaosema ukweli, hasa katika kujadili ufisadi unaoliangamiza taifa letu. Huyu huwezi kumlinganisha na Kasaka ambaye in my opinion ni spent force.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom