Mbunge Musukuma akataa kuiacha simu yake ya miaka 10, asema hataki ulimbukeni

Ukitazama comments za humu kuhusu hii Habari ndio utajua kuwa sote tu madikteta isipokuwa wengine wanatumia silaha kuzima habari zisizo pendeza na wengine wanatumia matusi na kejeli

Kila mmoja ana chuki kali dhidi ya aliyetofautiana naye.......

Suala la kutumia vitu vya zamani ni suala la kawaida sana.....lakini kwa kuwa limeletwa kwenye siasa limekuwa jambo la ajabu na lenye kushangaza.........
 
Dah sioni ajabu kutumia Simu za zamani kama hizo hata mimi Nina broo wangu anayo simu flani ya Nokia huu ni mwaka wa 10 na zaid hadi leo anayo na haijafanya tatzo lolote kwahiyo ni mambo ya kawaida tu ns utunzaji pia. Mimi pia nilikuwa ninayo simu ya Nokia nillinunua 2009 kariakoo Ila ikanipotea 2015 na ilikuwa IPO vizr kabisa. Yaan hadi Leo hii naikumbuka kwahiyo utunzaji tu ikiwa ni mzur unaweza ukakaa na simu au kitu chochote kwa kipindi kirefu bila yakuleta usumbufu.
 
Mbunge wa Geita, Musukuma Kasheku amesema anafurahia kutumia simu yake ya mkononi ya zamani iliyofungwa na rubber band.

Sababu ni kwamba hataki ulimbukeni,
si fisadi na hapelekwi na mihemko ya fasheni.

Ona simu yake kupitia video chini


Very primitive! ushirikina mtupu!.Anamdanganya nani na kwa faida ya nani? ukifatilia hako katochi ndani utakuta ni tunguli na hirizi tu zimebandikwa
 
Hahaaa kwahiyo wapiga kura wake nao wanamiliki makatapila /skaveta na pia wanamiliki malandcruiser?
 
ni aina fulani ya ulimbukeni kufukuzana na fashion za simu kila zinapotoka mpya na kutupa za zamani zikiwa bado zinafanya kazi.

lakini ni majanga makubwa zaidi kushindwa kubadilisha back cover ya simu mpaka unafunga na rubber band, huyu mtu hataweza kuwasaidia watu wake kwa vile hataona umuhimu wa serikali kuratibu ukarabati wa majengo ya shule, mabarabara, vifaa vya hospitali, madaraja, vyombo vya usafiri n.k. n.k.

Na sababu ya kufunga rubber band anasema ni fundisho kutoka kwa wazee wa zamani ambao walikuwa chungu kikivunjika wanatumia upande ulio mzima. Ambayo ni ujima, kukosa busara, na hatari, unaweza kula vipande vya chungu, unaweza kukatwa mdomo na ncha kali. Ni ishara ya mtu asiyependa maendeleo.

Kasema simu yake inafafana na elimu yake, lakini kama elimu yake ni ndogo kiasi hiki basi hafai, manake hata mtu wa kawaida wa darasa la saba huwa anaona umuhimu wa kubadilisha back cover ya simu.
 
Mazoea yana tabu yake! Siwezi kumshangaa,ameizoea kiasi kwamba anaona tabu kuacha kuitumia. Hapo mpaka ipotee au iharibike kabisa
Ht mm ninayo yangu, Nokia105 ya kitochi nlinunua 2008....japo nina cm zngne mbili za smart lkn hii siiachi labda ipotee au iibiwe, naip3nda sana!
 
Mbunge wa Geita, Musukuma Kasheku amesema anafurahia kutumia simu yake ya mkononi ya zamani iliyofungwa na rubber band.

Sababu ni kwamba hataki ulimbukeni,
si fisadi na hapelekwi na mihemko ya fasheni.

Ona simu yake kupitia video chini


Cheap politics, mbona anamiliki mabasi na ma trekta hajaitwa fisadi.
Asiseme ulimbukeni ni kumiliki simu kali maana huwezi endelea ng’ang’ania technology ya miaka ya 90 wakati leo ni 2018 unless kama hiyo technology haikuhusu
 
Back
Top Bottom