Mbunge Musukuma: Ukiwatoa machinga Mtaa wa Congo biashara imekufa. Asema pamoja na Mwigulu kumtaja tajiri yeye ni zao la machinga

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,441
7,778
Mheshimiwa spika, nitalisema kwa upole sana suala la machinga maana nikizungumza kwa ukali nitasemwa mimi sio mtanzania lakini nilivyolisea mwanzo nahisi watu hamkunielewa. Niliposema niliambiwa mimi ni mrundi sio Mtanzania.

Mimi natoka vijijini na ni mkulima wa mpunga, gunia la mpunga ndani ya mwezi mmoja limeshafika elfu 90 na wiki mbili tatu tulikuwa tunauza elfu 40/50, mchele umepanda hapahapa ndani kwetu.

Nimefanya karesearch kulingana na akili yangu, walazi wa mchele wameongezeka, wauza viazi vya chips wanalia vimeoza hamna walaji. Tulizoea manaansi wananunu machinga wanakatakata wanawauzia watu 200 linanunulika, sasa hivi hayanunuliki.

Watu wamerudi kwenye wali, tunakula unabakiza na kiporo cha chai. Mtoto anatoka Mbagala anasoma shule ya Uhuru, unampa kaelfu anakula kachips kake kwenye nailoni.

Sasa hivi wamachinga wote wamefurumushwa mnataka watu wote wakale kwenye restaurant, mimi nilielewa kabisa Rais alivyosema tukawaandalie mazingira mazuri.

Nina duka Kkoo siku ya 7 sijauza, fikiria mfanyakazi nilikuwa nampa posho ya chakula 3000 leo anatakiwa akale restaurant chai 2000, mchana 5000 nitatoa wapi? Kila anayefungua duka ana mfuko una hotpot, Watu wanakuja na makande na wali wa kiporo, haiwezekani kuhudumia kwasababu hatuuzi.

Waziri wa fedha jaribu kuliangalia na bahati nzuri umenitaja maana wewe ni waziri wa fedha inawezekana una takwimu vizuri kwamba mimi ni tajiri, mimi ni zao la machinga, machinga wapo aina tofauti, kuna machinga anashinda mlangoni kupiga debe anakaribisha anapata 2000, usifikiri watu wote wana mitaji na hao wenye mitaji ndio wanawezesha machinga, huwezi kutenganisha, ukiwatoa machinga Congo biashara imekufa.

Mbunge Musukuma

Pia Musukuma ameongelea ukamilishaji wa miradi kwani miradi ipo mingi ambayo huwa haifikishi mwisho akitolea mifano kwenye majengo kwenye halmashauri akitolea mfano vituo vya afya vilivyoishia kati huku wanaanzisha ujenzi wa vingine.
 
Kumbe ana duka ndio maana analia lia. Kodi halipi kwa kujificha kqa machinga.

CCM mbere kwa mbere
 
Hivi vijana wote vijijini wakihamia mijini kufanya umachinga miji itakuaje? Msukuma fikiri kidogo. Kumbe kelele yote ya kutetea machinga wasiondolewe mitaani una maslahi nayo.
 
Msukuma aache sound, huyu jamaa yeye kila kitu anajua, basi anawadanganya wenzie mle mjengoni.
 
Kabla ya machinga kuruhusiwa huo mtaa ulikua hauuzi? Hamia huko huko machinga walikohamishiwa hawajafukuzwa wamehamiahwa.
Kama anaona mambo yake hayaendi ahamia burundi. Ngoja kwanza 2025 ubunge hapati.

Atachanganyikiwa hadi avue nguo
 
Nina duka Kkoo siku ya 7 sijauza, fikiria mfanyakazi nilikuwa nampa posho ya chakula 3000 leo anatakiwa akale restaurant chai 2000, mchana 5000 nitatoa wapi? Kila anayefungua duka ana mfuko, Watu wanakuja na makande na wali wa kipor...
Biashara ilikuwepo mtaa wa Kongo hata kabla ya wamachinga na itaendelea kuwepo baada ya wamachinga. It is a matter of choice tuifanye Dar es Salaam iwe na hadhi kwa usafi kwa kuwatafutia wamachinga location mbadala au kuwaacha wakazagaa kila mahali na kulifanya jiji chafu
 
Waendelee kubeba viporo kwanza itawasaidia kubana matumizi, mazingira lazima yasafishwe.
 
Msukuma mwongo sana jamani khaa!!

Pale Congo wanafanya biashara wamachinga??

fukuzia mbali hao wachafuzi wa mazingira.
Kauli za waajiriwa bana..unaongea kana kwamba hao wamachinga ni takataka yaani!!

Hili swala linapaswa kushughulikiwa kistaarabu maana mnaposema fukuza hao wachafuzi kumbuka hao unaowashauri wafanye hivyo ndy wametengeneza mfumo wa hii nchi kuwa nchi ya wamachinga..watafanya nn wakati mmeua kilimo Kwanza na kuwatelekeza,waacheni wakimbiile mijini kuja kufanya umachinga,maana ndy option waliyo nayo

Matokeo yake mnawavunjia usiku usiku kukwepa makamera na mmewapiga mkwara wanahabari huku mkipandikiza propaganda kwamba zoezi linaenda smooth wamachinga wote wamekubali kuhama bila tatizo,kwamba hao wanaoleta Fujo ni wahuni wachache ambao siyo wamachinga..mmekurupuka


Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Inamaana wamachinga ndiyo walikuwa wanamuuzia vitu. Kwamba alikuwa anakwepa kodi. Kama ni hivyo ni jambo zuri wameondolewa.
 
HUYO MZUSHI TU ACHA SERIKALI IREKEBISHE PALE AMBAPO ALIEPITA ALIHARIBU
 
Akili ya Musukuma ni ndogo sana! Sasa hayo maelezo yana pointi gani? Sheria itungwe angalau Mbunge awe amehitimu Form Four hata kama ana Division Zero sawa tu!
Lakini akaepo kwenye kuta za sehemu inaitwa Sekondari.
 
Back
Top Bottom